Kapteni David Nikols ambaye alikuwa mkuu wa wilaya mbalimbali nchini wakati wa zama za utala wa Ukoloni wa Kiingereza kabla ya Tanganyika kujipatia uhuru wake mwaka 1961.
KAPTENI David Nikols ambaye ana umri wa miaka 90 hivi, ni miongoni mwa wakuu wa wilaya za Tanganyika kuanzia mwaka 1948 hadi 1961 nchi ilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza.
Hivi karibuni nilikutana na kapteni Nikols mjini Moshi akiwa bado mwenye nguvu na kutoa wosia, mojawapo ni kuwataka kujiuliza kama kweli wanafanya ipasavyo katika kukuza uchumi wan chi…kwamba kila mtu awe chanzo cha mabadiliko anayotaka kuyaona nchini hasa kwa kufanya kazi kwa bidii.
Alikuja nchini mahsusi kuweka shada la maua katika mnara wa kumbukumbu ya mashujaa uliopo mzunguko wa magari wa YMCA mjini Moshi kama ishara ya kuwakumbuka mashujaa duniani.
Aliweka shada hilo kutambua mshango wa wanajeshi wa Tanganyika waliokuwa katika Jeshi la King Riffle Army (KRA) waliopigana vita kuu ya pili ya Dunia (1939-1944) na ile ya Uganda 1978-1979.
Baada ya kumalizika kwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia (WWII), alikwenda nchini Kenya, Burma na baadae akapangiwa kazi kama Kaimu Mkuu wa Wilaya Singida mkoani Singida 1948.
“Nilifanya kazi Singida na baadaye nikawa DC hapa Moshi, Handeni, Maswa, Njombe, Geita na baadaye nilimalizia Kisarawe mwaka 1961 baada ya Tanganyika kujipatia uhuru wake,”anasema Nikols.
Anaongeza kusema ”Wakati huo nikiwa naishi Tanganyika popote nilipokwenda niliwapenda sana wenyeji na kujitahidi kuinua hali zao kuanzia shule, hospitali, elimu, barabara, kuwafundisha kilimo na hata kufukuza wadudu aina ya ndorobo”.
Kapteni Nikols anayeongea Kiswahili fasaha anasema ilipotokea uhuru mwaka 1961, Mwalimu Jullius Nyerere alimwandikia barua akimuomba aendelee kufanya kazi kwenye serikali mpya.
“Nilitaka lakini mke wangu aligoma akisema watoto wetu walikuwa wadogo hivyo tulipaswa kuwapeleka Ulaya ili wakaanze shule, hivyo ikabidi tuondoke. Kwa sasa nafanya kazi ya kufuga kuku na nguruwe kule nyumbani Uingereza,”anasema.
Watanzania wazingatie kazi
Akatoa wosia kwa Watanzania kuwa ili waishi maisha mazuri wahakikishe wanafanya kazi hadi wafikie umri wa miaka 80 au hata zaidi, kwani kufanya kazi sio tu kwamba kunaingiza kipato, bali ni mazoezi na humfanya mtu kuwa na afya njema.
Akatoa wosia kwa Watanzania kuwa ili waishi maisha mazuri wahakikishe wanafanya kazi hadi wafikie umri wa miaka 80 au hata zaidi, kwani kufanya kazi sio tu kwamba kunaingiza kipato, bali ni mazoezi na humfanya mtu kuwa na afya njema.
“Jamani wosia wangu kwa Watanzania msiache kufanya kazi upesi, kazana kufanya kufanya hata kama unafika umri wa miaka 80, utakuwa ni mtu mwenye maisha ya furaha…. msikimbilie kustaafu mapema haifai,”anasisitiza Nikols.
Anailinganisha Tanzania ya leo na ile ya ukoloni, anaona yapo maendeleo makubwa yamepatikana na hasa katika elimu, afya, miundombinu ya barabara na utulivu na amani.
Nyerere na mpango wa Kiswahili kwa wote
“Tabia za watu wakati ule ndizo zilizonivutia, walikuwa wapole wastaarabu na waliotulia….Tabia za Watanzania leo msingi wake ni Julius Nyerere na yeye ndiye muasisi wa amani yenu leo,”anasema na kuongeza kuwa Watanzania waendelee kushirikiana.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment