ANGALIA LIVE NEWS

Friday, April 19, 2013

Mtuhumiwa amekamatwa akiwa hai wamemkuta na majeraha kwenye mguu na polisi wanaangalia kama ana mabomu ameficha alipokua amejificha. Pia wamethibitisha ndiye mtuhumiwa #2 waliokua wanamtafuta,  sasa hivi wanampeleka Hosipitali kwa matibabu chini ya ulinzi mkali na hii ndio mwisho wa hekaheka iliyaonzia jana saa 4 usiku ET. Kwa sasa Polisi wanazunguka eneo alilokuwa amejificha, wanachunguza kama kuna mabomu  ndani ya boti alikojificha Mtuhumiwa huyo wa Milipuko ya Boston Marathon mjini.
----------------------------------------
Kabla ya kukamatwa. Mtuhumiwa #2 alikuwa amejificha uani ndani ya boti kwenye nyumba iliyopo Mtaa wa Franklin, mji wa Watertown. Polisi walifyatua risasi kadhaa huku wakijaribu kumpata akiwa hai. Mapema mtuhumiwa wa kwanza ambaye ni kaka yake aliuwawa mapema leo baada ya kujaribu kutoroka na gari waliyoipora kutoka kwa mkazi mmoja wa mji huo wa Watertown uliopo maili chache kutoka Boston
-------------------------------------
Polisi waliingia ndani ya nyumba kuwatoa wenye nyumba ambao walikua hawaongei kiingereza kizuri na hawakutaka kuongea mbele ya kamera za TV. Polisi walijaribu kumshawishi aweze kutoka lakini mtuhumiwa huyu #2 hakujibu chochote na bado ilikuwa haijathibitika moja kwa moja kama ndio yeye wanaemdhania yupo nyuma ya Boti.

Hii nyumba ndio aliyokua amejificha mtuhumiwa # 2 wa milipuko ya mabomu Boston marathon, mtuhumiwa alikua amejificha ndani ya hiyo boti unayoiona hapo nyuma ya hii nyumba.

Polisi walipokua wakiendelea na msako mkali wa mtuhumiwa #2 kwenye mji wa Watertown, Massachusetts.

Msako ulikua mkali sana.

Polisi wa vikosi vyote wakipita kila nyumba kumtamfuta mtuhumiwa #2.

Mjomba wa watuhumiwa anayeishi DMV akiongea na waandishi wa habari.

Vikosi vya polisi vikiongezwa.

2 comments:

Anonymous said...

Go America!!!! Great Job!! Beautiful Job!!! Gof Bless America.

Anonymous said...

god bless africa na North korean uzushi huu wanampakizia jamaa