ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 3, 2013

WAHUSIKA GHOROFA LILILOPOROMOKA DAR WAPANDISHWA KIZIMBANI

Mkandarasi Raza Hassan Raza akiinama tayari kusujudu baada ya kufikishwa mahakamani.
Akiwa kaifikia ardhi kwa ajili ya kusujudu.
Juu na chini Askari akiwaongoza watuhumiwa mahakamani
Raza akivuta uradi
Watuhumiwa (waliokaa benchi la mbele) wakisubiri kusomewa kesi yao.
Raza Akiongea na wakili wake.
Wakirudishwa mahabusu baada ya kukosa dhamana.

MKANDARASI wa jengo la ghorofa 16 lililoporomoka Ijumaa iliyopita na kuua watu kadhaa kwenye Mtaa wa Indira Gandhi jijini Dar es Salaam, Raza Hussein Raza, na wenzake 10 leo wamepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini.
Washitakiwa hao wamesomewa mashitaka 24 ya kuua bila kukusudia. Katika kesi hiyo mawakili wa upande wa utetezi waliwapigania wateja wao kupata dhamana lakini upande wa mashitaka ulipinga ombi hilo na kuzua mjadala mzito ulioshindwa kupatikana suluhu.
Washitakiwa wamerudishwa rumande mpaka kesho kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.

(PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL)

10 comments:

Anonymous said...

Askari wetu wa jeshi la polisi wanapokuwa na nguo za ki raia ni vigumu kuwatofautisha na majambazi. Nashauri wavau uniform wanapokuwa kazini. Kama wanavaa ki raia basi waongeze bullet proof zenye maandishi POLISI mgongoni.

Anonymous said...

Ni kweli kabisa mtoa maoni wa April 3,2013 at 12:55 pm. Nakuunga mkono kabisa kwa hilo wazo lako.

Anonymous said...

Wakaguzi majengo kutoka Wizarani au Halmashauri ya jiji nao wamefikishwa mahakamani? Nao wananhusika asilimia 100.

Anonymous said...

ALLAH ATAKUSAIDIA RAZA INSHALLAH

MDAU NEW YORK

Anonymous said...

My name is Skeptic. I have several comments to make regarding a sixteen-storied building and its aftermath. It is a good gesture that the government is trying to do something to please the the public. But be assured that money talks, and only scapegoats will be arraigned, unfortunately! I believe this is a scandal that goes beyond the chief architect or engineer. Call me skeptic, but I will really like to see the big fishes on trial and be prosecuted to the fullest extent of the law [which is my wishful thinking].
Oh, as for unmarked poor cops? They look horrible---from head to toe! I couldn't have said better than the previous writer put "you can't distinguish them from armed criminals". They need serious grooming, man ¡¡

Anonymous said...

My name is Skeptic. I have several comments to make regarding a sixteen-storied building and its aftermath. It is a good gesture that the government is trying to do something to please the the public. But be assured that money talks, and only scapegoats will be arraigned, unfortunately! I believe this is a scandal that goes beyond the chief architect or engineer. Call me skeptic, but I will really like to see the big fishes on trial and be prosecuted to the fullest extent of the law [which is my wishful thinking].
Oh, as for unmarked poor cops? They look horrible---from head to toe! I couldn't have said better than the previous writer put "they can't be distinguished from armed criminals". They need serious grooming, man.

Ahsante Babu (DJ). Weka kitu hicho

Anonymous said...

Huyu mkandarasi kaua watu 36 na kusababisha hasara ya mabilioni, atafungwa tu kwa uzembe hata akisali vipi na kushika hilo likitu. Nikiangalia picha ya jengo na mabaki inaonekana nyumba imenyimwa cements na nondo ni kama za kujenga nyumba zisizo za ghorofa. Huyu arudishwe kwao Pakistan hafai kuwepo nchini kwetu, hao ndiyo wanaoharibu nchi yetu. Wote waliohusika wafungwe! wasilipe faini.

Anonymous said...

kwani wewe mungu anonymous wa mwisho unataka kumuhukumu huyu mkandarasi? kwani yupo peke yake? rome vatican ilijengwa siku mmoja?

nyinyi si mnaita rozari sisi tunaita TASBEEE, nakuelimisha ili uelimika next time usiwe juha wakuja hapa katika blog na kutuchafurilia hali ya hewa kwa fikra zako finyuuu.

jiulize haya maswali hapo juu na ujipe majibu

kweli kauwa lakini peke yake? na yeye alikuwa akibeba zege etc peke yake

mungu tu ndo atakaye muhukumu na mungu ndo atakaye mponya kwa janga hili so labda wee pagani huni dini ndo maana unaona na kushanga mtu akimuomba mungu wake na kutubia makosa yake unaona hawezekani
kwani umemuumba wewe na wewe mungu

kuwa mstaarabu na mwerevu na mfikirii wa kina si mfikiriwa wa domo kaya

Anonymous said...

MDAU WA MWISHO MTOA MADAA HLO LIKITU LINAITWA TAASBEE NYINYI MNAITA ROZAREEE AU SIJUI HUNA DINI WEWE

NATAKA KUKULIZA JE WEWE NI MUNGU UNAUWEZO WA KUMUHUKUMU HUYU MKANDARASI?

MUACHIYE ANAMUOMBA MUNGU WAKE YEYE NDO ATAKAYE MJIBU UBI NA DUA ZAKE SIYO WEWE ETI ATAFUNGWA WANGAPI MAFISADI WAME UWA NA WAKO NJE

YEYE SI WA MWANZO WALA SI WA MWISHO

MUNGU AWALAZE PEMA PEPONI MAREHEMU NA MUNGU AMSAMEHE KILA MKOSA ANASTAHILI KUSAMEHEWE NA IMANI YA MUNGU SI YAKO WEWE MDAU WA MWISHO MTOA MADAA

Anonymous said...

we mdau wa mwisho heshimu dini za wenzako wee akhaaa mbona hivyo au mteja wewe