Washishiriki Miss Utalii Tanzania 2013-ktk ziara ya mafunzo mto Wami- walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan Juzi(Photo kwa hisani ya Miss Demokrasia Tanzania
Miss Utalii Tz 2013 baada ya kuwasili Mikumi jana
Washishiriki Miss Utalii Tanzania 2013-ktk ziara ya mafunzo mto Wami- walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Saadan Juzi
Miss Utalii Tz wakiwa Udzungwa baada ya kupanda mlima
Gari la Warembo likiwa limenasa katika hifadhi ya Saadan
Baada ya kuahirisha kambi ya Miss Utalii Tanzania 2012/13 kambi hiyo imeanza upya kwa kishindo kwa washiriki wote kufanya Ziara katika hifadhi za Taifa za Saadani National Park, Udzungwa National Park na Mikumi National Park.
Wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Saadani washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walipata nafasi ya kutembelea vivutio mbalimbali vinavyo patikana katika hifadhi hiyo pamoja na Kutolewa kwa Tuzo mbili ambazo ni Tuzo ya hifadhi za Taifa (National Parks Award) pamoja na Tuzo ya Utalii wa ndani ya Nchi (Domestic Tourism Award).
Maeneo waliyo Tembelea ndani ya Saadani National Park ilikuwa ni pamoja na Kutembelea mbuga ya wanyama ndani ya hifadhi ya Taifa ya Saadani ambapo walijionea Swala wa aina mbalimbali,Twiga pamoja na wanyama wengine mbalimbali, Baada ya hapo washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walipata nafasi ya kutembelea Kijiji cha Saadani na Kujionea Shughuli mbalimbali zinazo endelea katika eneo hilo.
Habari na picha zaidi bofya read more
Siku iliyo fuatia Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walipata nafasi ya Kutembelea Mto Wami ambao ni Maarufu kwa kuwa na Mamba wengi pamoja na Viboko, ulikuwa ni utalii wa Boti, wakiwa Ndani ya Mto Wami washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walijionea Mamba wakubwa pamoja na Viboko, wengi wao walionekana wenye furaha na kushangaa kwa sababu asilimia kubwa ilikuwa ndio mara yao ya kwanza kuwaona wanyama hao, vile vile washiriki walipata Bahati ya kuona makutano ya Mto Wami na Bahari ya Hindi.
Usiku wa siku ya pili washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walionesha Show ambayo iliambatana na utoaji wa Tuzo za Kitalii ambazo ni Tuzo ya Utallii wa Ndani ya Nchi (Domestic Tourism) ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Katavi, na Tuzo ya Hifadhi za Taifa Tanzania (National Park award) iliyo chukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Lindi. Utoaji wa Tuzo hizo uliambatana na Burudani kabambe ya Ngoma za asili kutoka kwa Washiriki hao ambapo walikonga nyoyo za wakazi wa Saadani waliofika katika eneo la tukio.
Akizungumza Baada ya kutoa Tuzo, Mhifadhi wa Saadani National Park Ndugu Mwakapaje alisema kuwa amefurahishwa sana na ujio wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 ambapo kwao wameona ni Heshima kubwa kwa washiriki hao kutembelea katika Hifadhi yao ya Taifa ya Saadani, aliongeza kuwa huo ni uzalendo na ni njia nzuri ya kuutangaza utalii wa ndani ya nchi yetu ya Tanzania hasa Saadani National Park.
Washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 waliendelea na Ziara yao ya Kutembelea Hifadhi za Taifa na kuelekea Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa(Udzungwa National Park) washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walipata nafasi ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa na kupanda Mlima ambapo walitumia muda wa zaidi ya masaa mawili,wakiwa huko washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walijionea Misitu mikubwa, walijionea Maporomoko makubwa ya maji, pia walijionea baadhi ya viumbe mbalimbali wanaopatikana katika Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa.
Ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Udzungwa washiriki wa miss Utalii Tanzania 2012/13 walipata nafasi ya kufanya michezo mbalimbali ndani ya Maji, Kuogelea pamoja na kucheza ngoma za asili. Washiriki wote walifanikiwa kupanda mlima na wote walirejea salama.
Baada ya kumaliza Ziara ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya Udzungwa, washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walimalizia Ziara yao ya kutembelea Hifadhi za Taifa kwa kutembelea Mikumi National Park.
Wakiwa Mikumi National Park, washiriki wa Miss Utalii Tanzania walipata nafasi ya Kutembelea mbuga ya wanyama na kujionea wanyama mbalimbali wakiwa ni Simba ambao waliwafurahisha washiriki wengi kuona Simba wakiwa Juu ya miti na kushuhudia Simba akiwinda Swala, wanyama wengine walio waona ni Twiga, Tembo ambao walikuwa katika makundi, Nyati waliokuwa katika Makundi makubwa ya zaidi ya mia tatu, Swala pamoja na Punda milia, zaidi ya Hapo washiriki wa Miss Utalii Tanzania Walipata nafasi ya Kutembelea Bwawa la Viboko na Mamba.
Wakiwa Bado Mikumi National Park washiriki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walifanya Show kubwa ambayo ilikuwa ni ya utoaji wa Tuzo Mbalimbali za utalii ambapo zilitolewa Tuzo 12, kabla ya kutoa tuzo washirikiki wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 walikonga nyoyo za watu wa Mikumi National Park na baadae Tuzo hizo kutolewa.
Tuzo ambazo zilitolewa ilikuwa ni pamoja na Mikumi Conference Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Dar es salaam 2, Cultural Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka mkoa wa Simiyu ,Marine Park Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Mtwara, Forest Services Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka kutoka Vyuo vikuu, Mount Kilimanjaro Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Kilimanjaro,Ngorongoro Crater Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Dodoma, Sports Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Tanga, Serengeti Migration Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Rukwa, Tour Oparator Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Kagera, Wildlife Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Morogoro, Bee Keeping Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Tabora na Community Services Tourism Award ambayo ilichukuliwa na Miss Utalii Tanzania 2012/13 kutoka Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza Baada ya ziara nzima ya Miss Utalii Tanzania 2012/13 na kutoa Tuzo za Utalii Tanzania, Kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa wa Hifadhi ya Taifa ya Mikumi Ndugu Dattomax Sellanyika, alishukuru sana kwa waandaaji wa Miss Utalii Tanzania 2012/13 kwa kutembelea Hifadho hiyo ya Mikumi na kuifanya wenyeji wa utoaji Tuzo za utalii Tanzania, alishukuru pia kwa Burudani nzuri iliyo tolewa na Miss Utalii Tanzania 2012/13, pamoja na hayo aliongeza kwa kusema kuwa hii ni nafasi ya pekee ya kuutangaza utalii wa Ndani ya Nchi na kusisitiza kuwa Miss Utalii Tanzania 2012/13 wametokea katika Mikoa yote ya Tanzania Hivyo watakuwa ni Mabarozi wazuri katika kuutangaza utalii wa Tanzania na Hifadhi zote za Taifa za Tanzania ikiwemo na Mikumi National Park.
No comments:
Post a Comment