Saturday, May 18, 2013

SIMBA S.C. 0 - 2 YANGA S.C. NA MPIRA UMEMALIZIKA


Simba line up: Juma Kaseja, Nassor Masoud 'Chollo', Haruna Shamte, Shomari Kapombe, Mussa Mudde, William Lucian, Mwinyi Kazimoto, Abdallah Seseme, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba na Haruna Chanongo. Sub: Abel Dhaira, Miraji Adam, Ramadhan Singano 'Messi', Felix Sunzu, Christopher Edward, Jonas Mkude na Hassan Mkude

Yanga line up: Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite, David Luhende, Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Athuman Idd 'Chuji', Simon Msuva, Frank Domayo, Didier Kavumbagu, Hamis Kiiza na Haruna Niyonzima. Sub: Said Mohamed, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nurdin Bakar, Nizar Khalfan, Said Bahanuz na Jerry Tegete

Mpira unaanza uwanja wa Taifa
Dkk 1 YELLOW CARD...! Mbuyu Twite wa Yanga anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Haruna Chanongo wa Simba

Dkk ya 4 Didier Kavambagu anaipatia Yanga bao la kuongoza

Dk 8 Simba inapata kona ambayo haizai matunda

Dkk 10 Didier Kavumbagu wa Yanga anamchezea faulo Shomari Kapombe.

DkK 15 bado Yanga wapo mbele kwa goli 1-0

Dkk 16 YELLOW CARD......! Haruna Shamte wa Simba anaonyeshwa kadi ya njano baada ya kumchezea vibaya Simon Msuva.

Dkk 20 Cannavaro wa Yanga anachezewa faulo na Haruna Shamte wa Simba.

Dk 21 Hamis Kiiza wa Yanga anauwahi vizuri mpira katikati ya mabeki wa Simba waliojichanganya kuokoa lakini shuti lake hafifu linaokolewa na kipa wa Simba, Juma Kaseja.

Dakika ya 28 Simba walipata penati, akapiga Mussa Mudde na kukosaDk 27 PENALLLLTTY......! Simba inapata penalti baada ya Cannavaro kumchezea vibaya Mrisho Ngassa.

Dk 32 Mwinyi Kazimoto wa Simba anamchezea vibaya Frank Domayo wa Yanga.

Dk 35 Kiiza wa Yanga anakosa bao la wazi baada ya mpira alioupiga kutoka juu ya lango la Simba.

Dk 38 Simba inapata kona ya pili.

Mpira ni mapumziko, Young Africans 1 - 0 Simba SC

Kipindi cha pili cha mchezo kimeanza

Dkk 63 Hamis Kiiza anaipatia Young Africans bao la pili

Dkk ya 75, Young Africans 2 - 0 Simba SC
Anaingia Nizar Khalfani kuchukua nafasi ya Hamis Kiiza

Dkk ya 85, anaingia Juma Abdul kuchukua nafasi ya Mbuyu Twite

Dkk ya 89, Mpira umesimama kidogo, baada ya Nassoro Chollo kumsukuma Kavumbagu na wakati mwamuzi anamuulia kadondoka chini mwenyewe.

Mpira umemalizika, Young Africans 2 - 0 Simba SC
Kavumbagu ddk 4
Kiiza dkk 63

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake