Misimamo na mitazamo hiyo huiendeleza hata katika uhusiano wa kimapenzi. Yeyote yule ambaye humuona anazuia furaha ya moyo wake, hupambana naye. Ukiwa kwenye mapenzi na mwanamke, jaribu kuhakikisha huzuii furaha yake, vinginevyo atakuona adui kisha atakwenda kutoa penzi nje.
Katika sura hiyo, mwanamke humuona mwenzi wake ni mtu hatari kwa maslahi ya furaha ya moyo wake. Sasa basi, baada ya uvumilivu, huanza kusaka furaha kwa namna yoyote ile. Ni hapo ndipo mwanamke humsaliti mwenzi wake, hivyo kutia doa bay asana kwenye uhusiano.
Mwanzoni wakati wa usaliti, mwanamke huwa hajutii vitendo vyake. Zaidi, hujiona mjanja kwa maana hudhani anajibu mapigo ya mwenzi wake. Inapotokea baadaye wawili hao wanakaa chini na kumaliza mgogoro unaowakabili, ndipo mwanamke hujutia usaliti wake na kuamua kusitisha uhusiano wan je.
Bashasha, vicheko na amani ni nguzo muhimu katika uhusiano wa kimapenzi. Humjenga mwanamke kujiona yupo kwenye uhusiano sahihi. Anapovikosa, hudhani anaweza kutafuta penzi lingine. Ni jukumu la kila mwanaume kuhakikisha vitu hivyo vinakuwepo katika uhusiano ili kuufanya udumu.
Epuka sana migogoro isiyokwisha, inayoweza kumfanya mwanamke ajione mnyonge au akawa na hasira za mara kwa mara. Ogopa sana kuwa kwenye uhusiano na mwanamke halafu akawa anajiona hayupo huru kwenye mapenzi yake. Ukiruhusu hayo yatokee, usimlaumu mtu pale utakapogundua anakusaliti.
Katika pointi hii, nitoe muongozo kwamba usaliti huanzia kwenye hatua za awali. Wewe unaweza kuwa msaliti kwa mwenzi wako hata kama huna mpenzi mwingine wa nje. Mtindo wenu wa maisha kama humfanyi apate yale mahitaji muhimu ya uhusiano wa kimapenzi, huo nao ni usaliti.
Unapomfanya ajione mnyonge, mwenye msongo wa mawazo, huo nao ni usaliti, kwa maana hayakuwa mapatano yenu kuingia kwenye uhusiano usio na amani. Ahadi yenu ni kupendana kwa dhati na kila mmoja kujali furaha ya mwenzake. Sasa basi, usisahau kwamba kwenda kinyume nako ni kusaliti.
Atakapokusaliti utaumia, tena inawezekana ukawa hodari wa kumsema vibaya, sasa msifike huko kwa kuhakikisha mwenzi wako anafurahia uhusiano wenu na mnaishi kwa upendo ambao unakubalika. Ni suala la kuhakikisha unatengeneza mzani wa furaha kwenye uhusiano wako kila siku.
Kanuni ni wewe kujali furaha yako lakini hutafurahia uhusiano wako kama mwenzi wako yupo kwenye sononeko. Mpe anachokitaka, vaa uhusika ambao yeye anakubaliana nao. Kuishi katika mtindo ambao unamchukiza na ukaendelea hivyohivyo bila kujisahihisha, unakuwa unauchimbia kabu uhusiano wako kwa tabia yako mwenyewe.
Bila shaka hutaki akusaliti, sasa unalo jukumu la kuhakikisha unamtengenezea njia za kuona faida za uaminifu wake. Tendo la uaminifu kwa mwanamke huendana na namna yeye mwenyewe anavyojisikia katika uhusiano wake. Ukimfanya ajisikie furaha atakutunzia penzi lako, kinyume chake ataligawa kwa mwengine atakayehisi anaweza kumfariji.
6. IKIWA HUMPATII KITANDANI
Kuna tatizo kubwa sana lililopo kwa wanaume. Wengi wao hupenda kufanyiwa ‘madikodiko’ wakiwa faragha ila wao hushindwa kulitekeleza kwa wenzi wao. Hilo kwa namna kubwa ni majanga kwa wanawake ambao huhitaji kutendewa mambo matamu katika eneo la ‘uwanja wa fundi seremala’.
Kuna aina ya ujinga ambayo inaweza kuwepo kwenye vichwa vya baadhi ya wanaume kuwa wanawake ni chombo cha burudani. GPL
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake