Muda mfupi uliopita,Mtu mmoja aliYetambulika kwa jina la Shirima ambaye ni Mfanyabiashara katika moja ya Maduka ya Kariakoo jijini Dar es Salaam,amejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na amekimbizwa hospitali kwa uangalizi zaidi maana haijafahamika kama kapoteza Maisha au bado yu hai.
Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangukia Gari aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli hiyo....chanzo cha kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka sasa.Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita,wanaeleza kuwa walipatwa na mshuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa kimeangukia gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima.
4 comments:
Hivi kulikuwa na umuhimu gani kutaja kabila la mtu? Huu ukabila unauhusiano gani na mtu kujirusha? Mwalimu Nyerere ameondoka na hekima zote tumebaki watupu?
Acha ukabila, mchaga maana yake nini? Huwezi andika habari bila kutaja kabila la muhusika?
Hatutakiwi kulaumu kutajwa kwa kabila la mtu, kwani kichwa cha habari kinajieleza vizuri kabisa kwamba kuna mchagga alishawahi pata kifo cha aina kama hiyo je mnazani mtu alietoa habari hii angeripoti vipi kama si kutaja kabila? na kwa nini tusijifaharishe kwa makabila yetu?
Anonymous wa May 4, 2013 nawe ni mkabila. Hatujifaharishi na makabila bali tunajinafsisha na makabila. Katika suala hili hakuna haja ya kutaja kabila la mtu wakati kuna vielezo vingine.
Post a Comment