ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, May 7, 2013

Ruge Mtahaba kashindwa kujibu shutuma na hoja za Lady Jay Dee

Boss wa Clouds FM Bw.Ruge Mutahaba katika maamuzi ya "hasira za mkizi"

*Ruge Mutahaba kashindwa kujibu shutuma za comando Lady Jay Dee.
*Wasanii hamkeni kujua nani mchawi wa kazi zenu.


Na Buberwa Jackob.
Watanzania leo tulikua tukimsikiliza mkurugenzi wa utafiti wa redio Clouds FM Bw.Ruge Mtahaba katika mahojiano na redio yake ya clouds fm, mahojiano ambayo tulikua tukitegemea boss Ruge ajibu shutuma dhidi yake za kumtilia kauzibe katika kupata riziki mwanamuziki Lady Jay Dee bint machozi, katika mahojiano hayo ambayo sisi wasikilizaji tunayafananisha sawa na KESI YA NYANI mwamuzi awe Ngedere.

Tulichokua tunakitegemea katika mahojiano ni majibu ya shutuma dhidi ya Bw.Ruge lakini cha kushangaza Ruge kashindwa kabisa kujibu shutuma zinazomkabiri baadala yake akawa anarusha rushua maneno na kuhusisha mifano ya wasanii walishuka na nani kapanda, na kuenda nje ya hoja ya msingi,mwisho wa mahojiano Bw.Ruge alikurupuka kwakauli za kuamrisha kuwa ni maarufu kupiga nyimbo za kizazi kipya (Bongo Fleva) kwa mda wa siku nzima katika kituo cha clouds fm.
Sasa watanzania tunajiuliza hivi redio ya Clouds FM au Redio ya Ruge na wasanii pamoja na sisi wanachi nani ? muhimu kwa karne hii ambayo taifa lina vituo vya redio zaidi ya 80?
Kwani wasanii wanamuhitaji sana Ruge na mshirika wake Bw.Kusaga,yaani wao ndio tuseme miungu ya wasanii?

Wananchi walio wengi wanamuunga mkono Lady Jay Dee kwa kutokukubali afanywe ngazi au kitendea kazi cha kuwanufaisha wanyonyaji katika soko la muziki,na kahamua kujitegemea.mahamuzi hayo ya Jay Dee ndio yanamfanya Jide atake kugeuzwa "Kondoo wa Sadaka" .

MRADI WA RUGE MTAHABA KATIKA SEKTA HII YA MUZIKI NI KUUA MUZIKI WA DANSI NA TAARABU NA KUJENGA MSINGI WA UTAMADUNI NA MZIKI WA KIZAZI KIPYA .
Ukisikiliza sana maelezo ya Ruge katika mahojiano utagundua wazi kuwa alijenga au alijaribu kujenga mtandao wa kuwamiliki na kuwajenga wanamuziki wa kizazi kipya kwa manufaa yake,yaani mwanamuziki hasipoingizwa katika mtandao huu basi hatojulikana na kazi zake azitotambulika ,yaani mtandao ambao pia unampendekeza msanii gani aukubalike kupewa tuzo hata kama si msanii mzuri, mtandao huu pia unatumika kama sululu la kuuchimbia kaburi muziki wa dansi na muziki wa taarabu,mtandao huu pia unawalazimisha watanzania walio wengi muziki gani wa kusikiliza, na mara nyingine kuwalazimisha wanamuziki nini cha kupiga( Beat) n.k.

Leo Ruge anapomsema Lady Jay Dee ampe kijiti mwingine na Lady Jay Dee anaposema yeye ni Lady Jay dee anapiga muziki kwa maisha yake na kuwalidhisha washabiki wake,hakuna haja ya kupokezana vijiti katika gemu la muziki. Bali mfumo huu kupokezana vijiti ni mfumo unaoitwa "Ruge Mtahaba System" na wasananii wamesha istukia kuwa si mfumo mzuri. Je ? wanamuziki wapo tayari kufanywa kete za kuchezea bao au chess! kwanini? lazima wasanii wapate pumuuzi ya uhai kutoka katika mtandao wa Ruge? hivi wasanii hawezi kusimama kidete na kuungana kwa pamoja wakajipigania na kukataa kufanya wapagazi katika sekta hii? Ruge kaonyesha Kiburi kwa kusema mziki wa bongo flava usipigwe kwa siku nzima redioni Clouds ! Sasa wasanii na nyinyi
Onyesheni mshikamano na msimamo wenu kwa Ruge,kuwa nanyi ni muhimu kwa jamii ya watanzania.

Je ? Nani mchawi wa kazi za wasanii na muziki wa Tanzania?
Watanzania na serikali ya Tanzania imeshuhudia kuangushwa kwa makusudi muziki wa dansi wa tanzania,
na kuchimbiwa kaburi utamaduni na sanaa za maonyesho wa watanzania,ujuma ambazo zinafanywa na mtandao ya siri ya wajanja wanaujumu utamaduni na muziki wa watanzania.
Na wanamtandao ambao wanaangaliwa macho bila ya kufanywa chochote na watanzania au kuchukuliwa hatua zozote na serikali kupitia idara husika.
Leo watanzania tunajiuliza hivi hawa akina Ruge Mtahaba wanazijua historia ya muziki wa Tanzania? na  misingi ya miziki wa Tanzania, na wale waliojitoa waenga muhanga katika kujenga misingi hiyo imara? mbona nchi za wenzetu wanaendeleza misingi na miziki yao ya awali,kama ilivyo taarabu na mziki wa dansi.
Inakuaje leo hapa kuna baadhi ya wajanja wasiojua hata historia ya muziki wa tanzania watuchagulia nini? cha kusikiliza.
"JOTO HASIRA" KUNA HAJA YA KUWAFUKUZA KAZI NA KUVUNJA MTANDAO HUU UNAUJUMU UTAMADUNI ,MUZIKI NA WASANII WATANZANIA

8 comments:

Anonymous said...

Wana saikolojia wanasema unakuwa na bosi mwenye umbile dogo, mara nyingi huwa anahisi kudharauliwa. Ufupi na udogo wake kimaumbile unamfanya ajisikie kama haonekani. Kwahiyo anaweza akaamua kutafuta attention kwa njia yeyote ile, mfano kujitambulisha kuwa yeye ndiye mwenye mamlaka wakati watu wanalifamu hilo au kupiga marufuku kitu Fulani kutendeka ili watu watambue mamlaka yake. Bosi kama huyo anapokuwa anatokea kwa watani zangu kule Bukoba, hali ndiyo inakuwa mbaya zaidi. Hata awe amesoma au kuishi nje, hawezi kubadilika. Nafikiri wadau wote wenye ma-bosi wafupi na wadogo kimaumbile mtakubaliana na mimi.

Anonymous said...

kwa kweli Ruge ametokota badala ya kuchemsha,mahamuzi yake yanaonekana jinsi alivyokua na upeo mdogo wa kufikiri kabla ya kutoa mahamuzi.
Kingine kutojua historia na thamani ya utamaduni na sanaa

Anonymous said...

Kwa kuwa blog hii inasomwa na wadau wengi ndani na nje ya nchi, napenda kuchukua fursa hii kuandika machache kuhusu lugha yetu tukufu ya kiswahili. Kwanza nampongeza aliyeandika makala hii, "ila mnisahihishe kama ninakosea" ni vema mtu anapoamua kuandika habari ambayo itasomwa na wengi hususan wasio wazungumzaji wa lugha husika kwa nia ya kujifunza, basi ni vema tuandike kwa ufasaha.
Nimegundua na kukerwa na makosa mengi yaliyojitokeza katika makala husika na naomba nitoe maneno yenye usahihi kwa faida ya wote.Nitaandika maneno jinsi yalivyoandikwa katika makala(herufi ndogo) na vile yanavyopaswa kutumika kwa ufasaha9herufi kubwa).

tulikua............TULIKUWA
tulichokua.........TULICHOKUWA
zinazomkabiri......ZINAZOMKABILI
maarufu............MARUFUKU
mda................MUDA
wanachi............WANANCHI
kuhamua............KUAMUA
mahamuzi...........MAAMUZI
hasipoingizwa......ASIPOINGIZWA
azitotambulika.....HAZITOTAMBULIKA
unaujumu.......UNAOHUJUMU/UNAHUJUMU
Ndugu zangu Watanzania tusipokitumia kiswahili kwa ufasaha,dunia nzima itapotoshwa maana hii ni lugha yetu na hakuna anayekifahamu kiswahili zaidi ya Mtanzania.

Anonymous said...

Mimi binafsi namshukuru sana anonymous wa Ma7, 2013 @ 6:40 kwa mchango wako mzuri sana dhidi ya upotoshwaji wa maneno ya Kiswahili katika makala mbalimbali za libeneke (blog) la Vijimambo. Wewe mdau unaonekana ni mtaalamu mzuri sana wa Kiswahili ambaye umeonyesha kujali na kuitetea lugha yetu. Wengi wetu tunaotumia libeneke hili tunazo taaluma nyingine, tuliondoka nyumbani siku nyingi na hatutumii Kiswahili in regular basis. Tunaweza kutumia lugha yetu na tukawasiliana, lakini hatuwezi kuitumia kwa "ufasaha". Wasiwasi wangu ni kuwa unawezakupata heart attack kwa kukerwa na matumizi mabaya ya Kiswahili. Wewe pata 'context' ya kile kilichozungumzwa halafu uendelee na utaratibu wako wa maisha. Iwapo unakerwa na matumizi ya Kiswahili kwenye blog hii, tembelea blog zingine zinazoandika lugha kwa ufasaha. Ninauhakika kuwa nako huko utakerwa vilevile. Napenda kukushukuru kwa kutufundisha.

Anonymous said...

Mkosoaji wa makala:
Ulichosema kina ukweli sana tena saaaaana.
Mimi ni mmoja wa wanaokerwa na maandishi mabovu ya kiswahili.
Watanzania tunajigamba na kujidai sana eti kiswahili ni lugha "yetu". Cha kushangaza ni kuwa wengi kiswahili chao ni kibovu kabisa!
Matumizi hayo ni katika hususan kuchanganya herufi "l" na "r".
Tatizo hili liko mda mrefu safa.
Jipya ni kuondoa herufi "h" au kuiweka pasipo stahili.
Elimu mbovu, kiingereza kibovu na sasa hata kiswahili pia????

Anonymous said...

Ninyi mnaokerwa na ubovu wa lugha, basi chukueni fimbo mtuchape ili roho zenu zitulie. Hatuna PhD za Kiswahili.

Anonymous said...

Nami nimshukuru sana mdau aliyekosoa uandishi wa kiswahili kisicho sahihi. Hili tatizo la kiswahili kibovu linazidi kukua siku baada ya siku na sasa si katika kuandika tuu bali sikiliza nyimbo nyingi za kiswahili(Hasa za bongo fleva), Watangazaji wa redio mbalimbali, Washereheshaji, blogu na baadhi ya magazeti. Kwa kweli inakera sana. Hebu tujifunze na kukitumia kiswahili vile inavyopasa.

Anonymous said...

Nakupeni hongera kwa kukosoa na kurekebisha lugha yetu hii adhimu ya Kiswahili, lakini mkoasoaji wa awali napenda nimkosoe pia kuwa katika Kiswahili hakuna neno maamuzi bali uamuzi.