ANGALIA LIVE NEWS

Monday, June 3, 2013

COCA COLA WAMNUNULIA DIAMOND GARI MPYA!

 Ukikutana na Diamond mtaani akiwa na mchuma mpya wenye rangi nyeusi, usishtuke sana, jua ni courtesy of Cocacola.
Inavyoonekana ni kuwa Cocaboy kama anavyojiita siku hizi, amenunuliwa gari jipya na wadhamini wake kampuni ya vichwaji ya Cocacola.

“Ya all ready know what it’s….. tukutane Fuel station!! #CocaCola Mumetishaaaaaa,” aliandika jana kwenye picha ya Instagram ya gari hilo likiwa na maganda yake.

“Chatin infront of my Small baby… on @channeloafrica interview at my clib,” aliongeza.
Siku nzima ya jana, hitmaker huyo wa Kesho alikuwa busy kwenye interview na kituo cha runinga cha Channel O.

2 comments:

Anonymous said...

My "Clib" ndio nini? Big up Diamond ila tumia google kwa chati itakusaidia kimtindo!

Anonymous said...

naona Diamond hakukosea sana naamini "clib" kakusudia "crib" kwa maana ya nyumba yake au kijumba chake. Angalau amejitahidi yeye si mzawa wa hio lugha, lakini ndio yumo muhimu ni kueleweka. Pengine wengine wangemwambia tumia Kiswahili chako tu unachokijua na achana na KiEnglish usichokijua. naamini amefanya hivyo kuvutia hisia za wasomaji kwani kuchanganya lugha mara nyingi kunaongeza utamu wa lugha. ona ladha inaongezeka kumwita mpenzi "honey" badala ya "asali". hapa US nilimsikiliza mwanzilishi wa kampuni ya kuuza kahawa ya Starbucks Howard Shultz akiulizwa kwa nini amevipa majina ya kilatini vinywaji karibu vyote vya kahawa anayoiuza, alijibu ni kuongeza utamu wa hio kahawa ijapokuwa wamarekani wengi hawatamki wala kuandika sawa sawa hicho kilatini lakini biashara inaendelea. Mwacheni kijana afanye biashara, ajitanueeee!!! wakati wake huu, wengine wasubiri wakati wao. hata sisi wazawa wa Kiswahili tunaandika makosa matupu, hakuna mkamilifu.