Friday, June 7, 2013

MAHAFALI YA KUFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI DARAJA LA KWANZA KOZI NAMBA 20 KWA ASKARI MAGEREZA YAFANA MKOANI MBEYA

 Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akipokea Salamu za heshima kutoka kwa wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya

Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akikagua wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya

Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheo cha Ukoplo Askari B4448 Patric Babara kwa niaba ya wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya

Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheti muhitimu B7348 Patrick Chalemta aliye fanya vizuri masomo ya Darasani katika mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20

Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimtunuku cheti muhitimu aliye fanya vizuri somo la kulenga shabaha 3163 Tatu Amri katika mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 

kwa picha zaidi bofya read more


Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akimpa zawadi muhitimu 3914 Leonida Hillu ya mwnafunzi mwenye Nidhamu usafi na ukakamavu katika mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20

Baadhi ya Maofisa wakitoa heshima katika mahafali ya mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya

Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga (kushoto) akiwa na Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira Staniford Ntirudura wakipokea Salamu za heshima kutoka kwa wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya

Wahitimu wakiwa kwenye Gwaride wakipita kwa mwendo wa Haraka mbele ya Mgeni Rasmi.
"Hima..... Hima.... Hima!.... " Ni salamu ya utii ikiongozwa na Parade Kamanda SP Lucas Ndoteela


Baadhi ya Maofisa wakifuatilia kwa Makini shughuli za Mahafali


Baadhi ya Wahitimu wakionesha umahili wa kupambana na maadui

Watoto wanaolelewa na kituo cha malezi ya watoto wadogo katika chuo cha Magereza wakitumbuiza katika Sherehe za Mahafali

Mkuu wa Chuo cha Magereza Kiwira, Kamishina msaidizi wa Magereza Staniford Ntirudura akizungumza jambo katika mahafali hayo.



Wahitimu wa mafunzo ya uongozi daraja la kwanza kozi namba 20 katika sherehe za kufunga mafunzo hayo yaliyo fanyika katika chuo cha Magereza Kiwira Tukuyu Rungwe Mkoani Mbeya, wakifuatilia matukio yanayo endelea katika Sherehe zao.

Wahitimu B5414 Peter Ndalahwa na 3469 Matha Mwanjala wakisoma Lisara katika mahafali yao 


Muhitimu B3494 Willy Timoth akisoma Shairi wakati wa mahafali

Kamishna wa Fedha na utawala wa Magereza Gaston Sanga akizungumza na wahitimu


JUMLA ya Askari 984 wa Jeshi la Magereza, wanaume 845 na wanawake 139 wametunukiwa Vyeo vya Ukoplo baada ya kuhitimu mafunzo ya Uongozi daraja la Kwanza kozi namba 20 katika Chuo cha Magereza Kiwira Wilaya ya Rungwe Mkoa wa Mbeya.

Vyeo hivyo vilitolewa na Kamishina wa Fedha na Utawala Gaston Sanga kwa niaba ya Kamishna Jenerali wa Magereza katika Sherehe za ufungaji wa mafunzo hayo zilizofanyika katika Viwanja vya Chuo hicho leo Juni 7, Mwaka huu.



Akizungumza katika mahafali hayo, Kamishina wa Fedha na Utawala wa Magereza, Gaston Sanga amesema Askari wa Jeshi la Magereza Nchini wanatakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, taratibu na kanuni za kazi kwa kufuata uwajibikaji, unyenyekevu, ukakamavu, ujasili, upendo, ushirikiano, uvumilivu, uaminifu na nidhamu.

Kamishina Sanga amesema Maaskari wanapaswa kuzingatia elimu waliyopewa wakati wa mafunzo ili wakawe mfano kipindi cha utendaji kazi wao ikiwa ni pamoja na kuhamasisha na kuwaongoza wenzao ambao hawakupatiwa elimu kama yao.

Aidha amewaasa kutowatesa Wafungwa walioko magerezani bali kuwahudumia kwa kuzingatia kuwa wanamhudumia binadamu kama walivyo wao na siyo kuchukua nafasi ya kuwanyanyasa bila kuogopa haki na Stahili za binadamu japokuwa ni wafungwa.


No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake