ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 15, 2013

MAMA WEMA ATISHIA KUMCHOMA MTU KISU

Na Mwandishi Wetu
VIDEO inayomuonesha mama wa Wema Isaac Sepetu, Miriam Sepetu akizua timbwili ‘hevi’ nyumbani kwa mwanaye huyo huku akitishia kumchoma mtu kisu imevuja, Ijumaa limeinasa.
Wema Isaac Sepetu akiwa na mama yake Miriam Sepetu.
Kwa mujibu wa video hiyo, mama Wema alitimba nyumbani kwa mwanaye huyo Kijitonyama, Dar kwa lengo la kuwasambaratisha marafiki wanafiki wa Wema ambao alidai wanamharibu mwanaye.
Pamoja na matusi yanayosikika kwenye video hiyo, mzazi huyo alikuwa akitoa vitisho kwa Maila ambaye ni mmoja wa mashosti wa karibu wa Wema.
“Nitammaliza huyu…(tusi), hana kwao, hana chochote,” sauti ya mama Wema inasikika na kuongeza:
“Nina data, mimi nilipigiwa simu, huyu sijui Maila, sijui nani kuwa alishikwa na begi lenye vipisi vya bangi Airport (uwanja wa ndege).
“Hawamshauri Wema chochote, wanamharibu ili maisha yake achanganyikiwe. Ningekuwa na kisu ningemchoma…ningekuwa na kisu leo ningemchoma visu…potelea mbali.”
Mbali na vitisho hivyo, mama Wema anaonekana akibinua vitu vya ndani kama makabati na makochi ikidaiwa kuwa alikuwa akisaka bangi aliyoletewa mwanaye na rafiki zake.
Kwa mujibu wa watu walioiona video hiyo walisema marafiki wa Wema kama Kajala Masanja, Snura Mushi, Martin Kadinda, Jamila na wengine kibao wanapaswa kuwa makini na mama huyo kwani anaonekana kuwa na hasira nao.
Baada ya kuinasa video hiyo, Ijumaa lilimsaka mama Wema ili kupata mzani wa habari hiyo lakini simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.
Mwandishi Wetu alikwenda nyumbani kwa mama huyo Sinza-Mori, Dar ili kuzungumza naye ‘laivu’ lakini alipogonga tu getini alitokea binti aliyedai mama Wema hakuwepo.

4 comments:

Anonymous said...

Inasikitisha sana mama mtumzima anapo oonyesha tabia kama hiyo!!! Watu wana cheka na kudhani ni kichekesho ila hawaelewi akimchoma mtu kisu ataozea jela! Mie nashindwa kuelewa mama mtu mzima kwanza kuwa na lugha kama hiyo, pili kutishia mtu au watu maisha!! Inasikitisha sana hakika. Busara na Hekima za wazazi ziko waapi hapa jamani?

Anonymous said...

Haya ni majangaz hakika! Huyu mama tabia yake na matendo yake yanatia woga kidogo. Wema si mtu mzima kabisa mwenye akili yake timamu jamani? inakuwaje mama yake anavamia nyumba yake na kukurupusha watu na maneno mazito na kuitisha kisu awachome? Haya ni Majangaz, huyo Wema mwenyewe utulivu zero sasa sijui hao watu mama yake anadai wanamuharibu mwanae inahusika vijiii jamani? Majangaz haya. Simoooooooo...

Anonymous said...

things are falling apart, this girl is so dirty and may be people do not know why? I will tell you, you know what, her mother had spoiled her when she was a kid now she is grown up bad, the mother doesn't want to blame herself for the destruction instead she is shifting the blame to friends and partners. Wema is a big girl she know what she is doing that's the way of living she has learned from her parents, now what mama let the world teach her manners, and please before you jump onto the necks of others look at yourself first!!I hate to write this but I got to do what I got to do.

Anonymous said...

jamani msimlaumu sana mama yake wema jamani ni mapenzi ya mama nani asiyejua hakuna mtu anayependa mwanawe aharibikiwe jamani kama hamjaza subirini mzae na muone sikuobeeni lakini ukimpata mtoto mtukutu ndo utajua uchungu wa mwana, unadhani mzazi huyu anapenda mambo mwanawe anayoyatenda, mtoto kwa mama hakuwi hata kama akiwa mtu mzima tusijidanganye nanai kama mama

na nikweli kuna watu ambao wako karibu sana na wema ndo wanamharibia halafu wakiwa peke mbali na upeo wa macho wanamcheka huyo wema mzazi anayaona na kuyasikia unadhani atapenda

usidhani kama anasema maneno hayo kwa raha au furaha au ubabe ni kwa uchungu anaona mwanawe anaharibiwa hata kama wema ana akili zake mtu ukiwa na company mbaya marafiki waovu lazima watakushauri uovu na ubaya na yeye wema ndo anawaona wenzake kumbe sio mama ndo anaye ona mbali

jamani hamuoni watu wanaopata matunzo ya mama na kuwa karibu na mama zoa na kujisifu kwenye mitandao na vyombo vya habari kwamba nampenda mama yangu so unadhani mama wema hataki mwanawe awe kama hao sema wema anajidai ku act uzungu sana ndo tatizo lake na hawajui marafiki wanafiki

wema mdogo wangu tulia wema na penda unavyo act na ni mtaalamu mbona unajichafulia msikilize mama yako atakaye kuonea uchungu ni mama yako ana mapenzi ya kweli na wewe wema usimuone kazeeka ukaon hana la kukushauri kwa kizazi chako kipya 20 century girl, tulia mama

na nakuombea mungu uolewe mama

mdao anayekupenda kwa nia safi kazisa na kukuzimia kichizi

NY