Friday, June 7, 2013

MAPENZI NI HISIA TAMU ZENYE CHUNGU, USICHEZEE!


WENGI huwa hawapati muda wa kutafakari kwa kina japo kidogo tu kuhusu hisia za mapenzi.
Wapo wanaofikiri mapenzi ni kukutana kimwili halafu baasi! Wengine wanadhani kwamba mapenzi ni jambo la kawaida tu.

Rafiki zangu, kama nawe unawaza hivyo unakosea sana. Mapenzi si rahisi kama wengi wanavyofikiri. Ni hisia zinazotesa na na kuumiza kuliko kawaida.
Kwa faida ya ambao hawajui undani wa mapenzi leo wanakwenda kuwa wapya kabisa baada ya kusoma mada hii. Hebu twende tukajifunze.

KWA NINI TUNAJADILI?
Yupo msomaji mmoja alinitumia meseji akiomba ushauri. Aliandika: “Kaka Jose, naomba msaada wako. Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 19, nimeishia darasa la saba tu.
“Kwa bahati nzuri nilifaulu lakini kwa sababu wazazi wangu hawana uwezo sikuweza kuendelea na elimu ya sekondari. Nipo nyumbani sasa kwa muda wa miaka mitatu.
“Hivi karibuni nilikutana na kijana mmoja mtu mzima kiasi lakini hajaoa. Amesema ananipenda na lengo lake ni kuoa kwa ndoa, nikamweleza juu ya kiu yangu ya kusoma akasema yupo tayari kunisomesha.
“Ukweli ni kwamba moyoni mwangu hayupo hata kidogo lakini nahitaji anisaidie kunisomesha. Unanishauri nini kaka yangu?”

UMEONA?
Yaani anajua kabisa hampendi lakini anataka kuwa naye kwa ajili ya malengo ya kusoma. Hili ni kosa kubwa sana. Wengi wanafanya hivi lakini mwisho wake hauwi mzuri hata kidogo.
Kama nawe upo katika mkumbo huu ni vizuri ukaacha kwa faida yako mwenyewe. Hisia za mapenzi hazichezewi hata siku moja. Moyo hauchezewi.

MAPENZI NI KUWEKEZA
Ngoja nikuambie rafiki yangu, mapenzi ni kuwekeza. Ukiona mtu yupo tayari hata kutumia gharama zake kwa ajili ya mtu tena kwa matarajio ya baadaye ujue yupo tayari kufanya ‘investment’.
Siku zote mtu anayewekeza katika biashara hategemei kupata hasara. Uwekezaji mara nyingi huwa una lengo la kupata faida. Sasa kama mwenzako amewekeza akitegemea kupata mke bora, mke msomi hapo baadaye, vipi akija kugundua tofauti?
Unadhani atakuwa tayari kweli kupoteza miaka minne au zaidi kumsubiri ‘mke’ anayesoma kwa gharama zake halafu baadaye eti anabadilika na kumkataa?
Nini kitatokea unadhani? Ni matatizo ambayo yangeweza kuepukika. Bado kuna mengi ya kujifunza katika mada hii, wiki ijayo nitakuwa hapa kwa mwendelezo wake, USIKOSE!

Joseph Shaluwa ni Mshauri wa Mambo ya Mapenzi anayeandikia Magazeti ya Global Publishers, ameandika Vitabu vya True Love, Let’s Talk About Love na All About Love vilivyopo mitaani.

2 comments:

  1. ushauri uliyompa ni mzuri sana tena wenye busara kwa mtu mwenye roho njema lakini katika dunia ya leo naona mimi huyu msichana akubali tu kulewa na dingi amsomesha labda huwezi juea akikumbuka alipomfikisha katika ndoto yake ya kusoma ni huyu dingi huenda akampenda, usikikiye msichana huyu ni mdogo na ni mkweli kuna wasichana wangapi huwa hawasemi nia zao na wanakubali kuingia kwenye mapenzi na wanaume halafu wakipata wanachokitaka wanatimua

    so namsifu sana msichana huyu lakin ninacho ona mimi dunia ya leo biashara kubali kuolewa naye utimize ndoto yako ya kusoma mama halafu mbele kwa mbele mtajuana

    unaweza ukampenda baadaye kwa nia yake njema na pia unaweza ukamlipa pesa zake utakapo pata kazi nzuri

    maisha ndo haya ya siku hizi usisikiye kwani kila jinsi hufanya kuwekeza katika mapenzi kila mfanya biashara matarajio yake kupata lakini wangapi wanapata si wengi tu wana kosa hizo faida wanarudisha pesa tu walizo nunulia hivyo vitu

    tumia akili baby girl dunia ya leo biashara mamaa

    mtanisamehe wadau wenzangu simfundishi kuwa na roho hii lakini maisha ndo haya haya

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake