Mtendaji wa kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu akizungumzia hatua yao ya kushirikisha wadau katika zoezi la kufanya usafi manispaa ya Ilala, ambapo amesema mwezi ujao wanajiandaa kushirikiana na wenzao wa Chuo cha IFM, ili vijana hao waweze kuhamasika na suala la usafi na kuwa wataendelea kushirikisha taasisi, vikundi na asasi mbalimbali ili zifahamu kuwa usafi ni jukumu la kila mtu bila kuisahau kampuni ya usafi ilala ya Green Waste Pro ltd. Katika zoezi hilo leo wameshirikiana na Kikundi cha vijana cha Youth Power Group cha Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu kusafisha fukwe ya Bahari ya Hindi kuanzia eneo la Ocean Road Hospital mpaka Aga Khan.
Mchungaji wa Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu Marcos Braga akizungumza wakati wa zoezi la pamoja na viongozi wa kata ya Kivukoni na Kampuni ya Green Waste Pro kufanya usafi kutoka ufukwe wa Ocean Road hadi eneo la Aga Khan ambapo amesema ni jukumu lao kuendeleza maisha ya baadae ya taifa letu, hivyo kila wakati wanajitoa kushiriki miradi na kazi tofauti zitakazofanikisha kulikomboa taifa kimaendeleo likiwemo suala la usafi wa jiji.
Ameongeza kuwa walichifanya leo sio mwishi bali watakuwa wakifanya mara mbili kwa mwezi katika maeneo tofauti hivyo ameomba ushirikiano kwa serikali na wadau mbalimbali.
Mchungaji Marcos Braga wa Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi ya Kata ya Kivukoni kabla kuelekea eneo la tukio kwa ajili ya kushiriki zoezi la kusafisha fukwe ya Bahari ya Hindi kuanzisha Ocean Road Hospital mpaka Aga Khan.
Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Renatus Ruhungu (aliyeketi) Afisa Usafi wa Manispaa ya Ilala Bw. Samuel Bubegwa (na wa tatu kushoto), Meneja Msaidizi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro ltd Bw. Abdallah Mbena (kushoto) katika picha ya pamoja na baadhi ya vijana wa kikundi cha Youth Power Group cha Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu.
Wanakikundi cha Youth Power Group wa Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu wakielekea kwenye fukwe za bahari ya Hindi kwa ajili ya zoezi la usafi.
Vijana wa Youth Power Group wakiwa na Bango lao linalohamasisha vijana kupinga matumizi ya madawa ya kulevya kwenye Barabara ya Obama.
Picha juu na chini ni Mtendaji wa Kata ya Kivukoni Renatus Ruhungu (mwenye kofia nyeusi) akishiriki zoezi hilo na baadhi ya wanakikundi.
kwa picha zaidi bofya read more
Bw. Said Mazingira wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. akishiriki zoezi hilo na Kikundi cha Youth Power Group kutoka kata ya Gerezani.
Mchungaji Marcos Braga wa Kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu akijumuika kwenye zoezi hilo na vijana wake.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Usafi ya Green Waste Pro Ltd akishirkiana na vijana wa Kanisa la Universal La Ufalme wa Mungu wakati wa zoezi hilo.
Kazi imepamba moto.
Viongozi, walinzi shirikishi na baadhi ya wananchi wa kata ya Kivukoni katika manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam wakishirikiana na waumini takriban 100 wa kanisa la Uokovu na Ufufuo la Kidongo Chekundu leo wameendesha zoezi la kufanya usafi kwa kuokota takataka na kufagia kuanzia eneo la ufukwe wa Ocean Road hadi eneo la Aga Khan sambamba na kampuni ya usafi katika manispaa hiyo ya Green Waste pro Ltd.Akizungumza na vyombo vya habari Mtendaji wa kata ya Kivukoni Bw. Renatus Ruhungu amesema kwa leo wanashirikiana na wenzao wa Universal Church wa kata ya Gerezani na wadau wengine pamoja na Kampuni ya Green Waste Pro lakini wakati mwingine watashirikisha wadau wengine katika utaratibu wao wa kufanya usafi kila wiki ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya waraka wa Mkurugenzi na mkuu wa Mkoa.
Ameongeza kuwa wameona wakifanya wao tu ile dhana ya kuwa usafi ni wa kila mtu watakuwa wameipoteza, hivyo wakaona ni vyema sasa kushirikisha taasisi na jamii zilizo kwao na mbazo ziko nje pia kuzialika kuja kushikiana na wao kufanya usafi ili wananchi waone kumbe sio kazi ya serikali.
Naye wa Kiongozi wa kanisa la Universal la Ufalme wa Mungu Mchungaji Marcos Braga amesema wao kama kanisa wakiangalia nchi wanaona vitu vipi vinatakiwa kuendelezwa na nini kinatakiwa kifanyike, hivyo wameamua kutoka nje kwenda kuendeleza mji wao kwa kuanzia na usafi.
Amefafanua kuwa kikundi cha vijana wa kanisa hilo kinashiriki katika shughuli mbalimbali ambazo zinaigusa jamii moja kwa moja na pia tuna kampeni inayosema ‘Kijana Mwerevu Sema hapana kwa Madawa ya Kulevya’ kwa kuwa vijana wengi wanaangukia katika matumizi ya dawa hizo na kufanya maendeleo ya taifa la kesho kuwa duni.
No comments:
Post a Comment