Walimu
wa Kiswahili Jumuiya ya Watanzania DMV wakiwa pamoja na walimu wenzao toka Vyuo
mbalimbali hapa Marekani siku ya mwisho ya Kumaliza madarasa. Hawa sasa ni
wataalamu wa kufundisha Kiswahili kama lugha ya kigeni hapa Marekani.
Sherehe ya kukabidhiwa vyeti, walimu waliofudhu kozi ya
kufundisha Kiswahili wakiwa na waalimu wao Dr. Alwiya Omar (watatu kutoka
kushoto- waliosimama), ambaye ni Mhadhiri wa lugha ya Kiswahili katika chuo
kikuu cha Indiana na pia ni Rais wa NCOLCTL (National Council of Less Commonly
Taught Languages) na Dkt. Kiarie Wanjogu (watatu kutoka kulia- waliosimama),
ambaye yeye ni Mhadhiri wa lugha ya Kiswahili katika chuo cha YALE na ni Rais
wa ALTA (African Language Teachers Association).
Picha ya pamoja baada
ya kukabidhiwa vyeti na Dr. Antonia
Schleicher (wanne kutoka kushoto – waliosimama), ambaye ni Mhadhiri katika
chuo kikuu cha Indiana anafundisha lugha ya Yoruba na pia ni Mkurugenzi Mkuu wa NALRC (National African Language Resource Center) katika chuo kikuu cha
Indiana.
No comments:
Post a Comment