ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 31, 2013

Bastola nje nje, zauzwa mitaani nchini

Dar/Mikoani. Kukithiri kwa rushwa miongoni mwa baadhi ya maofisa wa Jeshi la Polisi nchini, kumesababisha silaha ndogondogo hususan bastola kumilikiwa na watu wasio na sifa nchini.
Uchunguzi wa kina wa gazeti hili katika mikoa mbalimbali nchini ikiwamo iliyopo mipakani inaonyesha kuwa, bastola zinamilikiwa na watu bila ya kufuata taratibu na nyingine zikitumika kwa ajili ya kufanyia uhalifu.
Hivi sasa hata vibaka ambao awali walikuwa wakitumia visu na mbao za misumari kupora mali za watu, sasa wanafanya uhalifu huo kwa kutumia bastola.

Tamasha la kiislam convention center, Washington, DC

 Tamasha la Kiislam lililofanyika Jumamosi Aug 31, 2013 Convention Center iliyopo Washington, DC na kujumisha jumuiya mbalimbali za Kiislam nchini Marekani.
 Vitu mbalimbali vinavyohusiana na Uiislam vilionyesshwa kwenye maonyesho hayo.
 Picha kama unavyoona.
 Mazuria kama unavyoona.
 Vitabu mbalimbali vinavyohusiana na Uislaam vilikuwepo kwenye tamasha hilo lililofanyika Jumamosi Aug 31, 2013 Convention Center.
 Madira kama unavyoona
 picha mbalimbali kutoka kila pende ya Dunia zilionyeshwa.
 Hiki ni kitabu kinacho muelezea mfanyakazi wa MTV aliyeenda Mecca na baada ya hapo kubadilisha maisha yake ambaye alikua anaitwa Babe na sasa anaitwa Burka
 Vitu mbalimbali kama unavyoona kwenye picha

Lulu akiongea na vyombo habari kwenye rad carpet siku ya uzinduz...

Mourinho apuuza ushindi wa Bayern

Bayern Munich dhidi ya Chelsea

Jose Mourinho alidai baada ya mechi kua timu bora ndiyo iliyopoteza kufuatia ushindi wa Bayern Munich dhidi ya watu 10 wa Chelsea kwa matuta 5-4 kufuatia suluhu ya bao 2-2 katika mchuano wa kombe la Uefa la Super Cup.

Chelsea ilionekana kukaribia ushindi zikiwa zimesalia sekunde chache kipenga cha kumaliza mechi kipigwe mjini Prague, lakini mchezaji aliyeingizwa katika mda wa majeruhi Javi Martinez akarudisha na kusababisha mda wa ziada na hivyo kusababisha mshindi aamuliwe kwa njia ya matuta.


Mchezaji Romelu Lukaku ndiye aliyekosa mkwaju wa mwisho ambao ungeamua mshindi lakini Mourinho hata hivyo kama kawaida alionekana kua katika hali ya ubabe bila kutaka kukubali matokeo.

"timu bora wazi wazi imepoteza," alisema. "wametushinda kwa sababu ya kufunga mkwaju mmoja zaidi yetu."

Awali mshambuliaji Fernando Torres aliipa Chelsea bao la kwanza katika kipindi cha kwanza lakini Franck Ribery akarudisha dakika mbili baada ya kipindi cha pili kuanza na kupelekea mchezo uingia mda wa ziada.

Mnamo dakika ya 85 mcheza kiungo Ramires akaonyeshwa kadi nyekundu na kuwaacha washindi wa Ligi ya Europa League uchi. Ingawa Eden Hazard aliirejeshea Chelsea matumaini katika kipindi hiki cha ziada, Martinez aliusukuma mpira wavuni sekunde chache kabla ya kipenga cha mwisho kusababisha mechi kuamuliwa kupitia matuta.

Somalia yakaribisha TED-X

Wasomi, wasanii na wafanya-biashara wa Somalia wamekuwa wakizungumza katika mji mkuu, Mogadishu, kwenye ile mikutano inayofanywa sehemu mbali-mbali za dunia iitwayo TED-EX.

Mazungumzo hayo yaliyofanywa kwenye ukumbi wa mikutano chini ya ulinzi mkubwa, yalihusu mapendekezo na ubunifu wa kuijenga tena Somalia.

Hotuba katika vikao vya TED-EX zimetolewa katika nchi zaidi ya 150.

Mandela hakutolewa hospitali

Serikali ya afrika Kusini imekanusha taarifa za vyombo vya habari kwamba aliyekuwa kiongozi wa afrika Kusini, Nelson Mandela, ambaye amelazwa hospitali tangu mwezi wa Juni, kwamba alirejeshwa nyumbani Johannesburg Ijumaa usiku.

Taarifa ya serikali imesema kuwa Bwana Mandela bado yuko hospitali mjini Pretoria na kwamba bado mahtuti, lakini hali yake imetulia.

Kulazwa kwa muda mrefu kwa kiongozi huyo kumewatia wasiwasi raia wa taifa hilo na ulimwengu kwa jumla.

Mandela ambaye ana umri wa miaka 95, alikuwa Muafrika wa kwanza kuwa rais wa taifa la Afrika Kusini, na anaheshimiwa na wengi kama baba wa taifa.

Putin ataka Marekani ioneshe ushahidi

Rais Vladimir Putin wa Urusi anasema tuhuma kuwa serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali ni upuuzi mtupu.

Anasema jeshi la Syria lilikuwa linasonga mbele, hapakuwa na sababu ya serikali kuwapa kisingizio wale wanaotaka kuingia kijeshi.

Bwana Putin alisema ikiwa Marekani ina ushahidi kuthibitisha tuhuma zake, basi ikabidhi ushahidi huo kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Alimkumbusha Rais Obama kuwa aliwahi kutunzwa tuzo ya amani ya Nobel, na alimsihi kuwakumbuka wanyonge katika mashambulio.

Alikaribisha uamuzi wa bunge la Uingereza ambalo halikuunga mkono Uingereza kuingilia kati Syria, na anasema ameshangazwa na uamuzi huo wa bunge.

KIJIWE CHA UGHAIBUNI KUHOST MECHI YA MAN U NA LIVERPOOL JUMAPILI SEPT 1, 2013 DMV

Juu na chini ni timu za Man U na Liverpool zitakipiga Jumapili Sept 1, 2013 Wanakijwe cha ughaibuni watahost mtanange huo kuanzia saa 1:30 asubuhi (7:30am) na kutakuwa na supu na chapati karibuni wote wapenzi wa soka
Address ni
6200 Ager Road
Hyattsville, MD 20783 

MALAWI YANYAKUA KOMBE LA LABOR DAY DMV

Timu ya Malawi ndio mabingwa wa mwaka huu wa Labor Day Tournament iliyofanyika Layhill Park na kushirikisha timu 5 wakiwemo Tanzania ambao walipoteza mechi zao mbili za mwanzo na kushindwa kutinga nusu fainali, Malawi waliwafunga Kenya waliotoka New Jersey kwa bao 1-0 lililowawezesha kunyakua kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo.
Timu ya Kenya kutoka New Jersey
Vitambi FC (Kenya ya Maryland) ambao ndio waliokua wenyeji wa mashindano hayo na walifungwa mechi yao ya robo fainali na Malawi.
Watembezi FC (Kenya kutoka Baltimore) ambao walitolewa na Malawi kwenye mchezo wa nusu fainali.
Timu ya Malawi ambao ndio wamechukua ndoo hiyo ya Labor Day kwenye michezo iliyoenda sambamba na nyama choma na kujumuisha Afrika Mashariki pamoja.
Timu ya Tanzania katika picha ya pamoja.
Marefa waliochezesha mechi hizo.
Mchezo wa Valleyball ukiendelea.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi

LABOR DAY LAYHILL PARK YAFANA DMV

Wadau mbalimbali kutoka afrika ya mashariki walikutana Layhill Park kwenye nyama choma iliyoenda sambamba na michezo ya mprira wa miguu na Valleyball ili mradi mambo ya Labor Day Weekend inafana.
Kushoto ni Mr TZ katika picha ya pamoja na rafiki yake.
Wabongo wakiwemo kwenye nyama choma hiyo.
Kushoto ni Dj Omoshi akiwakillisha katika picha ya pamoja na shabiki wa timu ya Vitambi FC.
Wadada wakiwa wamependeza katika picha ya pamoja walipojumuika na wanaAfrika mashariki kwenye nyama choma Layhill Park.
Wadada katika picha ya pamoja walipokua nao kwenye nyama choma iliyofanyika kwenye park ya Layhill iliyoo Silver Spring, Maryland.
Ni mapozi na kuringa kama unavyowaona wenyewe nani kama wao.
Mdau katika picha ya pamoja na mdhamini wa pendo lake.
Wadau kutoka Kenya katika picha ya pamoja
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

WAKAZI WA MTWARA WAIPOKEA KWA SHANGWE SEMINA YA FURSA KWA VIJANA


Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume  akizungumza mapema leo kwenye semin ya FURSA iliyofanyika kwenye ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia ni Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikijadiliwa ukumbini humo.Semina hiyo inaratibiwa na Clouds Media Group na kufadhiriwa na NSSF,Lake Oil,Zantel,MaxMalipo na wengineo imewashirikisha wadau mbalimbali wa Mtwara na vitongoji vyake wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya.
  Baadhi ya Wakazi wa Mji wa Mtwara na vitongoji vyake wakifuatilia kwa makini  yaliyokuwa yakijiri kwenye semina ya Fursa kwa Vijana iliyofanyika mapema leo ndani ya ukumbi wa  Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana mkoani Mtwara.
 Mkuu wa Wilaya ya Iramba (ambaye pia ni mzaliwa wa Newala mkaoni Mtwara),Mh.Yahya Nawanda akizungumza na wakazi wa mji wa Mtwara waliojitokeza kwa wingi kwenye semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo,Mh.Yahya alizunguma mengi zikiwemo fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara na Singida namna ya kuzifanyia kazi katika suala zima la kujikwamua na maisha. 
Mkurugenzi wa Vipindi Clouds Media Group,Ruge Mutahaba  akihitimisha semina ya Fursa kwa Vijana mapema leo mchana,ndani ya ukumbi wa ukumbi wa Pentecoste Ligula B,uliopo mkabala na Kituo cha Vijana Mtwara,kulia kwake ni Meneja Kiongozi,Uhusiano NSSF Makao makuu jijini Dar,Eunice Chiume pamoja na Meneja wa NSSF mkoani Mtwara Bwa.Stanley Mullanzi.Semina ya Fursa kwa vijana tayari imekwishafanyika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na sasa Mtwara. PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPO.COM

BASI LA LIVAI LAPATA AJALI MBAYA MAENEO YA MKURANGA PWANI

Basi la abiria la livai linalofanya safari zake Kutoka Dar es salaam kwenda nachingwea limepata ajali eneo la Mkuranga Mkoa wa Pwani na kuumia vibaya sehemu ya mbele hadi sasa haijathibitishwa kifo chochote kutokea.

RAIS JAKAYA KIKWETE APOKEWA NA GWARIDE LA SUNGUSUNGU WA AUSTRIA

 Taswira za askari wa jadi wa jimbo la Tyrol huko Alpbach nchini Austia wakiingia kwa gwaride rasmi lililoandaliwa kwa heshima ya Rais Jakaya Kikwete aliye katika mkutano wa Kamisheni ya Ulaya mjini humo. Historia ya askari hawa, wanaojulikana kama Schuetzenkompanie, inakwenda miaka ya 1810 wakati wa vita na watu wa Bavaria. Soma historia yao BOFYA HAPA
 Sungusungu hao wakiendelea kuwasili
 Kila mmoja ana gobole lililotengenezwa kienyeji
 Watoto kwa wakubwa wamevutiwa na Sungusungu hao
 Gwaride rasmi
 Mdau anajiunga na Rais Jakaya Kikwete na Rais wa Austria Mhe Heinz Fischer (katikati), Rais wa Kamisheni ya Ulaya Mhe Jose Manuel Barroso (wa pili kushoto), Rais wa Mkutano wa Alpbach Dr Franz Fischer (kushoto) pamoja na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (kulia) akifuatiwa na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Profesa Rwekaza Mukandala

KUMEKUCHA LAYHILL PARK PICHA YA MAMBO MUDA HUU DMV

Wachezaji na mashabiki wakianza kuingia mambo ndio hvyo Labor Day Jumamosi Aug 31, 2013 14901 Layhill Rd, Silver Spring, MD 20906
Wachezaji wakipata picha ya pamoja kutoka kushoto Libe, Dedi Luba, Best wa Vitambi FC na Kuringe

 Mude kulia akipata mulo wa asubuhi kukazia tumbo
 Wadau kutoka Kenya
 Umoshi katika picha
 One Mic akifanya vitu vyake
 Mchezaji wa Tanzania DMV Yusuf katika picha
kwa picha zaidi bofya soma zaidi