Advertisements

Thursday, July 9, 2015

ROSE MUHANDO: NAFIKIRIA KURUDI KWENYE UISLAM

Muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini, Rose Muhando.

NYOTA wa nyimbo za Injili Bongo, Rose Muhando amesema hakuna jambo jema alilojifunza tangu abadili dini kutoka kwenye Uislamu na kuwa Mkristo zaidi ya ‘ugaidi’ wa kiroho mbaya na sasa anaangalia namna ya kurudi katika imani yake ya kwanza.

Akizungumza na Amani hivi karibuni, Rose alisema hana furaha katika maisha ya Ukristo tofauti na alivyokuwa akielezwa wakati akihubiriwa kuokoka.

Pia Rose alikwenda mbali zaidi kwa kuwarushia madongo baadhi ya wachungaji kwa kumhukumu kwa maneno ya walimwengu bila kutumia hekima za kidini.

“Wakati nahubiriwa kuokoka, niliambiwa nitakutana na upendo lakini matokeo yake nimekuwa mtu wa ‘kupigwa mashuti’ tu.

“Mfano, mtu anakualika kwenye tamasha, kwa bahati mbaya unashindwa kufika na unampa taarifa lakini kesho yake unasikia umetapeli, wameshindwa kuona hata jema moja kwangu? Nafikiria kurudi kwenye dini yangu, naamini nitapata faraja,” alisema Rose.

Mwimbaji huyo amekuwa akikumbwa na skendo ya utapeli ambapo hudaiwa kupokea fedha kwa ajili ya kutumbuiza kwenye matamasha ya dini halafu kuingia mitini.\

GPL

14 comments:

Anonymous said...

Rudi mama ulipoenda ulipotea njia

Anonymous said...

Dada dunia (pesa/utajili) ndio ulikutoa uislam sasa umeshaona kama dunia sio bora,1st Allah subhuhana uwattawalla remember that

Unknown said...

Dear Rose Mhando,
Mimi napenda sana nyimbo zako za kidini.
Zinatangaza neno la Mungu kama ilivyo andikwa ndani ya Bible.
Usiwe kigeugeu. Ulishabadili usirudi nyuma. Ni mwiko kutazama nyuma.
Ukutizama nyumba au kurudi kwenye dini ya zamani na mambo yatarudi kama ulivyokuwa.

Anonymous said...

Jitathmini vizuri issue sio dini bali ni tabia yako.sitashangaa kusikia kesho unahamia dini ya Budhaa ..

Anonymous said...

Dada,
Kila la kheri, kumbuka haijali dini...cha muhimu
Ni wewe,dhamira yako na amani ndani ya roho yako. Binadamu siku zote ana maoni na maneno hivyo fanya maamuzi tu na uridhike....vinginevyo utahama kulia na kushoto. Ikiwa roho yako inakutuma kurudia Uislam basi rudi tu.
Ikiwa maisha yako yana msimamo na muelekeo mzuri hamna litakalo
sumbua akili yako. Kila la kheri.

Anonymous said...

Umenena vyema kutamka ulokole. Wengi wenu mnaojidai kuokoka na kuingia ulokole ni tamaa za pesa tu. Mkikosa mafanikio mnaanza kuhaha. Ulokole siyo ukristo ni mvurugano tu wa watu wasioeleweka. Nenda kokote utakako Mama ila usije Roman Catholic tabia zako za kurukaruka hatutazivumilia.

Anonymous said...

Wewe anonymous wa july9@6:08pm nimependa comment yako

Anonymous said...

Wewe dada Rose Muhando MUNGU akusaidie sana. Ni wewe wakati ukiondoka kwenye uisilamu ukiwa mgonjwa na hakuna aliyekuthamini, ukasema mwenyewe wakristo wakukuta katika magonjwa na shida nyingi ulizikuwa nazo. Ukamkabidhi YESU kuwa BWANA NA MWOKOZI wa maisha yako, akakuponya magonjwa na shida zote ulizokuwa nazo. Leo hii umefahamika dunia nzima kwa kuwa ni YESU aliyekuinua, sasa unamkana kabisa. Swala hilo halihitaji ushauri wa mtu, wala halihitaji kwenda shule, ila ni kukumbuka nani alikuponya kutoka katika magonjwa yale uliyokuwa nayo. Kitu cha kukusaidia ni kuwa kila binadamu ana mapungufu yake, ya kwako ni kutokuwa mwaminifu katika ahadi unazoahidiana na wanaokualika, sasa funga na kuomba YEYE aliyekuponya na magonjwa na umaskini uliokuwa nao NDIYE atakayekusaidia kuondokana na mapungufu uliyonayo. Pia ukumbuke kuwa nafasi uliopo sasa ni kubwa na ina upinzani. " mti wenye maembe mengi ndio unaotupiwa mawe". Na BWANA YESU akubariki sana.

Anonymous said...

mimi ninaonavyo mimi bora uwe mpagani usiye na dini. because katika dini ya kiislamu kurudi tena utakuwa mnafiqh.
ukiristo si dini hata katika bibilia imeshaeleza hilo.yesu si mungu sasa wewe ulijingiza huko hujafanya reseach halafu yamekukuta yaliyokukuta sasa unataka kurudi tena katika uislamu.
utapokelewa lakini ukae ukijua uislamu si unafiqh.

ukiristo hakuna kitu kule.wala hakuna dini inayoitwa ukiristo nitakutoleeni maandiko mtazimia wenyewe.

na makatoliki waliokuambia hapo juu si dini.ni uraia wa watu wa roma.

sijui mummy kwanini unaingia katika dini hizi bila ya kufanya research na umeuacha uislamu dini ya haki na kweli.

nenda sasa kuwa pagani au baniani.

yesu haponyi yeye mwenyewe kisha sema bila ya babayake hawezi fanya kitu so jiulize kwa kauli hiyo.

pole sana mummy.ukirudi uislamuni lazima ufate masharti ya dini na uwe muislamu wa kweli otherwise.wewe na mungu wako ndo atakuhukumu.

Anonymous said...

Maneno ya udini yaliyowekwa na anonymous wa July 10 @ 3:36 yanaonyesha wazi ni kwanini nchi nyingi zenye Waislamu wengi hazina Amani. Kila siku ni mauaji tu. Umesema Ukristo siyo dini! Hayo ni mawazo yako ila Mungu ajua undani wake. Mimi nasema Uislamu ni dini ila tatizo elimu ndogo kwa Viongozi na Waumini wote. Waliosoma hawawezi kuwa na fikra mbovu na jazba zinazotawala uislamu duniani leo hii. Huyo mwanamke Rose arudi tu huko tangu lini nyoka alishageuka kuwa Simba??

Anonymous said...

Dada Rose Mwombe Mungu akusaidie katiks kufanya maamuzi,wewe ni kioo cha jamii na na kila ufanyacho kinaacha alama,Mungu akusaidie ili usije ukawayumbisha ambao hawajakuwa kiroho

Anonymous said...

Rose ulipohamua kuwa mkristo sidhani kama uliomba ushauri. Pia unapotaka kurudi kwenye uisilami ushauri wa nini? Nenda kawe jiwe la chumvi kama Ruthu.
Aliyesena Mtoto akililia wembe mpe hakukosea.
Good luck to your career!

job said...

Maamuzi unayoamua si mazuri mbele ya Mungu na kurudi ktk dini ya uislamu si suluhsho la mambo yako wew n kupga magoti na kumwambia MUNGU akusaidie. pia biblia inasema wabarkn wanao wauz

ni mim mch francis said
magugu manyara

job said...

Dini haikupeleki mbinguni fanya uokoke.
by mch francis saidy