Advertisements

Monday, August 24, 2015

PICHA ZINGINE ZA LOWASSA NDANI YA DALADALA JIJINI DAR LEO

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa ndani ya Daladala alilopanda kutokea Gongo la Mboto Mwisho mpaka Pugu Kajiungeni jijini Dar es salaam,mapema leo asubuhi.
Mh. Lowassa akishuka kwenye daladala.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo, wakati alipofanya ziara ya kushtukiza eneo hilo ili kujionea hali halishi ya biashara ndogo ndogo. Mh. Lowassa aliianza ziara yake eneo hilo la Gongo la Mboto na baadae alipanda daladala mpaka Pugu Kajiungeni, jijini Dar.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akimsikiliza Bi. Kulwa Juma ambaye ni mfanyabiashara ndogo ndogo ya kuuza Mihogo ya Kukaanga katika Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na vijana wanaoendesha Bodaboda waliokuwepo kando ya Kituo cha Mabasi cha Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo. Kulia ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akiwa katikati ya umati wa watu wakati alipotembelea eneo la Gongo la Mboto mwisho, Jijini Dar es salaam leo.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na baadhi ya wanafunzi waliokuwa kituoni hapo kusubiria usafiri.

Wakazi wa mji wa Mbagala wakiushangilia msafara wa Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni wakati walipotembelea Kituo cha Mabasi cha Mbagala Rangi tatu jijini Dar es salaam, wakati walipotembelea kituo hicho leo

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na Vijana wanaojihusisha na shughuli mbali mbali katika stendi kuu ya Mabasi yaendayo mikoa ya Lindi na Mtwara, ilipo Mbagala jijini Dar.
Mgombea Mwenza wa Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Juma Haji Duni akiwasalimia wakazi wa Mbagala.

37 comments:

Anonymous said...

Mtaka cha uvunguni hata kinyesi atalamba! .......Yeye ndo leo anapanda daladala?! Ooh! Au ana tengeneza movie eeh?? Hahahh! Classical Lowassa at his best!

Mwambieni Dr Magufuli mama yake alitembea kwa miguu kwenda kujifungua toto John Pombe Magufuli! Yani hata hela ya kupata da dala dala hakuwa nayo!

Dr Magufuli amezaliwa kwenye dhiki za Tanzania, amekuli kwenye dhiki ya Tanzania, amesoma elimu yake mpaka PhD hapo hapo Tanzania kwasababu hakuwa na uwezo wala connection ya kwenda kusoma nje ya nchi kama Lowassa. Hivyo Dr Magufuli anaelewa umasikini na shida za Watanzania kuliko Lowassa kwani yeye mwenyewe alisha wahi kuwa masikini na bado baadhi ya ndugu zake pamoja ni masikini siyo kama huyo wa "chakawa" sijui Chadema ambaye anafanya maigizo oops! Nimekumbuka kuiga / Sanaa ndiyo fani aliyosomea hahahh!......#MagufuliNdiyoMpangoMzima , #HapaNiKaziTuu , #WanawakeTaifaKubwaMagufuliIkuluLazima
#UtaisomaNumberMwakaHuu
#IkuluSiyoMovieTheater



Mwambieni Lowassa aache kutudhihaki siye wapanda dala dala!! #UnafikiMtupu #WiziMtupu

James Bond said...

Sasa kwa mama Magufuli kutembea kwa miguu kujifungua ndiyo iwe sababu ya sisi Kuchagua tena CCM? Umeishiwa fikra kama CCM ndugu:( kwa hiyo kama mtu alizaliwa kwenye utajiri hafai kuwa Rais? Kifo cha CCM Kipo njiani mtaongea sana Lowasa ni chaguo la wengi .

Anonymous said...

Watanzania Wanachotaka kusikia kutoka kwake ni maelezo ya ushiriki wake katika kashfa za Richmond na utakatishaji wa fedha kupitia kampuni yake ya Barare Limited.Hayo ya dalax2 Si issue ya msingi wakati huu.

Anonymous said...

Mwandishi mawazonuliyotoa hapa juu inaonyesha wewe ni mmojawapobwa wale walala njaa lakini ukonradhi kuipokea alfu kumi na tshirt sambamba na hao kina mama wanaotaabika kila siku simkwa biashara ndogo zinazokula mtaji, hospitalini kulazwa chini mama ntilie kunyanyapaliwa hatimae wanakuja kuambulia vitenge na kofia. !! Je wamekutumaah.

Anonymous said...

Raisi anayeondoka madarakani hayajui ya wananchi kazi ni kupanda ndege kila baada ya wiki! Si bora huyo anayetaka kuyaelewa ili ajue jinsi ya kushughulika nayo! Acheni mawenge njia ni nyeupeeh.

Anonymous said...

Annon wa hapo juu ebu acha ulimbukeni , Lowassa kupanda Dala dala kama sehemu ya campaign ni kitu cha kawaida. Mbona viongozi kama Obama walipanda public transportation kutembelea migahawa ya chakula, kula pizza na kuongea na wananchi.Na hafanyi hivyo siku za kawaida ila kwenye campaign. Ebu waelemishe wana CCM wenzako mwaka huu wataisoma Namba!

Anonymous said...

WE MDAU SIO WOTE WALIOKUJA KUSOMA NJEE NI WATOTO WA WAKUBWA AU WENYE UWEZO, SISI WENGINE NI WATOTO WA WAKULIMA ILA TULIPATA SCHOLARSHIP ZA KUJA KUSOMA NJE KUTOKANA NA BIDII ZETU MASHULENI.HAIMAANISHI SHIDA HATUZIJUI.AU UKISOMA HAPO HAPO BONGO NI KWAMBA UNAZIJUA SHIDA KULIKO WATU WENGINE TUNA MAWAZIRI WANGAPI WALIOSOMEA HAPO HAPO BONGO KUANZIA MSINGI MPAKA UPROFESA LAKINI BADO NI MAFISADI.
-EX TANGA-TECH 1998-2000.

Anonymous said...

daladala yenyewe kakaa kiti cha dirishani....angeshikilia mchuma aone uhalisia wake. kwanza alikuwa wapi siku zote kupanda daladala!

Anonymous said...

wewe mkeretwa wa kwanza nani kakwambia lowasa alizaliwa katika raha au alisoma nje?amepita humo humo alipopita mafunguo,na inaonekana upo nje muda mrefu fanya utafute makaratasi uwaone ndugu zako mpaka leo wanatembea kilometa kadhaa kwenda kujifungua na pale amana hospital wajawazito wanalala chini,na kama upo Tanzania basi umekunywa maji ya bendera ya chama cha mafisadi hutaki kukubali ukweli kwamba chama cha mafisadi na mafunguo wako alieuza nyumba za serikali kwa hawara zake wamesababisha hali hiyo ya waja wazito kutembea chinI tangu Enzi za magufuli anzaliwa mpaka leo hii,JITAZAME NA ACHA KUKARIRI.

Anonymous said...

Lowassa people's choice.

Anonymous said...

THIS IS THE BEST MOVE EVER FOR ANY PRESIDENTIAL CANDIDATE FROM ANY ANGLE !
WE DON'T HAVE TO HIRE DALADALA,MALORI ,MABASI,TRENI KAMA IPO FOR my fellow friends like
STREET VENDORS TO COME FOR YOU'RE CAMPAIGN, JUST GO WHERE THEY ARE ? OCT 25 IS AROUND THE CORNER ? MAKE YOUR MINDS B4 ELECTION DAY.

Anonymous said...

Acha ujinga wewe hapo juu....huyo Mnaye msema ndiyo ticket yenu mpaka sasa anatumia kodi ya watu kujipigia debe....kama anajua shida za watu asinge uza nyumba au kubwata upuuzii au jiulize kwa nini mama hake alikosa pesa ....nadhani jibu unalijua
Na sasa hivi i am sure debe analojipigia gharama ni serikali yetu au kodi za watu .
Pigeni kura zenu na hata ccm ikishinda bado nchi itadidimia since no true democracy under ccm. Jiulize why kupiga kampeni for two months and winning...be serious pls.
BORA NI MPIGIE KURA MTU YOYOTE KULIKO CCM .

Anonymous said...

Magufuli hawezi kuleta maendeleo yoyote kutokea CCM.Sisi tunamwangalia tu na kubwabwaja kwake na excitements nyingi alizonazo. Nakwambia pindi akianza kugusa INTERESTS ZA WAKUBWA!! ndiyo kwishnei yake!! wewe jiulize tu watu kama akina Chenge,rugemalila,mkapa(kashfa ya makaa ya mawe kiwira) na wengine tele wako wanadunda mtaani pamoja na kashfa zote hizo za rushwa na hakuna hata mtu mmoja anayethubutu kuwagusa SEMBUSE magufuli???? amkeni tulete mageuzi yaani hata Kenya wanatushinda kwa uchumi???

Anonymous said...

Sisi haituhusu magufuli na story yake
Tunataka maendeleo na maendeleo si kigezo eti katoka family maskini
Wangapi wametoka kwenye family masikini huko ccm walipopata uongozi wakasahau
Tatizo si magufuli tatizo ni mfumo wa ccm

Anonymous said...

Hivi dhiki na umaskini ndio kipimo cha kuwa Rais. Tutumie hizi nguvu zetu kuchukia umaskini. I hate Poverty kama Lowassa alivyosema. Siasa za Ujamaa na Kujitegemea ndio chanzo cha umaskini. Lets end poverty. Poverty is a shame. Poverty ni laana.

Anonymous said...

Na wewe nenda kafanye kama yeye,hizo unazo ongea ni pumba kweni ulikuwa po wakati anazaliea,acha pumba hizo ,punguza pumba utazeeka vibayq

Anonymous said...

Utachukia umaskini umpende maskini?

Nafikiri kimya kimya!

Anonymous said...

Nendeni shule Kama zee lenu pamoja kutuibia mabilion na majumba aliyopewa na magufuli

Eti kutuita sisi wapumbavu na malofa
Anajuwa maana ya ukombozi ni nini
Ukombozi unaweza ukautafisir kwa maana tofauti
Eti alisoma lugha toba
Tuombe radhi tutakuombea misikitini na makanisani mungu akulani

Anonymous said...

Kama hampendi lowassa nendeni huko huko kwenye picha za magufuli msifieni hadi akhera kwenye picha za lowassa tuwachieni wenyewe
Matusi yote yanatoka kwenu ccm
Tangu spika, mawaziri, wabunge hadi rais
Mmekuwa wa vijembe kama wanawake
Wekeni fact tuwaelewe
Angalieni bungeni wapinzani wanavyojua kujenga hoja
Wabunge wen kazi kulala na kupinga ndiyo
Ndo maana 50 years hakuna maendeleo

Anonymous said...

Au mlitaka awe kama vascodagama
Kila kikicha foleni ya wasindikizaji na wapokeaji airport
Bora anavyo ondoka tuliichukia airport hiyo
Cha ajabu akija ughaibuni hata kuku hawamjui
Leo Lowassa kupanda daladala imekuwa issue kwenu CCM

Daniel said...

Wabongo uweni waelewa! Ndo maana mnaitwa malofa! Maana yake ni kwamba MH. LOWASA alishaeleza kwamba hakuhusika YALIKUWA NI MAAGIZO KUTOKA JUU. SASA KAMA WEWE UNA USHAHIDI--- MZEE ALITANGAZA MKUTANE KISUTU. SHIDA IKO WAPI? ACHENI UJINGA

Anonymous said...

Hata mimi sipendi CCM wala UKAWA lakini Nina imani na Dr Magufuli kuliko actor Lowassa!

Aliuza nyumba kwa bei nafuu ili kila mtu aweze kununua na siyo matajiri pekee yake!

Nafikiri huitaji scientists kukuonyesha kuwa demokrasia iliyopo ndani ya CCM ni kubwa kuliko Chadema! So usijitie wazimu hapa

Anonymous said...

Uwo utajiri wake ameupataje?? Mbona hatakagi kuelezea? Siku zote yeye amekua mtumishi wa UMMA sasa uho utajiri wa Lowassa ambao hauelezeki kupata je kama si Fisadi???

Atasemaje CCM mbaya baada ya kukataliwa kugombea urais? Shame!
#DrMagufuliNdiyeMkomboziWetu
#MagufuliNiMzalendoHalisi
#MagufuliNdiyoMpangoMzima

Anonymous said...

Sawa tuu kama Mbowe alivyo kubali kuuza chama kwa milioni 10! Kila mtu anakula kwa urefu wa kama yake, hupo hapo! #WanawakeTaifaKubwaMagufuliIkuluLazima

Anonymous said...

Yani pamoja na kuzaliwa Tanzania na kuwa kiongozi wa ngapi za juu ya Watanzania bado alikuwa hajui matatizo ya Watanzania mpaka leo??? Sasa hapo kwenye daladala ndiyo atayajua au sikuhizi matatizo ya Watanzania yameandikwa ndani ya daladala???? He's simply out of touchy /out of clue / out of reality!! #IkuluSiyoMovieTheater

Anonymous said...

Obama alizaliwa kwenye umasiki daladala kwakwe ilikuwa ndiyo way of living siyo kama huyo actor wenu Lowassa #MwakaHuuMtaisomaNumber

Anonymous said...

Exactly mdau! Kula 10 ! Yani ungekuwa hapa ningekununulia chips kuku na Azam baridi!

Anonymous said...

Hahahahaha! eti nitafute makaratasi?? Kweli wewe punguani! Mie nakuja kwa Obama daily na sihitaji makaratasi kenge wewe!

Embu muulize Lowassa kuhusu kuondoa watu kwenye Kota za Nasako pale Masami na kununua binti yake Pamela?? Huo sio ufisadi??

Magufuli alikuwa anatoa fursa kwa kila Mtanzania kununua nyimba ila mazoba kama nyinyi hamkuelewa!

Hata kama alimuuzia nyumba hawala yake bado ni Mtanzania siyo kama huyo Fisadi and actor Lowassa anaye ingizia Tanzania umasikini kwa kwa makampuni fake!

Ukiongelea hawala yani huyo Lowassa ndo anavimada hadi UK so just shut up!

Anonymous said...

Si umeona eeh! And lowassa will never dare to speak about them!! Maendeleo ya taifa letu yataletwa na sisi wenyewe kupitia Dr Magufuli. #MagufuliNdiyoMpangoMzima

Anonymous said...

Tatizo ni mfumo siyo? Na huyo Lowassa kazaliwa na kukulia kwenye mfumo upi? Mpaka leo hii at age of 60+ ndo aone huo mfumo ulio mlea na kumneemesha haufai???? Mfumo =DNA sasa how can you change your DNA especially after 60+ yrs??? You can only change your Identity kama Catlin Jenner au actor Lowassa but your DNA / Mfumo will always be the same!! Wake-up wewe!!
#MagufuliNdiyoMpangoMzima

Anonymous said...

Sijasema ndio kipimo cha urais bali tunatofautisha kati ya Male ndo halisi na Fisadi! Wote hatupendi umasikini lakini tunataka mtu muandilifu ambaye atatutowa kwenye huo umasikini kwasababu anaujua na kuelewa nini maana ya umasikini as he has been there before na siyo Actor kama Lowassa! Upo mpaka hapo???

#HapaNiKaziTuu

Anonymous said...

Hhahhahha! We heard you loudly and clear!
Si ndiyo hapo sasa palipo patamu!! Anachukia umasiki lakini anataka kutumia wamasikini kutajirika?! Shame!
#IkuluSiyoMovieTheater

Anonymous said...

Subiri baada ya mgombea wa CCM kuapishwa ndio uone mapenzi halisi ya Lowasa na maskini.

Anonymous said...

WAKATI KAMATI YA BUNGE ( YA MWAKYEMBE ) INATOA TAARIFA YAKE.LOWASA HAKUNA MKA KUWA NI USANII BALI HE MELTED DOWN LIKE AN ICE NA KUAMUA KIJIUZURU ILI KUEPUSHA AIBU ZAIDI.LEO HII LOWASA ANATUMIA UDHAIFU WA BAADHI YA WA TANZANIA WA KUFIKIRI NA KUWEKA KUMBUX2 NA KUJA NA AGENDA ZA KUSEMA ULIKUWA NI USANII.TULITEGEMEA FOR ANY STRONG LEADER TO STAND ON HIS GROUND NA IKIBIDI AISHITAKI KAMATI YA MWAKYEMBE.
MKUU,WATANZANIA WENGI WANATAKA MABADILIKO BUT PLEASE SIO KUPITIA KWA LOWASA.

Anonymous said...

Waswahili walisema "Mtaongea mchana na usiku mtalala". Kwa mantiki hii wakati huu wa mwelekeo kwenye uchaguzi ni sawa na mchana na mengi yataongewa. Baada ya uchaguzi na mshindi kutangazwa usiku utaigubika Tanzania yetu na wengi wa Watanzania wanaoipenda nchi yao hatimaye wataona mchana ukirudi na wataanza kuongea tena wakiwa wanasherekea ushindi wao. Kwa upande mwingine wakiwa wakiwa wameshindwa kwenye uchaguzi watabaki wakiponda usingizi wao wakijutia kuto pata usafiri wa kuwapeleka walikotaka. Na haya yote mara nyingi yanamfanya mtu ajutie pale anapokuwa anasambaza sera ambazo lengo lake ni kuwazuga tu wanachi badala ya kuwaeleza ukweli. Kama kuna mtu anafikiria kuwa kuna kiongozi yeyote hapa duniani anaweza akatokomeza umasikini na kuwatajirisha wananchi wake wote au anaweza kutatua matatizo ya wananchi wake wote basi huyo kiongozi ni punguani. Hata hizi nchi zilizoendelea pamoja na majigambo yake yote bado matatizo ni yapo na masikini ni wengi pia. Wadau wenzangu tunaotoa changamoto zetu hapa mtandaoni lazima tuwe wakweli kuhusu kile tunachokiandika. Mimi naishi New York, Marekani, ambayo mtu yeyote duniani anaifahama lakini pamoja na yote haya kuna wananchi wengi tu hapa, wakuja na wazawa, ambao wanateseka wakiwa hawana mahali pa kulala na wengi hawajui hata watakula nini. Hii ndiyo nchi ambayo inasemekana imebobea kwenye maswala ya kidemokrasia na katika haki za binadamu. Kama hali ndivyo ilivyo katika nch kama hii ni jambo gani atakalolifanya kiongozi wa nchi kama yetu kunyesha mvua ya mapesa yatakayomfanya kila Mtanzania kuwa tajiri. Hizi ni ndoto za alinacha sa na hadithi za Alfu lela na ulela tulizokuwa tunazisoma kwenye vitabu vya Hekaya za Abunuasi. Tunakubali kuwa umasikini ni mbaya na hakuna mmoja wetu anayetaka kuwa masikini, lakini ukweli ni kuwa kitu kinachoweza kufanyika ni kupunguza mfumuko wa umaskini kwani hakuna nchi yoyote duniani ambayo imefuta umaskini wote na hivyo kuwafanya kila raia wan chi hiyo kuwa tajiri. Kwan nchi yetu sioni vipi mamluki wanaojidai wanawajali wananchi leo wanaweza wakawasaidia wakati wao wenyewe wamekuwa ni tatizo katika maendeleo ya nchi. Mwalimu alisema maendeleo ya nchi yetu kama hayataletwa na CCM yanaweza yakaletwa na vyama vya upinzani wakati huo akasema kuwa alitarajia upinzani ungeundwa na wana-CCM amabao walukuwa wanachama tu kwa vile hakukuwa na chama kingine. Mwalimu hakuimanisha kuwa mpinzani ni yule aliebakia CCM na baada ya zaidi ya miaka 10 tangia upinzani kuanzishwa anahama chama hicho baada ya kuenguliwa kwenye kura za maoni. Huyu mtu siyo mpinzani bali ni mtu mwenye ajenda yake binafsi na hivyo tunatakiwa kumuogopa kama ukoma. Wapinzania walikuwa akina Dr. Slaa, Lipumba, Cheyo, Makani, Mtei na wengine aina hiyo ambao walihama CCM (kama walikuwa wanachama) na kuunda vyama vya upinzani na mapema mara tu kipenga cha kuanzaisha vyama vya upinzani kupulizwa. Tunajua wengi wameyasema kuhusiana na upungufu wa chama tawala lakini angalau tuna rekodi ya ufanisi wa kazi ya chama hiki. Hatuna rekodi yoyote kutoka kwenye vyama vya upinzania zaidi ya majigambo ya kwenye majukwaa. Tukumbuke kuwa hakuna majaribio katika kuongoza nchi hivyo lazima tuwe makini sana katika kuchagua viongozi wetu. Kumchagua kiongozi au chama ambacho huna uhakika au rekodi ya ufanisi wake kwa ajili tu unataka mageuzi ni hatari kwani ukifanya hivyo hakuna kurudi nyuma na matokeo yake yanaweza kuwa na madhara makubwa. Kuondokana na matarajio yasiyokuwa na matokeo mazuri ni afadhali kuendana na methali ya Waswahili waliosema “Zimwi likujualo halikuli likakumaliza”.

Anonymous said...

Chukia umasikini, lakini utafute utajiri kwa njia halali. Huyo fisadi wenu amekuwa mtumishi wa umma maisha yake yote. Utajiri kaupataje?

Anonymous said...

You made me cry! Umesema ukweli mtupu bila ushabiki yani maneno yanakuingia haswa! Mungu awatangulie Watanzania waache ushabiki siku ya kupiga kura!