ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 24, 2015

KONGAMANO LA WIKI YA HUDUMA ZA KIFEDHA NA UWEKEZAJI KUFANYIKA AGOSTI 28-30, 2015 JIJINI DAR ES SALAAM

 Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nuebrand EC, Cathreen Bukuku (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, kuhusu kongamano la wiki ya  huduma za kifedha na uwekezaji litakalofanyika Agosti 28 hadi 30 mwaka huu, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkufunzi na Mratibu wa Mipango wa Kampuni hiyo, Daniel Wadelanga. Kongamano hilo limeandaliwa na Kampuni ya Nuebrand EC.
 Mjumbe wa Timu ya Mauzo wa Benki ya Uba United Bank for Africa, Tesha Filemon (katikati), akizungumza katika mkutano huo  kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na benki hiyo.
 Meneja wa Tawi la Kariakoo wa Benki ya The Peoples Bank of Zanzibar Ltd, Badru Idd (wa pili kushoto), akizungumza katika mkutano huo kuhusu benki hiyo na matawi yake.
 Ofisa Usanifu Bidhaa na Usimamizi wa Sharia Amana Benki, Jaffari Kesowani (kulia), akizungumza na wanahabari kuhusu kazi mbalimbali zinazohusiana na na benki hiyo.
 Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Jubilee Life Insurance, Adam Samson Namuhisa (kushoto), akizungumza katika mkutano huo.
 Msimamizi wa Masoko wa Kampuni ya Avic Town, Daniel Kure (kulia), akielezea kadhi kadhaa zinazofanywa na kampuni hiyo katika mkutano huo. Kushoto ni maofisa wa kampuni hiyo.
 Meneja Masoko na Uhusiano wa Kampuni ya  Covenant Bank, Mhina Semwenda (kulia), akizungumzia shughuli zinazofanywa na benki hiyo.
 Wadau mbalimbali kutoka taasisi za kifedha wakiwa 
kwenye mkutano huo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Wapiga picha wakiwa kazini. "Chezea kazi wewe"
Mmoja wa wanufaika na makongamano hayo yanayotolewa na  Kampuni hiyo ya Nuebrand EC, Alphonce Mkubwa kutoka Mbeya akieleza faida ya makongamano hayo aliyoshiriki kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Na Dotto Mwaibale

TAFITI zinaonesha asilimia kubwa ya watu hawatumii njia zilizo rasmi za kifedha kutokana na kukosa elimu ya masuala ya kifedha na uwekezaji.

Hayo yamesemwa Dar es Salaam leo na Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni ya Nuebrand, Cathreen Bukuku wakati akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu kongamano la wiki ya  huduma za kifedha na uwekezaji litakalofanyika Agosti 28 hadi 30 mwaka huu, viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam ambalo litahusisha watu wote, wawe wajasiriamali au si mjasiriamali una biashara au huna na wawekezaji wote ambapo washiriki watatoa kiingilio cha ada sh. 2000/- kwa ajili ya kushiriki kongamano hilo ambapo watapata cheti cha ushiriki,"alisema Bukuku.

Alisema lengo la kongamano hilo ni kuweka uelewa katika masuala ya kifedha kwani watanzania wengi wamekuwa hawatumii njia zilizosalama na rasmi za kifedha katika uwekaji, akiba na kutengeneza mazingira kuhusiana na huduma za kibenki pamoja na ujasiriamali.


Bukuku alisema washiriki watapata elimu ya uelewa wa bima mbalimbali kama za maisha, afya na bima ya mali, kupata elimu ya jinsi ya kuandaa mchamganuo mzuri wa biashara, kujifunza ujuzi mbalimbali na kupata fursa ya kushiriki katika shindano la kuandaa mchanganuo wa biashara ambapo atashinda fedha itakayomsaidia kuanzisha au kuendeleza biashara yake.

 Mkuu wa Mauzo na Usambazaji wa Jubilee Life Insurance, Adam Samson Namuhisa,  alisema lengo lao ni kutoa elimu ya bima za maisha kwa watanzania na kujua haki zao pamoja na kujua fursa zilizopo huku mshiriki akipata huduma myimgi kwa wakati mmoja.

Mshindi wa kongamano hilo msimu uliopita, Alphonce Mkubwa aliwataka vijana kujitokeza kushiriki ili wapate elimu ya kufanya biashara ili wapate mafanikio," Nilikuwa mshindi katika kutoa wazo la biashara ambapo nilishinda zabuni ya ukusanyaji ushuru katika halmashauri ya Wilaya ya Chunya...huu ni muda wa kufanya kazi kwani huu ni ukombozi kwa kutokukaa kijiweni,"alisema Mkubwa.  

No comments: