Advertisements

Wednesday, August 28, 2013

ARSENAL UTAIPENDA HATA KISIRI SIRI...YAFUZU KIUME HATUA YA MAKUNDI ULAYA

MPANGO mzima. Kidokezo cha mpango wa pili ni rahisi: tumia, tumia, tumia.
Arsenal imefuzu kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa usiku huu, kiulaini ikiitoa Fenerbahce.
Arsene Wenger sasa anatakiwa hadi usiku wa Jumatatu kumaliza tatizo lake sokoni kwa kununua wachezaji.
Mabao mawili ya Aaron Ramsey Uwanja wa Emirates katika dakika za 24 na 72 usiku huu yameifanya Arsenal iwatoe Waturuki kwa jumla ya 5-0, baada ya awali kushinda 3-0 ugenini.
Kikosi cha Arsenal leo kilikuwa: Szczesny, Jenkinson, Sagna, Mertesacker, Monreal, Wilshere, Ramsey, Cazorla, Walcott/Miyaichi dk73, Giroud/Sanogo dk59 na Podolski/Gibbs dk48.
Fenerbahce: Demirel, Gonul, Bruno Alves, Korkmaz, Erkin, Sahin, Baroni/Potuk dk65, Meireles, Kuyt/Webo dk65, Emenike, Sow/Topuz dk82.
Aaron Ramsey akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao la kwanza dhidi ya Fenerbahche Uwanja wa Emirates

Ramsey akifunga bao la kwanza

Aaron Ramsey amekwamisha mpira nyavuni

Oliver Giroud akikimbilia mpira

Pigo: Lukas Podolski ameongeza idadi ya majeruhi Arsenal angalia picha za chini akitolewa uwanjan

No comments: