Balozi Wa Tanzania nchi Marekani Muheshimiwa Liberata Mulamula, Jana October 8, 2013, alikutana na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania ya Washington, DC, Maryland and Virginia (DMV). Balozi alijadili mambo mbalimbali na viongozi hao ikiwa ni pamoja na kutambulishana, ushirikiano kati ya balozi, maofisa wa Ubalozi na Watanzania wanaoishi DMV na Marekani kwa Ujumla. Halikadhalika Balozi alielezea ni jinsi gani serikali na ofisi yake inavyoendelea na kupanga mikakati ya kuwajumuisha wanaDiaspora katika kuleta maendeleo ya nchi. Kutoka Kushoto ni Shamis Abdulla,Asha Nyanganyi (Wajumbe wa kamati), Genes Malasy (Muweka Hazina), Elias Mshana (Mjumbe wa kamati), Iddi Sandaly (Raisi), Balozi Liberata Mulamula, Raymond Abraham( Makamu Raisi), Hamza Mwamoyo (Mjumbe wa Bodi) na Amos Cherehani (Katibu).
No comments:
Post a Comment