ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 7, 2013

NEW YORK TANZANIA DREAM SOCCER TEAM MAMBO YA ZIDI KUONGEZEKA SIKU HADI SIKU UKO BROOKLYN, NY

New York Tanzania Dream Soccer Team Ukodak wa Pamoja, kabla ya mazoezi siku hadi siku team inazidi kuimarika na vijana wana jituma mazoezini ili kuhakikisha team inakuwa na kikosi imara kama Duracel battery. Team inajiandaa na safari ya Houston Tx kwenye Thanksgiving. Kinachosubiriwa ni waandaaji wa mechi hizo ku confirm. Wafadhili wa Team wamesha ahidi ticket 15 hadi Houston TX. Kwa hiyo vijana wanafanya mazoezi kwa khali na moyo wote ili kujenga team ya ushindani ukisikia phah........
Vijana wakipasha kabla ya kuanza mazoezi dimbani
Hapa ni Hamza Mandia rasta kipara akipiga jaramba pembeni ni beki asie chafuka Childboy.
Kama unavyoona mwenyewe kuna winga tereza Ommy kulia na katikati ni Salum Akida Stam wakipasha 
Ankal aka New York One akipiga jaramba akiwa golini ananikumbusha enzi za Mwameja kwa wale wenye kumbukumbu ya jina hilo wana weza kuelewa Mwameja alikuwa nani.
Childboy akipambana  na Captain wa Team Mubah a.k.a (hitokee tu) Kwa picha zaidi nenda chini
Chini na juu ni Childboy beki asie chafuka akimtoka mtu
Katibu wa NYTC Mr Mhella akionyesha ufundi wake
Chini na juu ni Rasta kipara akionyesha utaalamu wake utaipenda tu New York Tanzania Dream Soccer Team ni mambo yote
Chini na juu ni Ny, mwenyewe akionyesha kiwango chake siyo kama kazi yake ni kushika Camera ya Vijimambo na Technical wa T.E.S tu hata akiwa uwanjani habari ndiyo hii. 
Chini na juu ni Ally Sadik (Mido) wa Kikwajuni zama hizo akionyesha uwezo wake, 
Ally a.k.a Myemen akitoshana ubavu na rasta kipara unaweza kuona ni kiasi gani team inavyo fanya mazoezi kwa moyo, Picha ya chini ni Rasta na Myemen aka Valencia.
Akida Jr akijifua nae tayari kwa kalinye kalinye yeyote itakayo jipendekeza mbele ya safari
Najma Akida akijifua. samaki mkunje angali mbichi
Vitu hivyo hapa achomoki mtu anaetoka moto anaingia sindano ukibwaga mboga wa2 wana mwaga ugali ngoma bila bila. live bila chenga. 
Mchezaji mwalikwa Jeff kutoka Tanzania akionyesha ufundi wake bila kukunja goti
Mido ana jiweka sawa kabla ya ubavu kwa ubavu kuanza. 
Najma na Akida Jr wakipata ukodak baada ya mazoezi

No comments: