-MeTL Group watangaza zawadi nono kwa atakayefanikishwa kukamatwa kwake
KAMPUNI YA MOHAMMED ENTERPRISES TANZANIA LIMITED (MeTL) Makao Makuu inatangaza kwa umma wa watanzania kwamba Meneja wa MeTL tawi la Iringa Mr Aamir Iqbal anatafutwa na mwajiri wake kwa kosa la wizi wa mamilioni.
Mr Iqbal (pichani juu) aliyekuwa Meneja wa tawi la MeTL Iringa anatuhumiwa kwa kosa la kumwibia mwajiri wake mamilioni ya pesa yeyote atakayewezesha kukamatwa au kutoa taarifa zake katika kituo chochote cha Polisi zawadi nono itatolewa.
Tukio hilo lililotokea jana mchana Iringa limeripotiwa Kituo Kikuu cha Polisi Iringa na RB ya Polisi ni ref no. IR/RB/7229/2013.
Kampuni ya MeTL Group itatoa zawadi nono kwa yeyote atayefanikisha kukamatwa kwake.
Au piga simu namba: 0755 030 014 , 2118930/1, 0713 324 332, 0715 030 024
Hati ya kusafiria ya Aamir Iqbal.
Kibali cha kazi cha Meneja huyo.



2 comments:
Hivi walikosa watu wanaostahili kuwa branch managers Tanzania nzima, wakaenda kumtafuta mtu Pakistani? Waache waibiwe tu, tena wawafilisi kabisa.
Ndo mkomeeee kupapatikia wageni Wenye rangi nyeupe! Hata nao wana njaa kaali vilee vileee! Ingekuwa mzawa wa TanZania mngempata kirahisii sasa huyu Kama ameshakwenda kwao Pakistan mtamuonea waaapi???? Jifunzeni kutoa aajira kwa Watanzania wenzenu na si kupapatikia wakuja Kisa wana rangi ya tafauti!!! Haya poleni kwa kuuibiwa! Mmmh
Post a Comment