ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, November 12, 2013

RAIS KIKWETE AKATAA DONGE LA DHAHABU LENYE GRAM 227

Rais Kikwete arudisha zawadi ya dhahabu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameirudishia Kampuni ya Nyamigogo Grand Vezir Holdings ya Mkoani Geita zawadi ya gramu 227 za dhahabu safi akielekeza kuwa zawadi hiyo itumike kuwasaidia watoto yatima. 
Rais Kikwete ametoa maelekezo hayo leo, Jumatatu, Novemba 11, 2013, baadaya kukabidhiwa zawadi ya dhahabu hiyo wakati wa sherehe ya kuzindua mgodi wa uchenjuaji dhahabu wa kampuni hiyo nje kidogo ya mji mdogo wa Kharuma ambako ndiko makao makuu ya wilaya mpya ya Nyang’hwale,Mkoa wa Geita.
Gramu hizo 227 ambazo ni sawa na aunzi nane zina thamani ya Sh. milioni 16 kwa bei ya sasa ya soko la dhahabu duniani.
Baadaya kukabidhiwa zawadi hiyo, Rais Kikwete ameuliza: “Sasa nifanye nini na zawadi hii? Nawarudishieni hii dhahabu, iuzeni popote mnakotaka na fedha itakayopatikana tutawapa watoto yatima.”

Akizungumza na wananchi katika mgodi huo, Rais Kikwete ameupongeza uongozi wamgodi huo akisema kuwa umeongeza thamani ya dhahabu na ya maisha yawananchi katika eneo hilo nje ya mji mdogo wa Kharuma.

Hatahivyo, Rais Kikwete ameushauri uongozi wa mgodi huo kufanya jitihada za kuboresha teknolojia inayotumika. “Mmefanya vizuri sana na mgodi huu ni mradi wa maana sana kwa kuongeza thamani ya dhahabu na kuboresha maisha ya wananchi katika eneo hili. Ubunifuhuu unastahili pongezi.”

Ameongeza Rais Kikwete: “Lakini lazima tuboreshe teknolojia. Teknolojia inayotumika kwenye mgodi huu bado ni ya zamani kidogo. Hii ni sawa na hadithi ya mtu mwenye chongo katika jamii ya vipofu watupu. Yeye anaonekana kama mfalme.”

Mgodi wa Nyamigogo ambao ni mgodi wa marudio kwa maana ya kwamba unazalishadhahabu kutokana na mchanga ambao huko nyuma umepata kufuliwa nakutoa dhahabu, ulianzishwa mwaka 2011 na mpaka sasa zimewekezwa kiasicha Sh.bilioni 1.6 katika uendelezaji wa mgodi huo.

Risala ya uongozi wa mgodi huo inasema kuwa mgodi huo unaozalisha kiasi chagramu kati ya 500 na 600 kwa mwezi na unaajiri watu 45 wakiwemo wanawake 10.

Tokea kuanzishwa kwake, mgodi huo umekuwa unaunga mkono shughuli za jamii inayouzunguka ikiwa ni pamoja na kujenga zahanati na madarasa yashule katika vijiji viwili.

Rais Kikwete amezindua mgodi huo ikiwa sehemu ya kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo katika ziara yake rasmi ya kikazi katika Mkoa waGeita, moja ya mikoa minne ambayo aliianzisha mwaka jana. Mikoa mingine ni Simiyu, Njombe na Katavi.

Ziara hiyo ya siku tano inamalizika kesho, Jumanne, Novemba 12, 2013, na mbali ya kuzindua mgodi huo, Rais Kikwete leo amepokea ripoti ya maendeleo ya Wilaya ya Nyang’hwale na kuhutubia mkutano wa hadhara katika mji mdogo wa Kharuma uliohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi. 

Rais kikwete anatarajia kufanya majumuisho ya ziara yake Jioni ya leo!

Imetolewana:
Kurugenziya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dares Salaam.
11Novemba, 2013

4 comments:

Anonymous said...

Any presidential gift does not go to the president himself but to the presidecy na ni mali ya taifa sio raisi binafsi. Hata Bush alivyoondoka madarakan zawadi zota alizopewa ziko zilizobaki white houise na zingine zimeenda kwenye library yake. Bongo tuache miyeyusho

Anonymous said...

WALA SI UONGO BONGO TUACHE MIYAYUSHO LAKINI HII NI JANJA YA SIASA BONGO HIZI ZAWADI HUWA WANAZICHUKUA NA HATA HUKU MAREKANI WANACHUKUA BWANA HIYO LIBRARY ULIYOSEMA MKUU HAPO JUU YA BUSH HIZO ZAWADI ZI AMEZIWEKA KWENYE LIBRARY YAKE AMAA SO KWA KIFUPI TUACHENI MIYAYUSHO DUNIANI POTE BORA ZAWADI YA DHAHABU KULIKO PESA NDO MAANA HUKU MAREKANI WANATAKA WATU WASIWE NA DHABABU WAWE NA PESA UKENDA KATIKA PAWN STORE NA MITAANI NY UTASIKIA KILA LEO KAMA UNA DHAHABU YAKO IMEHARIBIKA IMEVUNJIKA WE LETE TU TUTAKUPA PESA KWA HIYO DHAHABU UNADHANI WAJINGA HAWA WATU TUACHENI MIYAYUSHO JAMANI WATU WAMESHAFUNGUA MACHO.

NA NIMECHEKA KWELI KWA KAULI YA TECHNOLOGIA ETI CHONGO ANAONEKANA MFALME KWA WATU VIPOFU NA NI KWELI JAMII YA WADANGANYIKA NDO WANAVYOONA HIVYO KILA LEO WAKUU WETU WAKO MAJUU KUUOMBA UMBA NA UFISADI UNAKWENDA MBELE WALALA HOI WANAKAA KIMYA KAMA VIPOFU AU SIJUI NDO CHONGO WAO WANAONA KIDOGO SI FULL VISION HA HA HA KAZI IPO MUNGU YUPO LAKINI

Anonymous said...

Unafiki mkubwa, he was given as a President, so he should have taken it and then himself give it to hao maskikini au inakuwa mali ya taifa. Hawakumpa kama JK bali as the President.

Iko kazi Bongo, labda wangewire kwenye account yake.

Anonymous said...

zipi ambazo alichukua kimya kimya?
Can we do a stock take?