Nimetoka makao makuu ya polisi, upelelezi, kuandika statement kuhusu vitisho dhidi yangu kufuatia hekaya inayoitwa "Ripoti ya Siri ya Zitto Kabwe".
Chanzo cha hekaya sasa kinabadilishwa kutoka makao makuu ya CHADEMA na kuwa ni usalama wa Taifa au CCM.
Wahusika waendelee kuhamisha chanzo lakini wajue watasakwa na kukamatwa na kuburuzwa mahakamani. Nimewashitaki kwa kunitishia maisha. Ninawashitaki kwa kunichafua kwa tuhuma za uongo.
Ninafanya haya kwa lengo la kuhakikisha kuwa siasa za kuzushiana na kusambaza uongo zinakuwa na gharama kubwa.
1 comment:
Kaka Zitto wewe bado kijana si unazijua siasa za Tanzania, ukiwa msemaji wa haki na kukomboa waTz lazima watatafuta mbinmu za kukunyamazisha!!, Mwenzetu DR. .. umeona walilolifanya?? Ndugu yangu hata ile ruzuku ya vyama uliyokomaa nayo si unaona wamekudunga sindano!!
mbona imeishia hewani, sasa swala la mabillioni lina hatari kwani wameguswa wenyewe!!
Post a Comment