ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 25, 2013

Membe awashauri Watanzania walioko nchini Sudan Kusini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amewataka Watanzania waishio Sudan Kusini waanze kuondoka na kwenda katika ubalozi wa Kenya mjini Juba.
Akizungumza kwenye mahojiano katika kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na ITV, Membe alisema ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa hali ya usalama nchini humo ni tete kutokana na mapigano yanayoendelea kati ya majeshi ya serikali yanayomtii Rais Salver Kiir na wapiganaji wanaoungwa mkono na mpinzani wake, Riek Machar.
Wiki moja iliyopita yalizuka mapigano kati ya wanajeshi watiifu wa Rais Kiir na mpinzani wake Machar anayedaiwa kupanga njama za mapinduzi.

Membe alisikitishwa na migogoro inayoendelea ndani ya nchi za Afrika na kusema wakati umefika viongozi wa nchi za Afrika kuwa na busara za uongozi ili kuepusha migogoro katika nchi zao.

Wakati Membe akiwataka Watanzania kujihifadhi katika ubalozi wa Kenya, baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani zimeshawataka raia wake kuondoka nchini humo kwa ajili ya kuepuka mapigano hayo ambayo wachambuzi wanasema huenda yakageuka kuwa vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Sudan Kusini ilijitenga na Sudan na kuwa nchi kamili mwaka 2011kufuatia mapigano ya kutaka kujitenga yaliyochukua zaidi ya miongo miwili.
SOURCE: NIPASHE

3 comments:

Anonymous said...

Unawashauri??badala ya kutuma ndege ya kijeshi kwenda kuwaokoa raia wa tz huko kama zinazovyofanya nchi nyingine kuokoa raia wake....hebu ifike mahali maisha ya wa-tz wote yawe na thamani mbele zenu viongozi..!

..hivi kutoa ushauri kama uliosema hata mtoto wa sekondari si anaweza kuutoa..wewe ni Waziri hebu basi uwe unafanya mambo kama waziri.

mdau UK

Anonymous said...

Wakijihifadhi then what next?

Anonymous said...

Mdau wa UK umenenaa kabisaa'!! Unashauri wakati maisha ya Raia wa Kitanzania yapo matatani? Namie nakushauri uwajibike kwa matendo Kama Waziri wawa Tanzania! Asanteeeeee