ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, December 25, 2013

THELUJI, MVUA ZA BARFU, BARIDI KALI VYALETA ADHA KWENYE CHRISTMAS YA MWAKA HUU NCHINI MAREKANI

Majimbo mengi yamekumbwa na tofani ya theluji, mvua za barafu ikiwemo baridi kali  na kuleta kero kwa familia nyingi ambazo hutumia muda huu wa sikukuu ya Christmas kujumuika pamoja. Theluji iliyoanguka na hali ya hewa kuwa baridi sana imesababisha watumiaji wa barabara kuwa na wakati mgumu kutokana barabara kuwa barafu zilizosababisha ajali nyingi kutokea na watu wengi mwaka huu wanakula Christmas kwenye giza baada ya tufani ya theluji kusababisha kukatika kwa nyaya za umeme majimbo kama Michigan, mji wa Cleveland, Ohio na majimbo yaliyopo magharibi ya kati Illinois, Minnesota huko ni balaa, New York na hapa DMV baridi nako ni kali sana japo hakuna theluji iliyoanguka.
Barabara kuteleza kutokana na theluji iliyoganda na kusababisha ajali kama unavyoona mwenyewe.
Walitumia usafiri wa anga nako hakukuwa rahisi kutokana na ndege nyingi kusogeza muda mbele wa kuondoka au kusitisha kabisa safari hizo kutokana na majimbo wanayoelekea kukubwa na tufani hiyo.
Mvua za barafu zilizosababisha miti kuonekana na muonekano huu kama unavyoonekana kwenye picha hii.
Juu na chini barabara haziebesheki kutokana na barabara kuteleza kulikosababishwa na theluji kuganda na kuwa barafu kutokana na majimbo hayo kuwa na baridi kali.

No comments: