Hiki “Kiswanglish” kimeendelezwa kwa ndugu zetu wa Kenya miaka mingi; hadi wakachanua "Shenge" - Wenzetu lakini wametuzidi mawili. Moja wanakijua Kiingereza (hata Mkenya asiyesoma sana mitaani, akihojiwa anazungumza Kiingereza fasaha), vizuri sana. Pili, wanakijenga Kiswahili vyema hasa vyuoni na mashirika mazuri ya kuchapisha vitabu kama Sasa Sema (Longhorn) kiasi ambacho baadhi ya waandishi wetu wakubwa (Adam Shafi na Prof Said A Mohammed wanachapisha riwaya zao kule Sisi je? Wangapi tunaandika na kuzungumza Kiingereza fasaha siku hizi? Wazaire (Congo DRC); hali kadhalika. Wale wa miji mikubwa kama Kinshasa wanaongea "Kinois"(tamka “Kinwaa”). Huu ni mseto wa Kilingala, Kingwana (Kiswahili cha Kikongo) na Kifaransa. Lakini ukichunguza wenzetu nao wanamudu Kifaransa fasaha, hata wale wasiofikia chuo kikuu. Kusisitiza Kiswanglish si maendeleo kilugha, Tanzania. Ujuzi wa lugha moja (Kiswahili au Kiingereza hata Kikabila ) umelegea, umedhoofu, umedidimia miaka ya karibuni. Kutokana na tatizo hili, kusisitiza lugha mseto (isiyokaa sawa) kutatufanya, wale tusiofahamu Kiingereza fasaha (lugha ya kimataifa ya kibiashara na kitaaluma) kutetereka tunapotafuta kazi, au tunapoongea (au kuhutubia ) mirengo ya kimataifa. Shuhudia mwenyewe video zinazosambaa mitandaoni za baadhi ya Watanzania katika mikutano ya kimataifa- tukiongea Kiingereza. Aibu tupu. Hilo ndilo tatizo la Kiswanglish. Si kwamba ni vibaya "lugha" hiyo (kama ni "lugha" , lahaja au nahau) kukua, bali kwamba wale wanaoitumia watakuwa si wala nyama, wala si watafuna majani.
1 comment:
Hiki “Kiswanglish” kimeendelezwa kwa ndugu zetu wa Kenya miaka mingi; hadi wakachanua "Shenge" - Wenzetu lakini wametuzidi mawili. Moja wanakijua Kiingereza (hata Mkenya asiyesoma sana mitaani, akihojiwa anazungumza Kiingereza fasaha), vizuri sana. Pili, wanakijenga Kiswahili vyema hasa vyuoni na mashirika mazuri ya kuchapisha vitabu kama Sasa Sema (Longhorn) kiasi ambacho baadhi ya waandishi wetu wakubwa (Adam Shafi na Prof Said A Mohammed wanachapisha riwaya zao kule
Sisi je? Wangapi tunaandika na kuzungumza Kiingereza fasaha siku hizi? Wazaire (Congo DRC); hali kadhalika. Wale wa miji mikubwa kama Kinshasa wanaongea "Kinois"(tamka “Kinwaa”). Huu ni mseto wa Kilingala, Kingwana (Kiswahili cha Kikongo) na Kifaransa. Lakini ukichunguza wenzetu nao wanamudu Kifaransa fasaha, hata wale wasiofikia chuo kikuu.
Kusisitiza Kiswanglish si maendeleo kilugha, Tanzania. Ujuzi wa lugha moja (Kiswahili au Kiingereza hata Kikabila ) umelegea, umedhoofu, umedidimia miaka ya karibuni. Kutokana na tatizo hili, kusisitiza lugha mseto (isiyokaa sawa) kutatufanya, wale tusiofahamu Kiingereza fasaha (lugha ya kimataifa ya kibiashara na kitaaluma) kutetereka tunapotafuta kazi, au tunapoongea (au kuhutubia ) mirengo ya kimataifa. Shuhudia mwenyewe video zinazosambaa mitandaoni za baadhi ya Watanzania katika mikutano ya kimataifa- tukiongea Kiingereza. Aibu tupu. Hilo ndilo tatizo la Kiswanglish. Si kwamba ni vibaya "lugha" hiyo (kama ni "lugha" , lahaja au nahau) kukua, bali kwamba wale wanaoitumia watakuwa si wala nyama, wala si watafuna majani.
Post a Comment