Balozi Tuvako Manongi akiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Hifadhi ya Mazingira, Bw. Robert K Sweeney ( Mb)
Wengi waliojitokeza kusikiliza majadiliano hayo.
Mauaji holela ya tembo na biashara haramu ya tembo ni suala linalowagusa watu wa kada mbalimbali
Sehemu ya washiriki wakifuatilia majadiliano hayo ambayo pia yaliwahusisha wataalam kutoka Asasi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na hifadhi ya mazingira na mali asili.
Muwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi akizungumza katika mkutano huo ambapo pamoja na mambo mengine alielezea jitihada zinazofanywa na serikali katika kudhibiti ujangili na biashara haramu ya pembe za tembo
Bw. William C. Woody ( mwenye tai ya njano) Naibu Mkurugenzi kutoka Ofisi inayosimamia sheria akiwa na Bw. Richard G. Ruggiero Mkuu wa Kitengo cha Afrika, Uhusiano wa Kimataifa , huduma za Samaki na Wanyamapori nchini Marekani. Wakitoa ushuhuda wao kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo katika udhibiti na usimamizi wa sheria zinahusu biashara ya pembe za tembo na wanyama wengine walio katika hatari ya kutoweka
Mwenyekiti wa Kamati ya Hifadhi ya Mazingira ya Bunge la New York, Bw. Robert K. Sweeney akiongoza mkutano ( public hearing) aliouandaa kujadili na kubadilishana mawazo kuhusu ufanisi wa sheria na kanuni zinazodhiti biashara ya pembe za tembo katika New York, mkutano huo ulifanyika siku ya Alhamis. New York ndiyo inayoongoza katika Marekani kwa kuwa kituo cha Biashara ya pembe za tembo na biadhaa zake katika mwaka 2012 pembe za tembo zenye thamani ya dola milioni mbili zilikamatwa
KUJUA ZAIDI ALICHOSEMA BALOZI MANONGI BOFYA SOMA ZAIDI
Na Mwandishi Maalum
Wakati
Serikali ya Tanzania ikijipanga kwa utekelezaji wa awamu ya pili
ya Operesheni Tokomeza Ujangili, Bunge la New York, nchini Marekani, kupitia Kamati yake ya Hifadhi ya Mazingira linajipanga
kuangalia namna ya kuboresha
ufanisi wa sheria na kanuni zinazolinda na
kudhibiti biashara ya pembe za Tembo na wanyama wengine.
Katika
kutekeleza azima hiyo, jana alhamisi, hapa
New York, Mwenyekiti wa Kamati ya Hifadhi ya Mazingira Robert K. Sweeney(Mb) aliitisha
mkutano ( public hearing) uliokuwa na lengo la kusikiliza michango na maoni kutoka kwa wadau
mbalimbali, michango ambayo kwa namna moja
ama nyingine itachangia katika
uboreshaji wa sheria na sera zilizopo hivi sasa.
Mwakilishi
wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja
wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi,
alikuwa miongoni mwa waalikwa waliopewa fursa ya siyo tu, kutoa ushuhuda wa ukubwa wa tatizo la ujangili na adhari zake. Lakini
pia kuelezea nini mamlaka husika zinafanya kukabiliana na tatizo hilo na kutoa
ushauri na mapendekezo ya hatua zaidi
za kukabiliana na changamoto hiyo.
Pamoja
na kuwasilisha ushuhuda wake na hatua zinazochuliwa na
serikali , Balozi Manongi pia alijibu
maswali mbalimbali yaliyoulizwa na
Mwenyekiti wa Kamati na wajumbe wengine.
Akifungua mkutano huo,
Mwenyekiti wa Kamati ya Hifadhi
ya Mazingira, Robert Sweeney alisema. Tembo wa Afrika ambao ni urithi wa dunia na
muhimu kwa ustawi wa mwanadamu wamo hatarini kutoweka kama hatua
madhubuti zaidi hazitachukuliwa.
Akatahadharisha kuwa uwindaji haramu wa tembo kwaajili ya pembe zao siyo tu
kwamba umekidhiri na kuongezeka badala ya kupungua, lakini
pia hivi sasa mitandao ya mbalimbali ya uhalifu na ugaidi inajiingiza kwa kasi katika eneo hilo.
“
Hali ni mbaya, mauaji ya tembo yanaongezeka,
tunahitaji kuchukua hatua zaidi na ndio maana nimeitisha mkutano huu ili kuangalianamna gani sheria na kanuni zetu zilizopo
zitaweza kuwa na ufanisi zaidi katika
kudhibiti biashara ya meno ya tembo” akasema Mwenyekiti.
Akabinisha
kwamba katika New York biashara ya meno
ya tembo inadhibitiwa kupitia sheria na kanuni mbalimbali lakini
pamoja na sheria hizo, bado
New York inaongoza katika Marekani kwa kuwa kituo cha biashara ya pembe za tembo.
Akatoa
mfano kwa kueleza kuwa katika mwaka 2012,
pembe za tembo zenye dhamani ya dola 2 milioni ambazo
ziliingia New Yor kwa njia zisizo
halali zilikamatwa na kutekezwa. Na kwamba tatizoni kubwa.
Akitoa ushuhuda wake, Mwakilishi wa Tanzania Balozi Manongi,
alielezea kwa kina namna ambavyo
Serikali ya Tanzania chini ya
Uongozi wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete inavyoshughulia tatizo la ujangili na biashara haramu ya
pembe za tembo.
Akasema utekelezaji wa sheria, será na kanuni
mbalimbali unachangamoto nyingi lakini
Serikali haijakata tamaa imejipanga vyema ili kuhakikisha kwamba uridhi
huo wa Tanzania na dunia kwa ujumla haupotei kabisa
Akasema tisho la kutoweka kwa tembo si la
nadharia ni la kweli kabisa na kwa sababu hiyo akasema Tanzania inaunga mkono juhudi za kimataifa za kukabiliana na ujangili na itakuwa tayari kushirikiana na wadau mbalimbali kuokoa Tembo
wa Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Akarudia
wito ambao umekuwa ukitolewa mara kwa
mara na Mhe. Rais
Kikwete kwamba, njia mojawapo na muhimu ya kukabiliana na biashara ya
pembe za tembo ni kudhibiti soko la bidhaa hiyo.
Hata
hivyo akasema , umaskini pia
unachangia kwa baadhi ya watu kujihusisha na kushirikiana na majangili kama
njia ya kujipatia kipato.
TESTIMONY BY TUVAKO N. MANONGI, AMBASSADOR AND
PERMANENT REPRESENTATIVE OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA TO THE UNITED
NATIONS, NEW YORK AT A PUBLIC HEARING ON “THE EFFECTIVENESS OF NEW YORK’S
RESTRICTIONS ON THE SALE OF IVORY”, NEW YORK, 16 JANUARY 2014
Mr. Chairman,
Distinguished Members
1. At
the outset permit me to thank you for holding these hearings and for inviting
us to add our voice to your effort to strengthen “the effectiveness of New
York’s restriction on the sale of ivory”.
2. It
has rightly been stated that elephants – the largest remaining land mammal on
earth – are today facing one of the greatest crises to hit the species in
generations as a result of a dramatic rise in poaching for their ivory. Efforts
such as those being expended by this Committee and the State Assembly are
important and necessary in our global effort to save the African elephant
population from extinction. The scale of the problem is such that the President
of the United Republic of Tanzania, H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, in September
2013 at the United Nations, here in the city, called for the international
community to close down ivory markets.
3. In
my country, the slaughter of elephants and the seizure of illegal ivory have
soared in the recent past. Voracious markets, particularly in Asia, coupled
with under-resourced and under-equipped wild life protection units have placed
elephant herds at risk throughout Africa. We testify to the fact that illegal
trade in ivory is having a devastating impact on the elephant population in the
continent. It also possesses a threat to people, as poachers are gun down
families and even game wardens.
4. According
to a recent report by the Secretariat of the Convention on International Trade
in Endangered Species (CITES) 22,000 elephants were killed in 2012 compared to
25,000 that were killed in 2011. The Wildlife Conservation Society (WCS)
estimates that 96 elephants are killed each day in Africa. It is troubling to
note that most of the slaughter is happening in Tanzania and in neighboring
Kenya, which like my country is also a source and transit State for ivory
smuggled from landlocked countries in the Great Lakes Region of Africa,
including those countries afflicted by conflicts. The illicit ivory is mostly
destined to black markets in Asia where it is deemed as “white gold”.
5. At
the African Elephant Summit held early last December 2013, it was observed that
current elephant poaching in Africa remains too high and could lead to
extinctions if the present killing rates are not reversed. Incidentally, the
high poaching levels are mirrored by the ivory trafficking figures as tracked
by CITES.
6. These
circumstances call for urgent and resolute actions at national, regional and
international levels to combat the flourishing wildlife trafficking. In
addition, they demand a multidimensional approach ranging from law enforcement,
advocacy, and stringent trade measures at all levels to curb illicit trade in
ivory. They also require investments in, and transfers of, relevant
technologies and knowledge on conservation of endangered wildlife.
7. Last
year, during his visit to the United Republic of Tanzania, President Obama
characterized wild life trafficking as “an international crisis that continues
to escalate”. The President committed the cooperation of the United States with
Africa in combating the criminality. Consequently, his Executive Order 13648 on
Combating Wildlife Trafficking, commits, in appropriate cases and upon request,
to assist those government experiencing wildlife trafficking. Tanzania has
sought such support with a view to strengthening our own enforcement mechanisms
to stop poaching and arrest the illicit trade.
8. What
is it that Tanzania is doing? We have in place a policy and legal framework for
protecting wildlife in the country, namely the Wildlife Act of 2009 together
with its Regulations and subsidiary legislations and the Wildlife Policy of
Tanzania. However, in spite of this framework, the country is experiencing a
rise in poaching incidents that have drastically reduced our elephant
population. In light of this
extraordinary situation, the Government resorted to unprecedented measures by
launching a countrywide special anti-poaching operation last October 2013.
9. The
operation apprehended 1,030 suspects together with a cache of around 1,600
military and civilian weapons. It also captured huge ivory stockpiles,
including those that had reached seaports for shipment to foreign destinations.
Some suspects have been arraigned in court while investigation is pending for
others. The second phase of this operation will commence soon to address
continuing poaching which in the month of December 2013 alone claimed the lives
of over 60 elephants. The fight must continue as long as the danger persists,
and it does!
10. Our interventions must aim at stopping the
massacres being perpetrated against elephants and other endangered species. We
must deploy all means at our disposal to achieve the objective. We need to
undertake more vigorous aerial surveillance, putting to use the technologies at
our disposal such as satellite and unmanned aerial vehicles (UAVs). We need to
scale up elephant tagging and strengthen game rangers patrols. Most critically,
we must scale up public sensitization to participate and assume ownership and
leadership in the fight against wildlife trafficking. We believe international
assistance is vital in enabling African countries to save their endangered
wildlife, which is a common human heritage.
11. We
applaud the recent move by the United States to destroy 6 tons of ivory seized
over 25 years. This move sends a clear message to the criminal gangs that
international resolve to stump the illicit trade is firm and growing. We have
seen similar actions by some Asian countries, namely China and the Philippine
as well as in Africa.
12. I must also say that in our view, we also need
to address the underlying causes of illicit trade in ivory. Poverty is among
the chief drivers of the illicit trade. It exposes the poor to criminal
networks that exploits the natural resources of the continent, fueling
conflicts and instability to feed the ever-growing demand for ivory in global
markets. Needless to say, poor governance and political instability is another
contributing factor. Organized criminals flourish in places with fragile or
non-existent government institutions as witnessed in some conflict and
post-conflict countries in the continent. It is therefore imperative that we
must also forge broader effort to address the root causes of such instability,
including through the support of institutions, rule of law and enforcements
mechanisms.
13. Finally,
we must enhance our efforts to combating trans-national organized crime.
Wildlife trafficking is increasingly associated with rebel and terrorist groups
such as the Lord’s Resistance Army (LRA) and Al Shabaab, an Al Qaeda terrorist
cell in East Africa. The cocktail of poverty, anarchy and trans-national
organized crime is extremely explosive and destructive. Groups such Al Shabaab
should not be allowed to mutate as they have done in the past decade. These
have moved from staging a rebellion in Somalia to engaging in piracy and armed
robbery at sea, to supporting armed groups in the Democratic Republic of the
Congo (DRC) and now into poaching. It in
this regard that President Kikwete regrettably noted that elephants have become
the latest conflict resource. New York City can make a difference in saving
elephants.
14. In the face of all these challenges that need
to be overcome, there are still rays of hope. Today there is expanding
international cooperation and growing national awareness and apprehension that
is paving way towards improved law enforcement and the reduction of demand for
ivory. We owe it to ourselves to do more to curb the disturbing rise in
poaching and illegal trade in ivory and other endangered animals. This must be
our calling and our destiny in the interest of our common heritage. We see the
work of this Committee as an important part of the optimism we hold. We also
see your work in enhancing the effectiveness of New York's restrictions on the
sale of ivory as yet another reason why we can all claim, We Love New York! I
thank you for your kind attention.
2 comments:
Kwa kweli Tatizo la kuua Tembo ni janga kubwa. Ni aibu kwa Nchi yetu. Hongera Mhe. Ambassador
yaani inasikitisha sana kuona waliohudhuria hii mada ni wageni (foreigners) ambao mara nyingi ndio wanaokuwa wanakamatwa na usafirishaji haramu wa pembe za ndovu.!? mbona mkutano huu haukutangazwa kwa WATANZANIA WOTE???? naomba mtu wa ubalozi ajibu hili swala. tumechoka kupigwa mchanga wa macho.
Post a Comment