Friday, January 3, 2014

WASHINGTON DC, WAREKEBISHA SHERIA YA KUMILIKI SILAHA, WAMILIKI WOTE WATAKIWA KUSAJILI UPYA

Serikali Washington, DC wamebadilisha sheria ya kumiliki silaha baada ya wamiliki wote kutakiwa kusajili upya silaha zao na mabao watashindwa kufanya hivyo watanyang'anywa silaha zao na sasa wamiliki wote watakua wanaripoti Polisi kila baada ya miaka 3. 

Japo wamiliki wengi wamepinga sheria hiyo mpya wengine wakidai ni kupotezeana muda wengine wakisema kwamba rekodi inaonyesha tangia 2009 hakujatokea uhalifu wa kutumia silaha iliyosajiliwa.

Serikali imebadilisha sheria hiyo kutokana na sheria ya zamani ilikuwa ikiruhusu wakazi wa DC kuhodhi Bunduki . Wasi wasi wa Serikali ni rekodi za wamiliki silaha hizo kupotea kwa sababu wakazi wengi wanapokumbwa na umauti silaha hizo huishia mikononi mwa watu wasiositahili kumiliki bunduki hizo na kutojulikana majina yao kwa hiyo kuanzia sasa Serikali itafuatilia wamiliki wote wa silaha kwa karibu zaidi.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake