ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, February 11, 2014

Mahakama yaamuru jengo karibu na Ikulu lipunguzwe urefu

Baada ya hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alisema ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya hukumu hiyo kutolewa, Kifungu cha 40, namba 1 na 2 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kinawaruhusu kutaifisha jengo hilo.PICHA|MAKTABA

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Makumba Kimweri na Msanifu Mkuu, Richard Maliyaga, kila mmoja kulipa faini ya Sh15 milioni au kwenda jela miaka tisa baada ya kuwatia hatiani kwa matumizi mabaya ya madaraka na kuruhusu ujenzi wa jengo la ghorofa 18 karibu na Ikulu.
Akitoa hukumu hiyo jana, Hakimu Mkazi, Sundi Fimbo alisema jengo hilo lilipaswa kuwa la ghorofa sita na kuamuru kubomolewa kuanzia ghorofa ya saba kwenda juu.
Hakimu Fimbo alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 13 wa upande wa mashtaka, vielelezo 20 vilivyowasilishwa na ushahidi wa utetezi uliotolewa na washtakiwa wenyewe, upande wa mashtaka ulithibitisha pasipo shaka mashtaka dhidi ya vigogo hao waliodaiwa kuruhusu ujenzi wa ghorofa 18.
Hivyo aliwahukumu washtakiwa hao kila mmoja kulipa faini ya Sh5milioni au kutumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kila kosa lililokuwa likiwakabili. Kila mshtakiwa alilipa kiasi cha Sh15 milioni mahakamani hapo na kuepuka kifungo.
Baada ya hukumu hiyo, Mwendesha Mashtaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alisema ndani ya kipindi cha miezi sita baada ya hukumu hiyo kutolewa, Kifungu cha 40, namba 1 na 2 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kinawaruhusu kutaifisha jengo hilo.
Washtakiwa hao walikuwa wakitetewa na Mawakili Majura Magafu na Paschal Kamala.
MWANANCHI

1 comment:

Anonymous said...

Jamani mahakama na walalamikaji mlikuwa wapi siku zote kuona hili mpaka leo jengo tayari limeisha.
kwani hakuna sheria zinazoruhusu ni umbali gani mtu anaruhusiwa kujenga kutoka Ikulu? mambo ya 10 percent yatamaliza nchi yetu