ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 24, 2014

MLIPUKO UNAODHANIUPDATES: BOMU WATOKEA ENEO LA MKUNAZINI HUKO ZANZIBAR ,WANAJESHI WAFIKA ENEO LA TUKIO

 Eneo ambalo limeharibika kwa kuchimbika na kitu kinachozwaniwa ni mripuko katika eneo la Mkunazini, na kuleta mtafaruku na tukio hilo la mripuko katika majira ya mchana, Katika mripuko huo hakuna mtu aliyepata majadhara na hakuna uharibifu wa majengo katika eneo hilo.   

 Mkuu wa Wilaya ya Mjini Unguja, Mhe. Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Kiongozi wa Kanisa la Mkunazini, Ndg. Nuhu Salanya, na Maofsa wa JWTZ , katika eneo la tukio na kutoa maelekezo kwa Uongozi wa Kanisa alipofika katika eneo la tukio kuangalia athari na uharibifu uliotokea katika eneo hilo wakati wa mripuko huo.  

Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Makamanda wa JWTZ waliofika eneo la tukio kuagalia na kuchunguza tukio hilo la mripoko katika eneo la Mkunazini jirani la Kanisani.
Maofisa wa JWTZ wakiangalia eneo la tukio lililochimbika kutokana na kitu kinachodhaniwa ni bomu.

PICHA NA ZANZINEWS 

1 comment:

Anonymous said...

Ah! Zanzibar umekosa nini. Tukio hili imekua mwao. Kijishimo hicho hata hakieleweki kimesambaza habari chafu dhidi yako dunia nzima.

Unatafutiwa sababu ubambikiziwe ugaidi na hawa vishuka wanaokupatia visenti vya mishahara wakimbie. Zanzibar umekua public toilet kila mwenye chafu lake aingie afanye aondoke. Umekosa udhibiti wa milango yako atakae na aje, unategemea ukweni kwa usalama wako.

Umejisahau. Hujisafishi. Unategemea Karima ya ukweni. Upangiwe. Umejidharau. Unadharauliwa. Unashutumiwa kwa mabaya. Unachekelea. Unasubiri ukweni. Uamuliwe hatima yako. Unapakwa machafu unachekelea. Huna nguvu za kuzuia hata harufu na uchafu upakwao siku hadi siku.

Kunya anye Kuku. Akinya Bata kahara.

I love Zanzibar.