Kwa ufupi
Umekuwa tegemeo pia kiuchumi kwa wakazi wengi;
wamekuwa wakiendesha shughuli za uvuvi na kilimo cha umwagiliaji.Kuna
viumbe vingi vinavyotegemea maji kama vile samaki, mamba na viboko.
Uhai wa Hifadhi ya Taifa ya
Ruaha (RUNAPA) unategemea sana uwapo wa Mto Ruaha Mkuu unaokatisha katika hifadhi hiyo.
Umekuwa
tegemeo pia kiuchumi kwa wakazi wengi; wamekuwa wakiendesha shughuli za
uvuvi na kilimo cha umwagiliaji.Kuna viumbe vingi vinavyotegemea maji
kama vile samaki, mamba na viboko.
Hali kadhalika, uzalishaji
umeme katika mabwawa ya Mtera na Kidatu unategemea maji ya mto huo.
Licha ya umuhimu huo, utafiti unaonyesha kuwa mto huo unakauka kwa kasi
Siku
hadi siku kiwango cha maji katika mto huo kimekuwa kikipungua. Katika
wakati mto hukauka kipindi zaidi, sababu kubwa ni shughuli za binadamu
zinazofanywa kando kando ya vyanzo vya maji au kwenye vyanzo vya maji
vinavyopeleka maji katika mto huo.
Mto Ruaha Mkuu wenye urefu wa
kilomita 475 unaanzia katika Mlima Kipengere ukimwaga maji katika ardhi
oevu ya Usangu kupitia RUNAPA hadi katika Mto Rufiji.
Mto huu unachangia asilimia 22 ya maji ya Bonde la Rufiji ukiwa na zaidi ya aina 39 za samaki.
Mito
inayochangia maji katika Mto Ruaha Mkuu ni pamoja na Lukosi, Yovi,
Kitete, Sanje, Little Ruaha, Kisigo, Mbarali, Kimani na Chimala ambako
kuna mito midogo ikiwamo Umrobo, Mkoji, Lunwa, Mlomboji, Ipatagwa, Mambi
na Mswiswi.
Mtaalamu wa Ikolojia wa RUNAPA, Paul Banga anasema
Mto Ruaha Mkuu unapata maji yake kutoka mito mikuu mitano ambayo ni
Kimani, Mkoji, Mbarali, Ruaha Mkuu (Upstream), Ndembera na Chimala.
Mito
hii yote huingia kwenye Bonde la Usangu. Baada ya Bonde la Usangu
kujaa, maji hutokea kwenye eneo la Ngiriama katika Mto Ruaha Mkuu ambao
hupita ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Ruaha kuelekea katika Bwawa la
Mtera.
Kupungua kwa maji katika Mto Ruaha Mkuu kulianza kuonekana
miaka ya 1990 hali inayosababishwa na matumizi mabaya ya maji kwenye
ardhi oevu ya Ihefu na Usangu; katika maeneo hayo kumekuwa na kilimo cha
umwagiliaji wa mpunga.
Wakati wa kiangazi, mto huo hukauka kabisa
kabla ya kumaliza kupita katika Hifadhi ya Ruaha jambo linaloathiri
wanyama na mimea sambamba na shughuli za uvuvi na uzalishaji wa umeme
kwenye mabwawa ya Mtera na Kidatu.
Ofisa Maji wa Bonde la Rufiji,
Idris Msuya anasema hali ya upatikanaji wa maji inategemea sana hali ya
mvua na huanza kujaa mwezi Desemba na kufikia kiwango chake cha juu kati
ya Machi na Aprili.
Anaongeza kuwa mabwawa makuu ya kuzalisha
umeme ya Mtera na Kidatu yako kwenye Mto huo ambayo yamesababisha
mabadiliko ya tabia ya mtiririko wa mto.
Kukauka kwa Mto Ruaha
Hifadhi
ya Ruaha imekuwa ikikauka wakati wa kiangazi kati ya Septemba na
Desemba tangu mwaka 1993. Kipindi cha kukauka mto huo kimekuwa
kikiongezeka na kuathiri viumbe wengi.
Msuya anasema kilimo cha umwagiliaji ndicho kinachotumia maji mengi zaidi katika eneo hili.
Watu
wamekuwa wakifanya shughuli za kibinadamu ikiwamo kilimo kama ufyatuaji
wa matofali na kilimo cha vinyungu na umwagiliaji karibu na vyanzo vya
maji au mito.
Mtaalamu huyo wa Ikolojia anasema tangu mwaka 1993 maji yamekuwa yakikauka kwa muda wa miezi mitatu hadi mitano.
Historia inaonyesha tangu kuanza kwa kilimo cha umwagiliaji kwenye maeneo ya Mbarali, maji yamekuwa yakipungua siku hadi siku.
“Baada
ya kufunguliwa kwa mashamba makubwa ya mpunga huko Mbarali ambayo
huendeshwa kwa kilimo cha umwagiliaji hususan Shamba la Mbarali, Kapunga
na Madibira yalipofunguliwa miaka ya 1970 na mwishoni mwa mwaka 1990,
kiwango cha maji kilianza kupungua,” anasema Mtaalamu wa Ikolojia wa
RUNAPA, Paul Banga
Anasema tangu kuanzishwa kwa kilimo hicho hali ya mto huo imekuwa ya kusuasua hatimaye kusababisha kukauka.
Sambamba
na mashamba hayo, mashamba madogo yameongezeka takribani mara nne hadi
tano na wakati ule ukilinganisha na sasa; kutoka hekta 10,000 hadi hekta
45,000-50,000 zinazolimwa na kumwagiliwa kwa sasa.
Anasema vyanzo
vingine ni uduni wa miundo mbinu ya umwagiliaji katika mashamba ya
mpunga yanayoendeshwa kwa kilimo cha umwagiliaji na matumizi
yasiyoendelevu ya maji yanayotumika kwa umwagiliaji wa mashamba ya
mpunga.
Kwa upande wake Msuya anasema kupanuka kwa kilimo cha
mwagiliaji kusikoendana na kiwango cha maji kumechangia kwa kiasi
kikubwa kukauka kwa mto huo.
Hali kadhalika kumekuwa na uelewa
mdogo wa jamii katika usimamizi wa rasilimali za maji. Kwa ujumla kuna
uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji kwa shughuli za kibinadamu. Pia
kupungua kwa maji kunasababishwa na mabadiliko ya hali ya hewa.
Athari
Kukauka kwa mto kunasababisha wanyama kutoka nje ya hifadhi kutafuta maji na malisho kipindi ambacho mto unakuwa umekauka
Kuongezeka
kwa vitendo vya uhalifu hususan ujangili pembezoni na kwenye mpaka wa
hifadhi kutokana na wanyama kutoka nje ya hifadhi na kwenda maeneo
ambayo usimamizi siyo mzuri au kwenye mashamba ya wananchi na
kusababisha uharibifu wa mazao na kuwindwa na wahalifu, mfano wa wanyama
hao ni tembo.
Kuna athari nyingine ikiwemo vifo vya wanyama na
wadudu waishio kwenye maji, kwa mfano Banga anasema viboko wamekuwa
wakihama kutoka sehemu chini ya mto hadi upande wa juu ambako kuna maji
na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi kipindi chote cha kiangazi.
Wakati mwingine wanyama hawa hujazana kwenye bwawa moja ambalo lina maji
na hupigana hadi kusababisha vifo vyao.
Pia eneo la ardhi oevu ya Bonde la Usangu limekuwa likipungua mwaka hadi mwaka sanjari na eneo la Bwawa la Mtera.
Hali
hii inaweza kudhoofisha shughuli za utalii katika Hifadhi ya Taifa ya
Ruaha na maeneo jirani kwani Mto Ruaha Mkuu ni kivutio kikuu cha Hifadhi
ya Taifa ya Ruaha.
Sehemu kubwa ya mto imejaa mchanga na kuota mimea ambayo haikuwepo kabisa miaka ya nyuma.
Naye
Kaimu Meneja wa Mtera Mhandisi Stephen Mpufubutsa, anasema kupungua kwa
kiwango cha maji katika Bwawa la Mtera kumesababisha kupungua kwa
uzalishaji wa umeme kutoka megawati 80 hadi 40.
Mpufubusta
anafafanua kuwa tangu mwaka 2011 bwawa hilo lilianza kuonyesha dalili za
kukauka, matokeo yake kuleta athari hizo katika uzalishaji wa umeme.
Ofisa
Utalii wa TANAPA ofisi ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Risala Kabongo
anasema kutokana na kukosekana kwa maji, tembo wamekuwa wakihangaika na
kuharibu miti hasa ile inayokuwa na maji ili kuweza kutuliza kiu.
Nini kifanyike
Mkurugenzi
wa Idara ya Misitu na nyuki wa Wizara ya Maliasili na utalii, Dk.
Felician Kilahama anasema hali ya misitu ni mbaya kwani shughuli za
binadamu zinafanyika kwa kiwango kikubwa kwenye vyanzo vya maji.
“Ingekuwa
amri yangu nisingeruhusu maji ya Mto Ruaha mkuu kutumika kwa ajili ya
mashamba ya umwagiliaji kule Mbarali na kwingineko, badala yake
yangetumika baadaya kufanya shughuli zote ikiwemo uzalishaji wa umeme
Mtera na Kidatu”, anasem
Anasema ni vema shughuli za kilimo,
ufugaji na uvuvi zifanyike baada ya maji kutoka Bwawa la Kidatu kama
inavyotumika kwenye mashamba ya miwa.
Kwa upande wake hifadhi imeanzisha mpango wa kutoa
Mwananchi
No comments:
Post a Comment