ANGALIA LIVE NEWS

Monday, February 10, 2014

Taswira ya Tanzania yachafuka nchini Uingereza kwa ujangili

Kwa jumla Tanzania inatawaliwa na chama kimoja ikiwa chini ya chombo kimoja cha intelijensia, hakuna mtu anayepinga kuwa hayo yanafanyika bila kuhusisha ngazi za juu. Lakini hakuna hata kigogo mmoja aliyekamatwa na kushtakiwa.” Inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Dar es Salaam. Wakati Rais Jakaya Kikwete akijiandaa kwenda London Uingereza kuhudhuria mkutano wa kuokoa viumbe vilivyo hatarini kutoweka duniani ukianza wiki hii, tatizo la ujangili limeweka wingu zito kwa Tanzania.
Rais Kikwete ni kati ya viongozi wa nchi 50 watakaohudhuria mkutano huo, utakaokuwa chini ya wenyeji wa mwana wa Wales na Waziri wa Mkuu wa Uinegerza, David Cameron,
Taarifa ya gazeti la The Mail on Sunday la Uingereza la Februari 8, limeitaja Tanzania kama kinara wa ujangili kwa kuua zaidi ya tembo 11,000 kwa mwaka, huku Rais wake (Jakaya Kikwete) akielezwa kufumbia macho.
Pia, gazeti hilo limemhusisha Rais Kikwete kuwa na urafiki na wafanyabiashara ya meno ya tembo, huku likiwahusisha wafadhili wa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika biashara hiyo.
“Utawala wa Rais Kikwete umetawaliwa na mauaji ya tembo yaliyovunja rekodi katika historia ya nchi yake. Kibaya zaidi, wahifadhi wanasisitiza kuwa, ndani ya Serikali kuna viongozi wanaoshiriki biashara hiyo,” imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Katika mkutano huo, viongozi wa nchi 50 na mawaziri wataweka mikakati dhidi ya biashara haramu ya wanyamapori, yenye thamani ya pauni 6 bilioni za Uingereza kwa mwaka zinazotumika kufadhili magaidi.
Taarifa hiyo inasema kuna wafanyabiashara wakubwa wa Dar es Salaam wanaohusika na ujangili.
“Miongoni mwao ni  matajiri wakubwa nchini, wafadhili na wanachama wa CCM na ndugu wa karibu wa Rais Kikwete. Lakini wanao marafiki wakubwa, huku majaji, waendesha mashtaka na polisi hurubuniwa kwa urahisi,” inasema sehemu ya taarifa hiyo.
Pia, taarifa hiyo inadai kuwapo kwa idadi kubwa ya Wachina wanaofanya biashara ya mafuta nchini, huku baadhi yao wakihusika na ujangili.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salva Rweyemamu alikiri kuona taarifa hiyo na kwamba, Rais Kikwete atahudhuria lakini aliipuuza taarifa hiyo.
“Ni kweli Rais Kikwete atahudhuria huo mkutano, lakini taarifa ni ya None sense, crap and malicious (ya kishenzi, kipuuzi na ovu),” alisema Rweyemamu.
Juhudi za kumpata Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu hazikufanikiwa baada ya simu yake kuita  muda mrefu bila kupokelewa.
Hata Naibu wake, Mahmoud Mgimwa naye hakupokea simu alipopigiwa.
Kuhusu CCM taarifa hiyo imeitaja idara ya wanyapori kunuka rushwa huku ikisingizia kuuzwa kwa meno ya tembo yaliyoko ghalani kwenye soko la kimataifa wakati lengo lao ni kupata fedha kuisaidia chama hicho  uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
“ Wabunge, maofisa wa juu na wafanyabiashara, wametajwa bungeni na kwenye vyombo vya habari, lakini uchunguzi unapotezwa,” inaongeza.
Jitihada za kupata viongozi wa CCM hazikuzaa matunda.
Mwananchi

4 comments:

Anonymous said...

JAMANI SASA TUUNGANE ILI KUTOKOMEZA UROHO HUU USIOPENDA VIZAZI VIJAVYO VIFAIDI URITHI HUU TULIOUPATA TOKA KWA WALIOTUTANGULIA.DAWA NI TUWAHAMASISHE WATANZANIA WOTE KUSEMA UKWELI KWA KUWATAJA WAZI WAZI WALE WOTE WANAOHUSIKA NA BIASHARA HII HARAM HUKU TUKIWA KIMYA.PAWEPO NA UHAMASISHAJI WA WATU KUTOA TAARIFA KWA SIRI MAHALA POPOTE TANZANIA ILI KULINDA USALAMA WA MTOAJI WA TAARIFA.NINAIMANI HILI LITAFANIKIWA SANA KAMA HAMASA ITAFANYIKA SAWASAWA KWA DHATI,HAMASA.KWANI HAWAFANYI PEKE YAO,LAZIMA WANA KIKUNDI,NDUDGU,MARAFIKI ZAO AMBAO WANAWAJUA USHIRIKI WAO KATAKA UJANGILI.TUWE WAZALENDO WA KWELI WAPENDA NCHI YETU,NA WATANZANIA WOTE!TULIYO TAYARI KUFA KWA AJILI YA NCHI YETU,HILI TUTALISHINDA.HAO SI MAADUI WA TEMBO TU,BALI NI WAASI WA NCHI YETU.HAWAIPENDI NCHI YETU,WANAPENDA MALI ZA NCHI YETU!na wanaowasAIDIA NI WASALITI NAMBA MOJA WA WATANZANIA.TUAMKE,TUSHIRIKIANE,TUWAUMBUE NA IKIBIDI KUWEPO NA MAHAKAMA FOR THEM ILI KUHARAKISHA HUKUMU ZAO. THEY SHOULD PAY THE PRICE ONCE FOUND MAJANGILI

Anonymous said...

The best way to discipline Tanzanian government is to expose this kind of evil to westerners who donate money to Tanzania in regular basis. Once financial donation shrinks, the government will act.

Anonymous said...

MDAU UMESHA AMBIWA NI CCM NA KILA MTU ANAJUWA NI VIGOGO WA CCM KUNA HAJA YA KUFANYA UPELELEZI? Una dhani serikali ya UK haijui kina nani? Au kwanini rais anafumbia macho? Basi na yeye anahusika na marafiki zake. Wanajurikana sana hizi nchi za madola Mimi sizielewi sometimes unadhani hawajui jinsi vile raia wa Tanzania wanateswa vichura chura na kupigwa na kuhuwawa? Wanayajuwa yote hayo lakini wanaiachia CCM ipete hii ni geresha toto politics ni mchezo machafu na wa dhambi tupu. Utamwona JK anarudi bongo meno yote yakiwa nje. Sijui uwa wanahongwa hawa viongozi wa nchi za ma$$$$$. Mimi siwaelewi kwakweli wanaudhi mana wameiachia CCM kupita kiasi this is too way much!.

Anonymous said...

wadau asanteni sana, Kusema ukeli wala tusitafute mchawi wa hali ya inayoendelea Tanzania, wahusika wakuu ni viongozi wa serikali ikishika mkondo CCM, na ufisadi. Hivi naomba tujiulize madawa ya kulevya yamepigiwa debe sana na wakakamatwa wengi tu! Wako wapi waliokamatwa na waliposemwa wakubwa wanahusika kuna hatua yeyote ilichukuliwa si tumeona kimya mambo yanaendelea kufanyika tu nani aliyechukuliw ahatua hadi leo hii na biashara inazidi kushamiri, Haya yasemwayo ni kweli tupu hata viongozi wenyewe wanalindani ile mbaya iko siku tu mawe yatashushwa vichwani!!