Joy Kalemera (wapili toka kulia) akiwa College Park Maryland alipowatembelea darasa la kiswahili DMV siku ya Jumamosi Feb 8, 2014. Wengine katika picha ni waratibu wa Miss Tanzania USA akiwemo mkurugenzi Ma Winny Casey (wa kwanza kushoto)
Wanafunzi wa darasa la kiswahili DMV wakimsalimia Miss Tanzania USA Pageant na kumwimbia nyimbo mbalimbali za kiswahili ukiwemo wimbo wa Taifa.
Miss Tanzania USA Pageant akijitambulisha na kuwaambia yeye ni mhandisi anayefanyakazi New Jersey na akawauliza kama wanafahamu maana ya neno uhandisi na wao wakajibu hawafahamu ndipo alipowaelewesha maana yake kwa Kingereza.
Wanafunzi wa darasa la kiswahili wakimsikiliza Miss Tanzania USA Pageant alipowatembelea shuleni kwao College Park, Maryland.
Mwalimu mpya wa hesabati Cechelela Timo akiwafundisha hesabu kwa kiswahili wanafuzi wa darasa la kiswali DMV.
Mwalimu Asha Nyang'anyi akiwaelekeza jambo wanafunzi wa darasa la kiswahili DMV.
Mmoja ya wanafunzi Briana akiwasomea kitabu cha hadithi wanafunzi wenzake.
Miss Tanzania USA Pageant Joy Kalemera akimuelekeza kitu mmoja ya wanafunzi wa darasa la kiswahili DMV
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
3 comments:
Nawapongeza walioanzisha Darasa la kiswahili,wenzetu waspanishi watoto wao wanaongea kispanishi kama vile wamezaliwa huko kwao......waanzishe mfuko wakuwakwamua,kuliendeleza.
Bwana Joel waspanishi wenzetu wanawasemesha watoto wao kispanish kila mahali nyumbani wapi sisi watanzania hatuwasemeshi watoto wetu kiswahili tunafanya kosa kubwa sana mtoto akikulia Marekani hata ukimsemesha kiswahili nyumbani saa yote lazima ataongea kingereza kizuri tu akienda shule tunakua na uoga huo kwamba tukimsemesha kiswahili atakua hajui kingereza sio kweli wasemesheni watoto wenu kiswahili muwaache walimu na majirani waseme nao kingereza.
Anonymous wa pili umenikweza na huu ni mtihani mkubwa maana hata hawa watoto wakifundishwa Kiswahili na wakirudi nyumbani wazazi mnawaongelesha kiingereza its waste of time kwa hawa walimu wanaojitolea. Wazazi muendeleze Kiswahili nyumbani 24/7! Kiingereza kiacheni penda wasipende watakijua tuu mbona sisi tuliokulia Bongo ung'ee unapanda???? na nyumbani hakuna aliyekuwa anazungumza ung'ee????
Post a Comment