ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 24, 2014

SIKU YA 17 KUPOTEA NDEGE YA MALAYSIA: NDEGE YA MALAYSIA ILIRUKA CHINI YA FUTI 12,000

Naibu Waziri Mkuu wa Australia Warren Truss akizungumza na waandishi wa habari juu ya maendeleo ya utafutwaji wa ndege iliyopotea.
NDEGE ya abiria ya Malaysia iliyopotea kiutatanishi wiki mbili zilizopita, inadaiwa iliruka chini ya futi 12,000 kutoka usawa wa bahari kutokana na matatizo katika chumba cha rubani kabla ya kupotea katika rada, ripoti mpya zimeeleza.
Wakati ndege hiyo Boeing 777-200 ikiwa bado inatafutwa katika bahari ya Hindi, habari zinasema chombo hicho kilibadili uelekeo ikiwa juu ya bahari ya Kusini ya China.
Mara ya mwisho ndege hiyo ilionekana katika rada ya jeshi la Malaysia saa 2.15 asubuhi kwa saa za nchi hiyo, Machi 7 mwaka huu, ikiwa katika kisiwa cha Penang kilicho kusini mashariki mwa taifa hilo, muda kama saa moja baada ya kuwa imeruka kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing nchini China.

Mapitio ya Rada yalionyesha ndege hiyo ikibadili mwelekeo baada ya kugeuka ghafla na kwa kasi upande wake wa kushoto kuelekea Malacca.

Ofisa mmoja aliyekataa kutajwa jina kwa vile siyo msemaji, aliiambia CNN kwamba kuruka chini ya futi 12,000 katika anga yenye ndege nyingi kama ilipokuwa ikipita kungeifanya ndege hiyo kutoonekana na ndege zingine.

CHANZO: DAILYMAILY

No comments: