ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 22, 2014

Ashambuliwa kwa kuvaa kimini

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita,Joseph Konyo.
Askari wa jadi maarufu kama sungusungu wa mtaa wa Mwatulole kata ya Kalangalala mjini hapa wanadaiwa kumdhalilisha na kumfanya ukatili mwanamke mmoja kwa kumkamata na kumcharaza viboko kwa tuhuma za kuvaa nguo fupi (kimini).

Inadaiwa kuwa walichukua uamuzi huo baada ya kamanda wao kuwaamuru na kutangaza sheria binafsi ya kuzuia watu kuvaa vimini kwenye mtaa huo.

Akizungumzia kwa masitikiko mwanamke huyo, Jennifa Nobo (24) alidai kuwa alishambuliwa na sungusungu hao Aprili 15, mwaka huuu katika mtaa huo wakati amekwenda sokoni.

Jeniffa alisema kuwa alipokwenda sokoni hapo kununua mahitaji ya nyumbani kwake, alikutana na sungusungu hao wakiwa wameongoza na kamanda wao huyo, Daud Kulola.

Alidai baada ya kukutana nao, walimkamata, kumpapasa maungoni wa kumhoji sababu za kuvaa kimini ndani na juu khanga wakati kiongozi wao amepiga marufuku kuvaa mavazi hayo katika mtaa huo.


Jeniffer alidai bila kusikilizwa utetezi wake, sungusungu hao walianza kumcharaza viboko hadharani na kumfuata kila alikokuwa akimbilia.

Alidai wakati wakicharaza viboko walimbakiza na kimini hicho Aliendendelea kudai kuwa kamanda huyo alipochoka kumuadhibu, alimrejeshea khanga yake.

''Nlilipita kila kona akanifuata na kunicharaza kwa fimbo nililia saba na kutokwa na haja ndogo kwa hofu na kipigo ..kilikuwa kitendo cha kinyama ambacho sijawahi kutendewa katika maisha yanguna, sitakisahau, ''alidai..

Baadhi ya wakazi wa mtaa huo walidai kuwa siku moja kabla ya tukio hilo la ukatili, Kamanda huyo alisikiska akitumia kipaza sauti akitangaza kuwa vijana na wasichana wote wake kwa waume wanaovaa vimini ni marufuku kuonekana mtaani.

Walidai wengi wao walidhani huenda lilikuwa ni agizo la Serikali.

Baada ya tukio hilo Jeniffa alikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi cha Geita kufunguliwa jalada GE/RB/2033/ 2014 la shambulio la kudhuru mwili kisha kupatia PF3 kwa ajili ya kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Geita.

na kukakamatwa hata hivyo alipewa dhamana wakati polisi wakiendelea na uchunguzi wao.

Alisema baadaye polisi walimkamata kamanda huyo wa sungusungu na kuachiwa kwa dhamana na kwamba uchunguzi dhidi yake unaendelea.

Kamanda huyo alikataa kuzungumzia madai hayo dhidi yake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa huo, Kalori Malicery amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kukataa kuzungumzia kwa undani kwa madai limeripotiwa polisi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Joseph Konyo alionyesha kusikitishwa na tukio hilo na kuahidi kuzungumzia leo ofisini kwake.

Konyo alisema kuwa iwapo ushahidi utathibitika mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani.
                   
CHANZO: NIPASHE

2 comments:

Anonymous said...

Sawa kabisa, enzi za miaka hiyo hata nyerere aliamrisha askari kutembea na mikasi na kuwasaidia wanawake wanaotembea nusu uchi kwa kumalizia kuzichana hizo nguo fupi. Ni bora kupigwa viboko kuliko kubakwa wamemsaidia. Nimekaa ughaibuni miaka takriban 25 NA SIJAWAHI VAA HIVYO VIMINI NA UMBO NINALO! Lets value our culture na miili yetu. Inabidi Steve Harvey afanye kazi ya ziada.

Anonymous said...

Wewe unayedai umekaa nje inaonekana uwezo wako wa kufikiri upo mdogo sana. Kaa huvai mini na umbo unalo kama unavyosema hilo ni tatizo lako. Huwezi kuingilia uhuru wa watu kuvaa watakavyo kwa sababu ya dini yako au culture yako....si kila mtu anatukuza culture yako, sasa kupiga kumesaidiaje? Na kama ni halali imekuwaje hao wapelekwe polisi? Inaonekana hujastaarabika hata kidogo! Nje umekaa nchi gani ambayo ukivaa mini skirt unashambuliwa? Saudi arabia au Iran? Usilete matatizo yako kwenye nchi yetu kwa sababu zako za dini yako?