Chama cha Mapinduzi Tawi la California kinapenda kupongeza na kutambua juhudi zifanywazo na serikali chini ya chama tawala cha CCM katika masuala muhimu yahusuyo maslahi ya wanachi wake.
Kwanza: Tunapenda kumpogeza Rais wetu, Mh Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM, kwa kuendelea kutuelimisha na kutushauri na kutupa moyo juu ya suala zima la Uraia pacha. Rai hiyo aliyoitoa wakati akiongea na watanzania waishio Uingereza juma lililopita imetupa moyo na mwamko kwamba hatujatupwa na maoni yetu bado ya nafasi ya kusikilizwa na kujadiliwa bungeni. Lakini zaidi tunapenda kumpogeza hasa kwa kuonyesha kuwa serikali ya CCM, bado imeliongelea hilo suala la uraia pacha na kuliwezesha liingie kwenye mjadala wa katiba mpya ili lifikiriwe. Tunapenda kuipongeza Serikali ya CCM,chini Mwenyekiti wetu kwa kulitambua hilo, na sasa kazi imebaki ni ya kwetu kufanya yaliyobakia ili tusikike na tusikilizwe na mwishowe hoja zetu zikubaliwe huko bungeni.
Pili: Tunapenda kutoa pongeza za dhati, kwa Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Taifa Mh Abdulrahman Kinana, kwa ukweli kwamba anafanya kazi kwa kasi, kwa kujituma na kwa viwango. Ziara za mikoani zimekuwa zenye mafanikio makubwa kwa chama na serikali yetu, na hasa kurekebisha yale yanayohitaji marekebisho na pia kuongeza bidii kwa yale yanayosuasua na kuwasilikiza wananchi mpaka wa vijijini ndani ambapo wengine hawajahi hata kutembelewa na viongozi wa hivyo.
Tumefurahishwa na tunapongeza juhudi zake za hivi karibuni wakati akiwa katika ziara kijijini Mawenzusi, wilayani Sumbawanga, Mkoani Rukwa na kusimamia kwa umakini mgogoro wa ardhi uliokuwa ukifukuta kwa muda mrefu baada ya wakazi wa maeneo hayo kulalamika kwa muda mrefu kupokonywa ardhi yao na kupewa na mwekezaji ambaye badala ya kuendeleza hiyo amefanya vioja tu.
Mheshimiwa Kinana tunampongeza kwa kusimama pamoja na wanakijiji ambao waliona hapo ndio kimbilio lao, na bila kusita mheshimiwa Kinana alifanya maamuzi ya busara yaliyoendana na maamuzi yaliyokuwa yameishatolewa na mheshimwa rais kwamba wananchi wale wafikiriwe na warudushiwe baadhi ya sehemu ya ardhi lakini maamuzi hayo hayakutekelezwa na wahusika. Mhehimiwa Kinana ameyatekeleza na wananchi watafaidika na ardhi yako na taratibu zitafuatwa.
Ni hayo mambo muhimu yametufanya tupongeze juhudi za viongozi, kuomba wananchi wote tuungane kushirikiana nao kwa nguvu katika kulijenga Taifa letu.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI-( Tuendelee kukiunga chama kutetea muundo wa serikali mbili)
KATIBU WA CCM-TAWI LA CALIFORNIA
ERICK BYORWANGO
2 comments:
ASANTENI, ndg zanguni wanaCCM tunatakiwa kuangalia mbele zaidi na sio kutoa sifa za matembezi ya mikoani tu hivi jamani tunajua jinsi gani ndugu zetu na watoto wanapata shida kule nyumbani bado serikali iliyoko madarakani inatakiw kufanya kazi ya ziada tunapowashabikia namna hii basi tunazidi kuharibu bora basi tuunde jumuiya ya waTZ na pia michango ya kusaidia kule nyumbani. Tusidhani maisha tuliyo nayo hapa ndo yale yaliyoko nyumbani kw akuishabikia CCM Ndugu zanguni. Kwanza sisi sio wapiga kura hata kidogo hilo lieleweke, tuyaone na makosa pia sio kusifia tu. Mimi ni mwana CCM wa tangu enzi lakini lazima tuwe wakweli. Nukuu "MPINZANI WA KWELI ATATOKA HUMU HUMU CCM" Baba wa Taifa letu MWL.. JK NYERER../
Je, haya ni ya kweli au ni kujifurahisha zidi ya ukweli. Ukweli utakuweka huru daima...
Post a Comment