Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Japan katika Umoja wa Mataifa, Balozi, Kazuyoshi Umemoto akizungumza machache wakati wa ufunguzi wa semina hiyo ya siku moja
Washiriki wa kutoka Balozi mbalimbali, Umoja wa Mataifa na Asasi zisizo za kiserikali wakifuatilia hotuba za ufunguzi wa semina hiyo waliokaa mstari wa mbele ni watoa mada akiwamo Bw. Dmitry Titov wa kwanza kulia ambaye ni Katibu Mkuu Msaidizi anayehusika na masuala ya utawa wa sheria katika Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja wa Mataifa ( DPKO)
4. Balozi Igor Vencel, Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Slovakia naye akisema machache wakati wa ufunguzi wa semina hiyo.
Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kuhusu ujumuishwaji katika mchakato wa uboreshaji wa taasisi za usalama (SSR), semina hiyo ya siku moja ilifanyika siku ya jumanne katika Uwakilishi wa Kudumu wa Japan katika Umoja wa Mataifa na iliandaliwa kwa ubia kati ya Japan, Tanzania na Slovakia
Balozi Igor Vencel, Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Slovakia naye akisema machache wakati wa ufunguzi wa semina hiyo
Sehemu ya Washiriki wakifuatilia semina hiyo ambayo iliambatana na kipindi cha majadiliano na maswali na majibu.
Na Mwandishi Maalum
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
imeihakikishia Jumuiya ya
Kimataifa kwamba itaendelea kushirikiana na
Umoja wa Mataifa na Jumuiya
za Kikanda katika jitihada za
urejeshwaji na uimarishaji wa mazingira ya amani na usalama katika nchi
zenye migogoro.
Kauli hiyo imetolewa na Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi, Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, wakati wa
ufunguzi wa semina ya siku moja iliyoandaliwa kwa ushirikiano kati ya Balozi za Japan, Tanzania na
Slovakia.
Mada kuu ya semina hiyo
iliyofanyika siku ya jumanne
katika Ubalozi wa Japani hapa
Umoja wa Mataifa, na kuhudhuriwa na
wawakilshi kutoka Balozi
mbalimbali, watendaji kutoka Umoja wa Mataifa, Mashirika yasiyo ya kiserikali
na wadau wengine , ilihusu Ujumuishwaji katika Ujenzi wa Nchi, Inclusivity in Building States: mkazo ukiwa katika ujumuishwaji
katika mchakato wa maboresho ya
taasisi za usalama. Inclusivity in secjurity sector reform ( SSR)
katika ufunguzi huo
Balozi Mwinyi aliwaeleza washiriki wa semini hiyo kwamba, wakati Tanzania ikiihakikishia Jumuiya hiyo ya Kimataifa na hususani Umoja
wa Mataifa, wa kuendelea kushirikina
nayo katika ujenzi huo wa amani, bado
inaamini na ingependa kusisitiza kwamba
serikali husika ndiyo inayopaswa kuwa mmiliki na muhusika mkuu wa
mchakato mzima wa uboreshwaji wa taasisi
za usalama .
“ pamoja na mambo
mengine, ningependa kusisisitza umuhimu
wa dhana kuu ya msingi inayosimamia mchakato mzima wa maboresho ya taasisi
za usalama, na dhana hii ni umiliki wa nchi husika katika utekelezaji wa mchakato huu” akasisitiza
Balozi Mwinyi
Na kuongeza , pamoja na kwamba, serikali husika ndiyo
mwenye dhamana na mmiliki wa mchakato
mzima wa SSR, itakuwa ni jambo jema kama
wadau wengine nje ya serikali husika wakashirikishwa au wakajumuishwa
katika majadiliano ya utafutaji wa
amani pamoja na mchango wa uboreshwaji wa sekta za usalama
kwa madhumuni ya kuhakikisha kwamba wadau wote wanakuwa katika muelekeo mmoja
ili kuepusha migongano.
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Tanzania kushirikiana na Japani
katika uaandaji na uendeshaji wa semina za aina hii kabla ya kuungana na Slovakia.
Pamona na Naibu Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kushirikia
katika ufunguzi wa semina hii, Manaibu wawakilishi wa Japani, Balozi Kazuyoshi Umemoto na Balozi Igor Vencel Slovakia nao
walizungumza.
Aidha Bw. Dmitry Titov,katibu Mkuu Msaidizi anayehusika na Masuala ya Utawala wa
Sheria katika Idara ya Operesheni za Ulinzi wa Amani katika Umoja
wa Mataifa Bw. Dmitry Titov.
No comments:
Post a Comment