Ni
magazeti kadhaa ya leo Tanzania ambayo yameripoti kuhusu kukamatwa kwa
gari la Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe huko Mombasa Kenya.
Jambo leo wameripoti kwamba gari la Mbowe lililokamatwa ni lile la
kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni ambapo limekamatwa kwenye msako wa
magaidi na uhalifu nchini humo na Polisi wanamsubiri Mbowe na Wenje kwa
mahojiano.
Gazeti
la habari leo limeandika kwamba gari la Mbowe lashikiliwa Mombasa,
namba mbili za STK na KUB zatisha Polisi Kenya na dereva ahojiwa
akihisiwa kuhusika na ugaidi.
Uhuru wameandika shangingi la Mbowe lakamatwa Kenya, alikwenda huko na Ezekia Wenje, dereva wake ahojiwa.
1 comment:
ccm balaa wanasuka kila mbinu na mipango kuwachafua wanasiasa wapinzani sasa hii story kweli inaingia akilini kama si njama za ccm na kenya mjuee kikwete ndo kwao ana biashara zake huko
Post a Comment