Waziri
wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Magufuli (katikati) na Mwenyekiti wa Kamati ya
Miundombinu Mhe. Peter Serukamba (kulia) pamoja na Naibu Waziri wa
Wizara ya Ujenzi Mhe. Eng. Gerson Lwenge (kushoto) wakiwa katika kikao
cha kujadili bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2014/15.
Kamati
ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mapema wiki
hii ilikutana na Watendaji wa Wizara ya Ujenzi kwa ajili ya kupitia
maepndekezo ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2014/15.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli awali kabla ya
kuwasilisha mapendekezo hayo kwanza alianza kwa kutoa tarifa ya
utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2013/14 ambapo Wizara ya Ujenzi
ilitengewa Shilingi 381,205,760,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.
Hadi kufikia mwezi Aprili 2014 jumla ya Shilingi 372,088,829,186.73
zilikuwa tayari zimetolewa na HAZINA. Kiasi hicho ni sawa na asilimia
97.61 ya kiasi kilichokuwa kimepangwa.
Akizungumzia
fedha za Mfuko wa Barabara (Road Fund), Waziri wa Ujenzi alibainisha
kuwa katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 Mfuko huo ulipangiwa kukusanya
Shilingi 504,306,000,000 kwa ajili ya Wizara ya Ujenzi, TANROADS na
TAMISEMI. Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014 fedha zote zilizokusanywa
zilikuwa zimefikia Shilingi bilioni 496.220 sawa na asilimia 98.4 ya
malengo ya mwaka huu wa 2013/14.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Alhaj Mussa Iyombe (wa pili kushoto)
akiwa na Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo Eng. Joseph Nymhanga (wa pili
kushoto) wakiwa katika kikao cha kujadili bajeti ya wizara hiyo kwa
mwaka 2014/15.
Waziri
wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. Magufuli akiwasilisha mapendekezo ya bajeti
kwa mwaka ujao wa 2014/15 alifafanua kuwa ili Wizara ya Ujenzi ili
iweze kutekeleza majukumu na malengo yake itahitaji kiasi cha Shilingi
trilioni moja, bilioni mia mbili kumi na tisa, milioni mia saba kumi na
saba, mia tano tisini na mbili elfu (1,219,717,592,000.00). Fedha hizo
zimeelezewa kuwa ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida pamoja na miradi ya
maendeleo.
Kamati
hiyo ya Bunge baada ya kupitia vipengele vyote ilihitimisha kikao hicho
kwa kupitisha mapendekezo hayo ya Wizara ya Ujenzi ili yaweze
kuwasilishwa rasmi katika Mkutano unaoendelea wa Bunge la Bajeti.
Hata
hivyo katika hatua nyingine, Kamati hiyo iliitaka Wizara hiyo ya Ujenzi
kuhakikisha inasimamia ipasavyo sheria na taratibi zilizowekwa kwa
lengo la kulinda miundombinu mbali mbali inayosimamiwa na wizara hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati hiyo Mhe. Serukamba alisisitiza kuwa kuwepo kwa matuta
barabarani pamoja na kutosimamia ipasavyo udhibiti wa uzito wa magari
hasa makubwa katika barabara zetu huathiri kwa kiasi kikubwa miundombinu
hiyo.
Baadhi
ya Wabunge (mstari wa mbele) ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Miundombinu
wakiwa katika kikao cha kujadili bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka
2014/15.
Baadhi
ya Wabunge (mstari wa mbele) ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Miundombinu
wakiwa katika kikao cha kujadili bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka
2014/15.
Naibu
Waziri wa Ujenzi Mhe. Eng. Gerson Lwenge akifafanua jambo wakati wa
kikao cha Kamati ya Miundombinu kujadili bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa
mwaka 2014/15.
Picha
juu na chini ni Baadhi ya Wakurugenzi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za
Wizara ya Ujenzi wakiwa katika kikao cha kujadili bajeti ya wizara hiyo
kwa mwaka 2014/15.







Mheshimiwa Magufuli, endelea kutuondolea keo zinazoikabili Tanzania, na tunakuomba uingie kwenye kinyanganyiro cha Uraisi 2015 unatufaa waTanzania kukemea ufisadi.
ReplyDelete