Wednesday, May 7, 2014

PITA PITA YA VIJIMAMBO NA T.E.S NEW JERSEY

Pita pita ya Vijimambo katika kiwanda cha Gaiser New Jersey timu ya T.E.S ilivyoenda kurekebisha machine ya kusafisha hewa ya kiwanda cha kutengenezea sausage. Hapa unaweza kuona jinsi moshi ulivyokuwa unatoka hadi kusababisha kero kwa wakazi wa eneo hilo la kiwanda. T.E.S walivyofika walipiga mzigo na kuweka mambo shwari  kwa kufunga vifaa vyao.
Hapa ni technician wa T.E.S Nyagaly Ebra! akifunga computer maalum ilikumaliza tatizo hilo la moshi mchafu 
Dr Temba Engineer wa T.E.S akirekebisha mambo
Hapa ni baada ya kufungwa vifaa maalum vya T.E.S na sasa unaweza kuona hakuna moshi tena.
Machine imesha malizika na sasa company inaweza kufanya kazi bila kusababisha moshi tena.
T.E.S ni company inayo simamiwa na Dr Temba ambae ndiyo Engineer wa vifaa hivyo maalum vya kusafisha hali ya hewa sehemu za viwanda. Vifaa hivyo vinaweza kufungwa hata Tanzania katika viwanda vinavyo toa moshi na kusababisha kero kwa wananchi.
 Nyama hii ikiwa inachomwa na machine hizo ndiyo usabisha moshi.
 Hapa ni workshop ya T.E.S wakidesign machine mpya na ya kisasa itakayotumia umeme mdogo na pia uwezo wa kutumia gas kwa sehemu ambazo hazina umeme.


2 comments:

  1. SASA MR TEMABE UNATOA AJIRA HEBU TUAJIRI BASI WATANZANIA WENZAKO UMEMUAJIRI IBRA TUU

    ReplyDelete
  2. Hongera sana Dr. Temba kwa kazi nzuri na kuweza kuajiri watanzania. Unastahili recognition kwa kazi yako daktari!!!
    Vijimambo hayo ndiyo mambo ambayo tunataka tuyaone katika blog hii. Nawapongeza kwa kutuletea habari hii.

    ReplyDelete

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake