
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
MAMBO
yaiva!. Kamati ya uchaguzi ya Simba imepanga uchaguzi mkuu wa klabu
hiyo kufanyika juni 29 mwaka huu baada ya msajili wa vyama vya michezo
na klabu kuipitisha katiba yao iliyofanyiwa marekebisho.
Akizungumza
na waandishi wa habari makao makuu ya Simba yalipopo mtaa wa Msimbazi
Kariakoo, jijini Dar es salaam leo mchana, mwenyekiti wa kamati ya
uchaguzi ya Simba sc, mwanasheria na wakala wa wachezaji wa FIFA, Dkt.
Damas Ndumbaro amesema kamati yake imekutana jana na kuamua tarehe hiyo
ya uchaguzi ili kupata rais mpya, makamu wa rais na wajumbe wapya wa
kamati ya utendaji.
“Kamati yangu ina watu makini na wenye uadilifu mkubwa. Pia wana mawazo ya kuijenga klabu ya Simba”.
“Jana
tulikutana na kupanga ratiba ya uchaguzi. Hatutakuwa na huruma na watu
watakaoenda kinyume na kanuni za uchaguzi”. Alisema Ndumbaro.
Ndumbaro
alisema kuanzia mei 9 mwaka huu mchakato wa kuanza kutoa fomu kwa watu
wenye nia ya kuwania nafasi za uongozi utaanza rasmi, na siku ya
kurudisha fomu ni mei 14 mwaka huu.
![]() |
| Ismail Aden Rage safari yake yaelekea ukingoni Simba sc |
Mei 17 mwaka huu kamati ya uchaguzi itafanya zoezi la kuhakiki fomu za wagombea wa nafasi mbalimbali ndani ya klabu ya Simba.
Aidha,
Ndumbaro aliongeza kuwa mei 19 mwaka huu kamati yake itatangaza majina
ya wagombea na mei 20 watafungua milango ya pingamizi dhidi ya wagombea.
Mei 25 mwaka huu kamati ya uchaguzi itaanza kusikiliza pingamizi na mei 27 zoezi la usaili wa wagombe litaanza.
Mei 29 kamati ya uchaguzi ya Simba itatangaza matokoe ya usaili na mei 30 masuala ya maadili yataangaliwa.
Baada
ya zoezi hilo, Ndumbaro alisema juni 2-9 mwaka huu zoezi likalofanyika
ni kukata rufaa kamati ya rufaa na juni 10-12 rufaa zitasikilizwa.
Juni
16, 2014 zoezi litakuwa ni kukata rufaa kamati ya rufaa ya maadili, na
juni 16-20 maamuzi ya mwisho ya kamati ya rufaa na kamati ya rufaa ya
maadili yatafanywa.
Baada ya hapo juni 21 orodha ya mwisho ya wagombe itatangazwa na juni 24-28 kampeni za kunadi sera kwa wagombe zitaanza.
Juni 29 ni siku ya uchaguzi ambapo Simba itapata rais mpya atayerithi mikoba ya mpiganaji Ismail Aden Rage.
Hii
itakuwa siku muhimu sana kwa wana Simba wote na wanachama ndio wenye
mamlaka ya kuamua nani aiongoze klabu hiyo baada ya sinema nyingi
kuonekana katika uongozi wa Rage.
Rage
amekuwa akilaumiwa kwa muda mrefu na baadhi ya wanachama wa Simba kwa
madai kuwa ameshindwa kukidhi matarajio yao, lakini sasa safari yake iko
ukiongoni.
Kuna uhusiano mkubwa sana kati ya viongozi na timu kufanya vizuri uwanjani, bila shaka wanachama mtachagu viongozi wazuri.
Safar njema kwa Simba kuelekea katika uchaguzi wenu. Amani itawale kwa muda

No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake