ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 1, 2014

SHOGA, MFANYE MWENZI WAKO AKOSE CHA KUFANYA



NAJUA nikisema sana nitaonekana nina mdomo wakati kila kiumbe kinao, lakini kwa vile kuwapasha ndiyo hobi yangu acha niwachane laivu, simuogopi mtu. Kwa mtindo huu wanawake wachache watabakia katika ndoa zao.

Wanasema nachonga sana, sasa sijui nachonga stuli au meza, lakini mwisho wa siku utaikubali chungu niliyokunywesha ni dawa au
chungu uliyoikataa ndiyo imekufanya leo ulie kilio cha mbwa mdomo juu.

Wanawake hii ni nafasi yenu adimu kupata ulichokikosa kwenye mafunzo ya unyago au huyajui kabisa lakini hii ni home work ambayo unaweza kuifanyia kazi mwenyewe ukapata majibu.

Wanawake wengi wamekuwa wakipokonywa wanaume kutokana na kutojua au uvivu wao, lakini ndiyo hao wa kwanza kulalamika wanaibiwa waume zao.

Kwa vile mimi ni nyani mzee, nimekwepa mishale mingi hivyo nalijua pori vizuri. Pia ukubwa wa miti
yote na jinsi ya upandaji wake, huwezi kupanda mbuyu kama unapanda mnazi kila mti una upandaji wake, ipo mifupi lakini minene
hiyo nayo ina upandaji wake.

Leo hii nikikueleza unanikunjia mdomo kama pindo la jamvi bovu, shauri yako utaula huu na hasara juu.
Najua nimekuwa kama kimbunga na kujiuliza leo nani kaniudhi, umeniudhi wewe tabia yako kwa kweli sipendezwi nayo hata kidogo inakuwaje mtoto wa kike unakuwa na bustani nzuri lakini unaiacha na kuwa kama shamba la mpunga linalosubiri kuchomwa moto
magugu ili kujiandaa na kilimo kipya.

Najua macho yameshakutoka na kujiuliza nimekuwa na misemo mingi kama nimekatika ulimi, lakini yote ni kwa ajili ya kukujenga
wewe mwanamke mwenzangu.

Jamani hivi kwa nini wanawake tunajitukanisha? Hivi hatuna aibu hata chembe kusemwa na wanawake
wenzetu au kuchukuliwa waume zetu kutokana na udhaifu wetu?
Hivi kweli wewe mwanamke unamwacha mumeo hata kucha au kunyoa Ikulu mpaka nyumba ndogo? Halafu akirudi kanyolewa wala huna
habari! Aaah jamaniii, sipendi mie, hebu mtunze mumeo apendeze huyo anayetaka kukuibia akose kazi ya kufanya.

Siyo akidondokea nyumba ndogo utasikia jamani kweli mkeo hakupendi hata kucha huku chini nako kama kichaka cha vibaka kukabia
wapiti njia. Hebu basi tunapowafanyia usafi waume zetu si kufua tu, kila kitu, kumkata kucha, kumnyoa kila kona ya mwili.

Hebu jisikie fahari kusikia mumeo akisifiwa kutokana na malezi yako, wengine tunadiriki hata kuwaacha waume zetu hata bila ya
kujua asubuhi wanavaa nini na nguo aliyovaa inampendeza au vipi. Wengine hata hatujui waume zetu asubuhi wamevaa kufuli gani,
jioni anaweza kurudi na chupi mpya wala mshipa haukugongi unamsubiri kitandani.

Shuuutu, nani alikuambia kitanda kinabeba
nyumba bila matunzo, utaula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua.
Wengine wakiisha kuwa na msichana wa kazi basi kila kitu anamuachia afanye yeye kwa vile anamlipa mshahara, tunasahau mahaba
anayompa mumeo ya kumtengea maji, kumpikia chakula na pengine Mungu kamjalia umemlisha kapendeza basi mumeo akihamishia
mapenzi kwake huna nyumba mamaa! Utaishia kukimbilia kwa waganga umroge nani wakati mchawi ni wewe mwenyewe?

Jamani wanawake tuwajali waume zetu wengine hata hawajui kama mwili wa mume au mpenzi wake una kovu sehemu flani, wanakwenda
bora liende. Mmh! Dada ukiacha yupo mwizi atajichukulia kama vyake. Hebu mfanye mwizi wako akose cha kufanya ili kuidumisha
nyumba yako. Kwa haya machache yafanyie kazi utashangaa hii dawa ya mapenzi isiyotumia mizizi wala hiziri.
Ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu

GPL

5 comments:

Anonymous said...

basi kama kweli wewe mwanamke mwenzetu basi andika jina lako tukone isije ikawa ni mwanamme unajifagilia na kutafuta mwanywa wa kuwatukana wanawake hapa kama kweli mwanamke mwenzetu weke jina tukujuwe tuje tupate unyago wako na je umeolewa usiwe ukawa hujaolewa unakuja hapa kujifanya kugwii si semi kwamba wasio olewa hawawezi kuwa kungwii wako wengi walio jaliwa wanaweza kuwa kungwil lakini adaa inatakiwa uwe umeolewa so tupe hilo jinalako unapo weka makala yako hapa okaa mwanamkee mwenzetu kama kweli

Anonymous said...

makala hii nzuri sana lakin ninachostaajaabu hivi mwanamme hawezi kujikata makucha au kujinyowa ikulu mwenyewe mpaka mumewe huko kwao kalelewa vipi kuwa mchafu mchafu mpaka ampate mkee ndo anatarajia kutunzwa na kusafishwa..

aaah msaliye mtume mummy uliyeandika hii makala.
tena ni aibu na fedhea mwanamme asiyejua kujitunza mpaka amngojee mumee kalelewa vipi porini najua mamayee hawezi kumnyoa huko ikulu basi hata kuchwaa anashindwaaa aende saloon au hana pesa mfukoni

aaah tunapo longa longa tuangaliye na nyuma hii makala imewatusi sana wanaume na si wanawakeee mkaae mkijua.

Anonymous said...

KAMA RISKI NI YANGU HAWEZI AKACHUKULIWA NA KAMA MCHAFU ATAKUWA MCHAFU DAIMA ATASUBIRI SANA NIMKATE MAKUCHA NA KUMNYOA IKULUU KWANI YAYA WAKE MIMI ALIVYOKUWA ANANITONGOZA SI ALIKUWA ANAJUA KWENDA SALOON KUKATWA MAKUCHAA AU KUJIKATA MWENYEWE NA KUJIWEKA MTANASHATI ALIVYONIPATA MIMI MKEE TENA NIMEKUWA KIJAKAZI CHAKE CHA KUUUMKATA MAKUCHA ATASUBIRI SANA NA HAO WANAWEZA KUMKATA NA WAKAMKATE BWANA KILA MTU NA RISKI YAKE TUSITISHANE HAPA BUREE UKIWA NA CONFIDENCE AKICHUKULIWA NA WEWE UTAMPATA WAKO MWENYE KHEIRI NA WEWE WA KULISHANA ZABIBU UKO BI KUNGWII PASHKUNA WEWE

Anonymous said...

ni kweli mkee amtuze mume na mume amtunze mkee na chaa ajabu ukingoja au ukitarajia mwenzako akukuate makucha just think about it wewe ni mume wa aina gani mapenzi kufanyiana si katai lakini umekuwa mtoto mdogo kiasi hicho hujiwezi kujisafisha mimi nimekuwa mkee na mama yako pia wa kukulea come on
mambo ya kuzalilishana na kuwapa wanaume kichwa ndo haya na wanawake wasio na mbele wala nyuma na wasio na confidence ndo watafanya mambo haya na kuzalilishwa daima karne hii inginewe wanaume wanajua kujitunza siku hizi wana jipodoa na kujitia ma cream so wewe subiri kukatwa makuchaa na ya ote na utamfute bimashavu mwenzio

Anonymous said...

mwanamke aliye caree minded and educated hana nafasi hii na hatakama akimkosa mume yake yanamuendea wakatafutane wenyewe wa kupelekeaane maji ya hiliki na kukatwa makuchaa na kuibiwa nyimbo za taarab

ndo maana kila leo wanawake wenzangu wenye mtazamo huu mnazalilika.

na kwa taarifa yako nimefunzwa kwetu na nikafundishika sema sina time ya kukatana makucha nitafanya kwa nafasi yangu kama sina nampa nafasi jiran anisaidiye tule mzigo wote pamojaaaaaaaaaaaaaaaa

na niko radhi niliye kilio cha mbwaaaa kwa sabbau kuna siku nitanyamaza hichi kilio changu cha mbwa na kupata wangu anayejua kujikata makucha mwenyeweeeeeeeee

mpoo makugwii wanaume wa vijimambo