.jpg)
Jamal Malinzi,Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
Jamal Malinzi, Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), amesema wanatarajia kuendesha kampeni ya kusaka jina jipya itakalopewa timu ya taifa (Taifa Stars).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Malinzi alisema kampeni hiyo ambayo pia itahusisha utafutaji wa jezi mpya ya Stars, utahusisha nchi nzima kwa kupendekeza jana na rangi ya jezi kisha kupiga kura kupitia njia mbalimbali zikiwamo za ujumbe mfupi wa maandishi (SMS).
"Tumepata malalamiko mengi juu ya jezi mpya za Taifa Stars, lakini hatuna namna kwa sababu 2012 TFF iliingia makubaliano na Adidas kupitia mpango wa FIFA wa kuzisaidia nchi zilizo chini kisoka kupata vifaa vya michezo.
Ni mkataba wa mwaka mmoja, kwa hiyo tutaendelea kuzivaa hadi Desemba 31 mwaka huu," alisema Malinzi.
"Baada ya hapo tutasaka kampuni ya kutengeneza jezi za timu ya taifa lakini Watanzania ndiyo watakaopendekeza jezi na jina la timu ya taifa kupitia kampeni ambayo itafanyika nchi nzima.
Chipolopolo (timu ya taifa ya Zambia) maana yake ni risasi za shaba, Harambee Stars (timu ya taifa ya Kenya ina maana ya kampeni za kupigania uhuru, sisi Taifa Stars ina maana gani?" Alihoji Malinzi.

CHANZO: NIPASHE
2 comments:
Bongo bana kwa kuhangaika na vitu visivyo na manufaa wako juu sana, wanahangaika na jina badala ya kutafuta mbinu ili next world cup waende Qatar...mbona timu za ulaya na america kusini na kaskazini hazina majina???
Sasa naona siasa imeingia rasmi kwenye soka.je, kuna tatizo gani la jina la 'Taifa Stars'? With due respect, Malinzi unatakiwa kufocus kwenye maeneo yenye tija, na kwa soka hakuna lingine bali kutafuta mwarobaini wa kujenga timu bora, itakayo tuletea ushindi...period.
Post a Comment