Balozi Manongi na Upendo Manongi wakiwa na Padre Dkt. Peter Le Jacq wa Shirika la Maryknoll ambaye alianza kufanya kazi na Bugando Medical Center katika miaka ya 80 ambaye kwa kushirikiana kwa karibu na Marehemu Mhashamu Askofu Aloysius Balina walianza juhudi za kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya sekta ya afya hasa upungufu wa Madaktari. Padre Dkt. Jacq pamoja na rafiki zake alikuwa chumbuko la Kamati ya Touching Tanzania katika miaka hiyo ya 80 na hatimaye kuzaliwa kwa Touch Foundation mwaka 2004. Dkt. Jacq naye kwa upande wake amesifu na kutambua mchango wa Mhe. Rais Jakaya Kikwete na kujituma kwake kuimarisha sekta ya afya kwa kushirikiana na wadau wengine.
Rais wa Touch Foundation, Bw. Lowell Bryan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa na Mke wa Balozi, Bibi Upendo Manongi wakati wa Hafla ya Asante Supper 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki, hafla hiyo ilikuwa ni kuadhimisha miaka 10 ya Taasisi hiyo iliyokwenda sambamba na harambee ya kuchangia uimarishaji wa sekta ya Afya nchini Tanzania. Touch Foundation inafanya kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania na Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki cha Afya na Sayansi Mwambata ( CUHAS) Bugando Tanzania. Katika hafla hiyo, ambayo ilihudhuriwa na Viongozi wa CUHAS wakiongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu, Yuda Thaddaaeus Ruwa'ichi, Bw. Bryan alisifu na kupongeza utashi wa Kisiasa na Uongozi wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi , ushirikiano wake na kutambua kwake mchango wa sekta binafsi katika eneo hilo.
Makamu Mkuu wa CUHAS Professa Jacob Mtabaji kushoto kwa Balozi Manongi na Professa Paschalis Rugarabamu ambao walikuwa sehemu ya Ujumbe uliohudhuria Asante Supper 2014 wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.
Na Mwandishi Maalum
Touch Foundation ,
Taasisi isiyo ya kiserikali na yenye makao yake nchini Marekani, mwishoni mwa wiki ( Mei 8), imeadhimisha miaka kumi ya kazi zake na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali
ya Tanzania na Taasisi nyingine katika uboreshaji na uimarishaji
wa sekta ya afya nchi.
Katika hafla iliyojulikana kama Asante
Supper 2014, ilihusisha pia
utoaji wa tuzo kwa wadau mbalimbali ambao wamekuwa nguzo muhimu ya Taasisi hiyo. Asante Supper ilihusisha pia harambee ya
uchangishaji wa fedha kwaajili ya kusaidia sekta hiyo
ya afya. Hafla hiyo ilifanyika
katika ukumbi wa Morgan Library Museum,
Jijini New York.
Akiwakaribisha wageni waalikwa, Rais wa Touch Foundation, Lowell Bryan pamoja na kuelezea mafanikio ya taasisi yake
iliyoanzishwa mwaka 2004 katika uboreshaji wa sekta ya afya nchini Tanzania, amewataka wafadhili
mbalimbali kuendelea kujitolea na
kuchangia zaidi ili sekta ya afya nchini Tanzania iweze kuimarika
na hatimaye kumaliza au kupunguza changamoto
mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo.
Akasema utashi wa kisiasa na wa kiuongozi ambao Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha katika, si
tu kutambua na kuthamini mchango wa
Touch Foundation na Taasisi nyigine
kama hiyo, bali pia amekuwa mstari wa
mbele katika kuhakikisha kwamba sekta ya
afya inaimarika nchini Tanzania na
huduma za afya zinawafikia wananchi kule walipo.
Naye Padre Dkt. Peter le Jacq ambaye naye amekuwa na
mchango mkubwa wa uimarishaji wa sekta ya afya nchini kupitia Hopistali ya
Buganda ana ambaye haswa ni chimbuko
la Touch Foundation, hakusita kutoa shukrani zake kwa Rais Kikwete na kumuelezea kama kiongozi anayejituma, kujitolea na mwenye ushirikiano
mzuri za sekta binafsi.
Katika
Miaka kumi ya uhai wake Touch
Foundation imekuwa ikishirikiana na
kufanya kazi kwa Karibu na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, na
hususani Chuo Kikuu cha Kikatoliki
cha Afya na Sayansi Mwambata cha Bugando (CUHAS). Ushirikiano huo unahusisha katika maeneo mbalimbali mtambuka yakiwamo
mafunzo ya madaktari na wataalam wa fani
mbalimbali kupitia CUHAS na hivyo
kuchagia ongezeko la madaktari na
wataalam.
Mbali ya watendaji wakuu wa Touch Foundation, wakiongonzwa na Rais wake, Bw. Lowell Bryan, pamoja na wafadhili.Asante Supper 2014
ilihudhuriwa pia na wageni maalum
kutoka Tanzania na ujumbe huo
ulihusisha Muhashamu Thaddaeus Ruwa’ichi Askofu Mkuu
wa Mwanza na Mwakilishi wa Kudumu
wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,Balozi Tuvako Manongi alikuwa miongoni wa wageni waaalikwa.
Wengine kutoka
CUHAS walikuwa ni Askofu Augustine Shao, Makamu Mkuu wa CUHAS ,Profesa Jacob Mtabaji, Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Padre Dkt. Charles Kitima, Profesa Paschalis
Rugarabamu, Dkt, Isidor Nyahomela, Dkt. Frederick Kigadye, Dkt. Charles
Majinge, Dkt. Manage Manyama, Dkt. Stella Mongella, Dkt. Godwin, Godfrey Sharau na Sister Marie-
Jose Voeten kutoka hospitali Teule ya
Sengerema.
Baadhi ya
Madaktari hao kutoka Bugando na
hasa wale walionufaika na ufadhili wa
Touch Foundation walielezea walivyonufaika na
ufadhili huo ambao umewawezesha kusoma, kujipatia ujuzi na hivyo kupata
fursa ya kuwahudumia watanzania wenzao.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake