Sehemu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa, wakati wa majadiliano kuhusu dhana ya maendeleo ya pamoja, uwekezaji, biashara na misaada ya maendeleo, majadiliano hayo yaliongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Uhispania, Bw.Jose Manuel Garcia- Margallo Y Marfil ambapo pia alielezea nafasi ya nchi yake katika kukuza ushirikiano na misaada ya kimaendeleo
Na
Mwandishi Maalum
Tanzania
inaweza kuongeza zaidi kasi yake ya ukuaji wa uchumi na maendeleo ya wananchi wake, kwa kujifunza
uzoefu wa nchi nyingine marafiki
kama vile Uhispania.
Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, ameyasema hayo siku ya jumanne, wakati alipokuwa
akichangia majadiliano ya
mada kuhusu “Kuendelea kwa Pamoja: misaada ya maendeleo ( ODA), biashara na uwekezaji”.
Muwasilishaji
wa mada hiyo alikuwa ni Waziri wa Mambo
ya Nje na Ushirikiano wa Uhispania, Bw. Jose Manuel Garcia- Margallo Y Marfil,
alipokutana na kubadilishana mawazo na
Balozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa.
Balozi
Manongi amesema katika majadiliano hayo,
kwamba Tanzania kama
nchi inaaamini kuna maeneo ambayo
inaweza kujifunza zaidi na kutumia uzoefu wa Hispania katika kusukuma mbele kasi ya ukuaji wa uchumi wake na maendeleo.
Akabainisha kuwa maeneo ambayo Tanzania kwa
kushirikiana na Uhispania inaweza kujifunza na kubadilishana uzoefu
ni uwekezaji, biashara na uvutiaji wa misaada ya maendeleo.
“Tanzania
inapenda kukushukuru kwa kuadaa mkutano huu na fursa hii ya kubadilisha mawazo
kuhusu dhana nzima ya maendeleo ya
pamoja, misaada ya maendeleo,
biashara na uwekezaji”
Na kuongeza
“Maeneo haya ni muhimu sana kwetu na nina amini tunaweza kubadilisha
uzoefu na kujifunza namna ambavyo nyinyi
mumefanikiwa” akasema Balozi
Na kuongeza
kwamba hata katika majadiliano yanayoendelea hivi sasa
kuhusu ajenda mpya za maendeleo endelevu
baada ya 2015, maeneo yanayotiliwa
mkazo mkubwa pamoja na mambo mengine , ni hayo ya uwekezaji,
biashara na misaada ya maendeleo.
“ Ni kwa kutumia fursa zilizopo za uhusiano baina ya nchi na nchi na ushirikiano katika
ngani ya kimataifa, tunaweza
kuendelea kwa pamoja”. Akaongeza Balozi Manongi
Aidha Mwakilishi huyo wa Tanzania kama ilivyokuwa kwa wawakilishi wengine
waliochangia majadiliano yao, akatumia
fursa hiyo kuishukuru Uhispania, kwa
uamuzi wake wa kuanzisha Mfuko wa Maendeleo Endelevu kwa ubia na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa ( UNDP).
Akiwasilisha mada hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Uhispania, pamoja na mambo mengine, aliwaeleza mabalozi kwamba, nchi yake ambayo ilikumbwa na mtikisiko mkubwa wa kuyumba kwa
uchumi angalau imeanza kutengemaa kwa
kuchukua hatua kadhaa wa kadhaa, ingawa amekiri kwamba safari bado ni ndefu.
Baadhi ya
mambo ambayo anasema serikali yake iliamua kuyafanyia kazi kwa kuyapa umuhimu
ni pamoja na, kufungua milango ya
uwekezaji ndani na nje ya nchi
yake, kukuza na kupanua biashara
na upatikanaji wa ajira kwa vijana wao.
Akabainisha
kwamba kama si kupanua wigo wa
biashara, kuongeza kasi ya uwekezaji
ndani na nje, Uhispania isingeweza
kujifunia mafanikio iliyonayo hivi sasa
ikiwa ni pamoja na kuyatafsri mafanikio hayo
katika ushirikiano wa
kimaendeleo.
Na kwa sababu hiyo akasema nchi yake imekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa misaada ya maendeleo kwa nchi mbalimbali
yenye uhusiano nao ikiwa ni pamoja Umoja wa Mataifa.
Akatoa
mfano kwa kusema kati ya 2007 na 2012
nchi yake imechangia zaidi ya
dola za kimarekani 30 billion kwenye eneo la maendeleo, misaada ambayo
ilitolewa kupitia uhusiano baina yake na
nchi nyingine na katika ngazi ya kimataifa. Ambapo Afrika Kusingi mwa Jangwa la Sahara ilipata jumla ya dola 4 billioni kama msaada
wa maendeleo.
Kuhusu
uwekezaji akasema nchi yake inamtaji wa
dola bilioni 640. Vile vile Uhispania ni nchi ya saba kama msafirishaji wa
huduma katika nchi mbalimbali na ni ya 17 kama msafirishaji mkubwa
bidhaa.
Akasema ni
katika kuamini kwake katika dhana nzima
ya ushirikiano wa kimaendeleo ndio maana
nchi yake licha ya kutoa misaada
kwa nchi moja moja na katika ngazi ya Umoja wa Mataifa, ndiyo maana
imeamua kwa kushirikiana na UNDP kuunda mfuko wa maendeleo endelevu kama
ilivyofanya kwa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Millenia ( MDGs).
Akasisitiza
kwamba nchi yake imeamua kuunda mfuko
huo kwa kile inachoamini kwamba utakuwa
daraja au kiungo kati ya Malengo ya
Maendeleo ya Millenia ambayo yanaishia
ukiongoni, na malengo mapya ya maendeleo
endelevu.
No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake