Mkuu wa Wilaya ya Wete, Omar Khamis Othman
Biashara haramu ya ununuzi wa karafuu kwa njia ya kikombe na pishi imeshamiri katika ya maeneo ya shehia za Wilaya ya Wete ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakijihusisha na ununuzi wa karafuu hizo kinyume cha sheria .
Uchunguzi umebaini baadhi ya shehia ambazo biashara hiyo haramu inafanyika ni pamoja na Shehia ya Mtambwe Kaskazini, Bopwe na ya Ukunwi na masheha wa shehia hizo wamethibitisha.
Akizungumzia juu ya kuwapo na watu wanaonunua karafuu kwa njia ya kikombe, Sheha wa Shehia ya Ukunjwi, Mkongwe Kasanje Khamis, alisema kuwa ofisi yake imebaini kuwapo kwa vitendo hivyo na kwamba anafanya uchunguzi wa kina ili kuwaripoti kwenye vyombo vya sheria.
“Wapo watu hawana mkarafuu hata wa kukodi, lakini mtu huyo huyo unamkuta ana karafuu nyumbani kwake, najiuliza kazipata wapi, naamini hizi ni dalili za kuwapo biashara haramu ya kikombe, ” alisema Mkongwe.
Aidha, Sheha Mkongwe aliwataka wananchi kuwadhibiti watoto wao ili wasijiingize kwenye matendo ya wizi kwani wanaouza karafuu kwa njia ya kikombe zaidi ni watoto. Mkuu wa Wilaya ya Wete, Omar Khamis Othman, alisema Serikali imejipanga kupambana na watu wanaonunua karafuu kwa njia ya kikombe na pishi katika maeneo yote ya wilaya hiyo.
Alisema kwa kuanzia wataaza kuwasaka wanaonunua karafuu hizo na kuongeza kwamba kudhibitiwa kwa watu hao utakuwa ni mwarobaini wa kutibu maradhi ya wizi wa karafuu katika mashamba ya wakulima.
“Sisi tumejipanga kuwadhibiti wanaonunua karafuu kwani hawa ndiyo chanzo cha kuwapo na wizi wa karafuu ikizungatiwa watoto ndiyo wahusika wakuu wa kuuza karafuu kwa kikombe, ” alisema.
Othman alisema tayari Serikali imepokea taarifa kwamba wafanyabiashara wa karafuu kwa njia ya magendo wamesema kuwa watakula sahani moja na Serikali, hivyo kuwatahadharisha kuacha vitendo hivyo kwani Serikali haitakuwa na huruma na atakayekamatwa akiuza au kununua karafuu majumbani .
“Tumesikia kauli zao na sisi tumejipanga kupambana nao, cha msingi niwaombe wale wanaojihusisha na biashara hii waliachie Shirika la ZSTC linunue karafuu kwani ndilo lililopewa mamlaka na Serikali ya kununua karafuu,” alisisitiza.
Aliongezasema kuendelea kwa biashara hiyo kunasababisha watoto wengi kutoroka shule.

CHANZO: NIPASHE

No comments:
Post a Comment
bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake