ANGALIA LIVE NEWS

Friday, June 20, 2014

KUVAMIWA KWA AKAUNTI YANGU BINAFSI YA BARUA PEPE - SULEIMAN SALEH


     

   Leo hii Ijumaa Juni 20, 2014, kuanzia saa 5 mchana kwa saa za Marekani na saa 12 jioni kwa saa za Tanzania nimegundua kwamba akaunti yangu binafsi ya barua pepe kidundo2001@yahoo.com imevamiwa na wahalifu. 
Nimechukuwa hatua stahili na za haraka katika kushughulikia tatizo hili. Naomba kuwashukuru wote walionitanabahisha kwa kufahamu kwamba niko Washington DC, Marekani,  na wakashangazwa kupokea barua pepe nyingi ambazo zimedai kwamba niko Nassau, Bahamas, Manila Philippines, Rio de Janeiro, Brazil na Singapore na kwamba nimepata matatizo ya kuvamiwa na majambazi na kuibiwa kila kitu na hivyo kuomba msaada wa dharura.
   Naomba kuchukuwa fursa kutoa taarifa hii  kwamba mimi niko salama Washington DC, Marekani, na ninaendelea na shughuli zangu za kazi katika Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila ya matatizo yeyote. Pia naomba mtu yeyote atayepata email kwa anuani hiyo aipuuze, si ya kweli. Nitatoa tena taarifa mara nitapokuwa na anuani yangu halisi muda si mrefu ujao.
   Namshukuru Ankal Muhidin Issa Michuzi kwa kunitumia taarifa ya kwanza kuhusiana na uhalifu huu, na kunishauri kuchukua hatua haraka.

Suleiman Saleh
Washington DC

Juni 20, 2014

Bofya soma zaidi uone barua iliyotumwa


Hello,

I hope my mail get to you in good health? I'm contacting you as I need your urgent financial assistance. My family and I had a trip visiting to Manila, Philippines some days back for a short vacation. everything was going on fine until last night when we got attacked and robbed by some unknown gunmen on our way back to the hotel were we lodged. All cash, credit cards and cell phones were stolen away including some valuable items, leaving our passports and life's safe. The hotel management has been unhelpful for reasons I don't know, and won't let us leave until we settle the bills.

The Embassy and Police over here have failed to be effective in this matter, besides paper work would cost us days which we can't afford. We just have to pay for our return tickets and settle the hotel bills before we're allowed to leave. Please I need you to loan me some money so we don't miss our flight, as it leaves in next 12hrs from now. I promise to refund back the money as soon as we return home. I will appreciate whatever amount you can assist us with. Please let me know what you can do, I'm looking forward to hear from you.

Thanks and Regards,

Suleiman

1 comment:

Anonymous said...

Pole sana Brother Suleiman Mungu atazidi kukulinda wewe na familia yako. Amin