Kifo cha George Tyson ni pigo kubwa lingine kwa taifa na fani ya filamu, George Tyson ukweli ametuinua wengi katika fani ya filamu kwa kazi yake nzuri ya kama director na producer wa filamu, nami ni zao la kazi nzuri ya Tyson katika kazi za filamu, hapa itakumbukwa mwaka 1998 hadi 2000 kipindi cha mambo hayo kilichokuwa kikirushwa ITV kilikuwa moto sana nchi nzima ilipata kushuhudia tulivyokuwa tunacheza, mfano wakati Bishanga alipomleta Waridi kama mchumba wake kule kijini kwetu (chijijini iwee), hadi Bishanga anakataliwa na mchumba kanisani na kurudi kumuoa Waridi nk, hakika Tyson alikuwa anatuandaa vizuri sana kwa kiwango cha juu sana ! Nami niliweza kupata Award ya msanii ,muigizaji bora ilionipa zawadi ya kwenda South Africa kwa mafunzo ya filamu katika runinga, na hiyo ndio ilikuwa baraka iliopelekea kukutana na mume wangu mwaka 2001 na kujafunga ndoa yetu baada ya miaka kumi mwaka 2011. Hakika taifa na fani ilikuwa bado inamuhitaji sana na kumpenda sana, ila Mungu amempenda zaidi Tyson na kumchukua katika pumziko la amani la milele, Amen.
Kwa upande wa mtoto Nasra Rashid Mvungi, ahaaaa roho imeniuma sana na nimelia sana na hadi leo hii namlilia mtoto yule masikini hakuona lolote duniani zaidi ya mateso hakumuona mama wala baba wala bibi wala babu! roho yangu binafsi namlilia sana Nasra alikuwa na umri sawa na mjukuu wangu Maria mtoto wa Kenny; nilifurahi alipopelekwa hospitali na nikawaza rohoni kuwa nikirudi tz nitaenda kumuona ama vipi nimchukue nikae nae, lakini Mungu amempenda sana Nasra kwa kumtoa hadharani watu wamuone na wawajua wanaongamiza maisha yake kabla ya kwenda kuungana na mama yake peponi! Mungu amlaze usingizi wa milele wa amani na furaha ya milele na malaika mbinguni! AMINA. Mwisho natoa wito! natoa la mgambo! chonde chonde watoto kama hamuwataki au mmeshindwa kuwalea wapelekeni kwa bibi zao huko watakula mlenda, korosho, maziwa, kunde nk watakuwa wakubwa kama nanyi mlivyolelewa mkawa wakubwa!
Nahitimisha kwa kutoa pole kwa familia ya George Tyson. Pia kwa bibi na babu wa Nasra! beautiful Nasra!
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA! AMINA
MAMA BISHANGA NA BABA.
Ohio/ USA
No comments:
Post a Comment