Friday, June 27, 2014

MBUNGE : JIMBO KWANZA, CHADEMA BAADAYE




Siku moja baada ya Mbunge wa Mpanda Mjini, Said Amour Arfi (CHADEMA) kushangaza kambi ya upinzani kwa kupiga kura ya kuunga mkono Bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2014/2015, mwenyewe amesema amefanya hivyo kwa ajili ya jimbo lake na si kutanguliza maslahi ya Chama chake kama wafanyavyo wabunge wengine.

Arfi aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa na nafasi hiyo kujiuzulu mwaka huu, aliunga mkono bajeti hiyo akiwa ni miongoni mwa wabunge wanne wa upinzani na kusababisha kushangiliwa kwa nguvu na wabunge wa CCM.

Akizungumzia kilichomfanya kupiga kura ya
kuunga mkono bajeti ya Serikali Arfi alitoa sababu kadhaa ambazo ni pamoja na kuridhishwa na serikali katika kutatua kero nyingi za jimboni kwake pamoja na Waziri wa Fedha, Saada Mkuya Salum kutatua kero za muda mrefu.

“Nikiwa kama Mwakilishi nina mambo matatu makuu ya kusimamia pamoja na kuwasemea watu, la kwanza ni Jimbo langu, pili Nchi yangu na tatu Chama changu (CHADEMA). Katika haya matatu kwa bajeti hii niliamua kwa ajili ya jimbo langutofauti na wengi wanaotanguliza vyama vyao kuliko majimbo na nchiyao,”alitetea uamuzi wake wa kuunga mkono Bajeti hiyo.

No comments:

Post a Comment

bila kutumia lugha ya matusi na kumharibia mtu siku
yake